Unajua kuna tofauti ya Askari wetu kukamata Mwafrika, Mzungu na Muhindi?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Wengi hawafahamu hili lkn lina mizizi yake tangu Ukoloni ni kwamba kuna tofauti ambavyo Polisi wanafundishwa jinsi ya kukamata Mhalifu, kwa mfano Polisi wetu hawawezi kumpiga tangayika jeki Mzungu au Muhindi bali tanganyika jeki ni kwa ajili ya mtu mweusi tu!
Hii ina historia ndefu tangu Ukoloni, jiulize ni kwa nini inaitwa tanganyika jeki na siyo Tanzania jeki!

Mtanzaia akipigwa tanganyika jeki!
MMGL3103.jpg

Juakali akipigwa tanganyika jeki!
upload_2016-10-24_19-43-54.jpeg

Mzungu akimatwa kistaarabu kabisa na Askari wetu!
images

Tanganyika jeki Kenya!
bmwangi.jpg
 
Kwa kijana wa mtaani bila jeki hatofika kituoni

Na hiyo ndiyo shida tuliyonayo, Wazungu wamewekeza miaka zaidi ya 100 kutuaminisha kwamba sisi ni tofauti na Binadamu wengine na kwamba tunahitaji kubaguliwa, na ndiyo maana unaamini hivyo, si ajabu hata pia unaaamini kabisa mtoto wako ni lazima aadhibiwe na kupigwa viboko kama mbwa mwizi kwa kuwa yuko tofauti na binadamu wengine, lkn laiti ukipewa mtoto Mzungu au Muhindi umlee hata awe mtukutu hauwezi kumpiga viboko kama utakavyompiga mtoto wa Kiafrika, hiyo inaitwa chuki binafsi yaani unajichukia wewe mwenyewe!
 
Hapo kinachoangaliwa ukoje ukoje, sio kila mwafrika anabebwa juu juu.

Mfano mzuri ni sugu, hakutakiwa atolewe vile bungeni hasa ukizingatia wadhifa wake na eneo alipo, lakini sababu alijifanya ni imara zaidi akatolewa kwa stail ile.
 
Na hiyo ndiyo shida tuliyonayo, Wazungu wamewekeza miaka zaidi ya 100 kutuaminisha kwamba sisi ni tofauti na Binadamu wengine na kwamba tunahitaji kubaguliwa, na ndiyo maana unaamini hivyo, si ajabu hata pia unaaamini kabisa mtoto wako ni lazima aadhibiwe na kupigwa viboko kama mbwa mwizi kwa kuwa yuko tofauti na binadamu wengine, lkn laiti ukipewa mtoto Mzungu au Muhindi umlee hata awe mtukutu hauwezi kumpiga viboko kama utakavyompiga mtoto wa Kiafrika, hiyo inaitwa chuki binafsi yaani unajichukia wewe mwenyewe!
Unanipangia cha kuamini? Suala halina utata kabisa umkamate kibaka hana id hana lolote halafu mwambie uko chini ya ulinzi twende wapi sio tz hii hatofika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom