Unajua kumuonesha mpenzi wako kama unampenda?

Soja p

Senior Member
Aug 24, 2017
190
223
Kwa upendo wao wote, kwa nguvu zao zote, na uzuri , mahusiano ni kama mmea ambao unahitaji kumwagilia maji na kuwekewa mbolea na kupata jua la kutosha ili uweze kunawiri vizuri

Sababu kubwa ambayo watu hukosa kujua kama wanapendwa ni kutohisi upendo. Kwa nini? Kwa sababu hata kama wanasema I love you mwisho wa kuongea kwenye simu au kabla ya kwenda kazini, hayo maneno hayana miujiza bila ya kuwa na mengine yalio rahisi .

Kuna vitu vidogo vidogo sana vinavyoonyesha upendo na kumfanya mtu ajisikie kupendwa.

1.Usisahau kumkumbatia kabla ya kusema kwa heri. Uelewa wa kimwili ni wa muhimu kuliko maneno

2.Mwambie jinsi alivyo muhimu kwako. Hii huenda zaidi ya neno i love you.

3.Express understanding panapohitajika kusema. Nimeelewa unachokisema. Kama hujaelewa elezea, kwa kusema hivi , Niambie jinsi unavyojisikia ili nikuelewe.

4.Sema mara nyingi jinsi unavyomkubali anapokuwa amefanya jambo kwako.

Husband and wife in park

5.Mwambie jinsi gani unafurahia vipengele vya upekee wake. Kwa mfano , napenda uchangamfu wako, mpongeze.

6.Toka nae siku nzima bila ya kusema kitu chochote zaidi ya kumsifia.

7.Mnunulie chakula anachokipenda bila yeye kusema.

8.Msaidie kupika

9.Kama mna watoto wapeleke kutembea, ili kufurahia michezo ya watoto ili kumwacha awe peke yake kwa utulivu.

10.Tuma ujumbe wa kimapenzi kwa mwenza wako bila sababu .

11.Mtumie email wakati yuko kazini ili kujua anajisikiaje.

12.Mpigie wakati akiwa break kusema tu hujambo

13.Karibia gari, meza, au kochi na umshike mikono yake japo kwa muda kidogo.

14.Mvutie kiti anapotaka kukaa au mfungulie mlango anapotaka kutoka au kuingia.

15.Kumbuka kumpa tabasamu, sio fake, lile ambalo umetunza kwa ajili yake .

16.Badala ya kumweleza jinsi ulivyokuwa na siku mbaya kazini, mwambie kuwa siku hio ulihitaji kuwa na yeye kwa sababu…au nimekuwa na siku mbaya nahitaji unikumbatie.

17.Fanya utani na ucheke nae

18.Nendeni kulala kwa wakati mmoja, ongeeni pamoja au kama kusoma msome pamoja au kama kutulia kwa muda fanyeni pamoja.

19.Kama una watoto mpongeze mwenza wako mbele yao. Watoto watafurahi pia.

20.Mkumbatie mbele za watu, ingawa ataona aibu lakini atafurahia.

21.Tafuta njia nzuri za kuambiana badala ya I love you

22.Muwe na tabia ya kutoka japo mara moja kwa wiki kama mkiweza

23.Mpe zawadi

24.Mpeleke movie

25.mpe massage bila sababu au kwa ajili ya kazi nyingi

26.Mwambie kuwa yeye ni rafiki yako

27.Usiogope kumshirikisha hisia zako, Ni vizuri kufahamu kama una furaha au huna furaha wakati huo na kwa nini

28.Sikiliza anapokuambia jinsi anavyojisikia

29.Kumbuka kila mara unapoweza nunua kitu kidogo kwa ajili yake.

30.Andika ujumbe mdogo wa kimapenzi na kuacha sehemu ambapo atafika

31.Mshike mikono yake mbele za watu

32.Mpate fundisho pamoja, halijalishi ni aina gani

33.Omba msamaha unapokosea

34.Wakati mwingine yeye awe sahihi

35.Mcheze game pamoja

36.Mpe nafasi anapohitaji hivyo.lakini afahamu kuwa upo kama atakuhitaji

37.Mchemshie maji ya kuoga anapokuwa na stress

38.Mwoshee gari yake

39.Jaribu kufanya kitu cha wema kila siku kwa ajili yake

40.Jaribuni kufanya kitu kipya pamoja. Changamoto moja ni bora

41.Mwache alale miguu pako

42.Mtengenezee breakfast, kama inawezekana mpelekee kitandani

43.Mkumbushe kuwa yeye yuko hot au sexy

44.Mkatembee kwenye hewa nzuri pamoja

45.Mnaweza kuvaa nguo za kufanana mnapotoka kupunga upepo

46.Mjitolee pamoja

47.Mtengeneze nywele zake

48.Muweke lengo kama wanandoa, kwa ajili ya fitness, finance, na personal growth

49.Kusafiri pamoja

50.Mpe compani anapoenda mpirani, kwenye game na uwe mmoja wao

51.Chukua muda wa kuwajua rafiki wa mwenza wako

52.Mwache atoke peke yake wakati mwingine

53.Mwekee nyimbo anazozipenda na mcheze pamoja

54.Usiwe serious sana, uwe mcheshi wakati mwingine

55.Mwimbie nyimbo anazopenda

56.Mwambie unampenda zaidi ya jana

57.Kama una siku mbaya , sikiliza kila unachotaka kusema

58.Mwambie kuwa anavutia kuliko wakati mliokutana mara ya kwanza

59.Mwambie unamfikiria kila mara

60.Mwambie kuwa unamsaidia kwa kuwa umemwelewa

61.Mwambie unapenda mwili na akili yake

62.Mwambie unachokifurahia siku hio. Na jinsi gani kinakukumbusha kuhusu yeye.

63.Siku yako imeendaje leo

Kila ukiamka mwambie habari za asubuhi kila siku

65.Kila siku ukitaka kulala mwambie usiku mwema

66.Hakikisha anafahamu kuwa yeye ni namba moja kwako

67.Mwonyeshe kuwa unamuheshimu kwa kusikiliza mawazo yake kwenye maamuzi muhimu

68.Onyesha kukubali alichokifikiria na kukiamua hata kama unaona kabisa hukubaliani nacho.

69.Mwambie akuchagulie nguo za kuvaa kazini

70.Nendeni gym pamoja

71.Mnunulie kadi bila sababu , hata kama hakuna sikuku

72.Tamani kumkiss kila mara

73.Mwambie kuwa umepata bahati ya kuwa na yeye na kuwa umebadilika tangu ukiwa nae

74.Kuwa mkweli . mfahamishe makosa uliyoyafanya

75.Kuwa mpole kwake kwa sababu mwanamke ni laini

76.Mwonyeshe kuwa unamwamini ili nae awe wazi kwako

77.Pigeni picha pamoja

78.Fanyeni mambo ya kijinga pamoja

79.Alika familia yake kwenye chakula cha jioni

80.Mwombe mwenza wako mshirikishane ndoto zenu

81.Cheka anapotania,hata kama utani huo hauchekeshi


82.Uwe rahisi ili aweze kukupenda. Utagundua kuwa kumbe ni mkarimu na ana wema.


Kwa hisani ya Lizz David


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mda wa kufanya yote hayo unatoka wapi maisha yenyewe haya mnaonana mda kulala na kulala
 
Hii ndio bongo lendi, badala ya kupiga kazi ka kujiingizia kipato sisi wenyewe na taifa kwa ujumla sisi tunajadili malavidavi.. aise poleni viongozi wangu kwa kaz ngum

Sent using Jamii Forums mobile app
Kichwa Cha Habari kilielezea Kiini cha kilichomo ndani na Wala Akikuzungumzia Kuuza Mpunga Wala Kulima Maindi Wewe wa Kupiga Kazi Uliifungua Na Mpka Ukaweka Mchango Wako Ili iweje!?

Hii Forum Ina Nyuzi Na Majukwaa Kibaoo, Na Kila Jukwaa Ina Vitu na Mambo Yake We Unaetaka Ishu Za Biashara Si uende Jukwaa La Biashara Uko Ukajifunze, Unaetaka Kupiga Kazi Si Uende Jukwaa la kazi Uko Ukaajiri Watu Uku Unafata Nini Sehemu Ambayo Aiendani Na Wewe....

Ata Mola Aliamua Kuweka Aya Mambo ya Mahusiano Alijua Kabisaa Kuwa Mtafanya Kazi Mtaangaika na Dunia Ila Kuna Wakati Na Muda Utafika Wa Wewe Kutulia na Unaempenda Ili Kusawazisha Misuli na Ubongo wako Ili Kesho Ukatafute Tena...

Ao Viongozi wenyewe Ikifika Muda Wanajifungia Chumbai Na Wake Zao...
 
Kichwa Cha Habari kilielezea Kiini cha kilichomo ndani na Wala Akikuzungumzia Kuuza Mpunga Wala Kulima Maindi Wewe wa Kupiga Kazi Uliifungua Na Mpka Ukaweka Mchango Wako Ili iweje!?

Hii Forum Ina Nyuzi Na Majukwaa Kibaoo, Na Kila Jukwaa Ina Vitu na Mambo Yake We Unaetaka Ishu Za Biashara Si uende Jukwaa La Biashara Uko Ukajifunze, Unaetaka Kupiga Kazi Si Uende Jukwaa la kazi Uko Ukaajiri Watu Uku Unafata Nini Sehemu Ambayo Aiendani Na Wewe....

Ata Mola Aliamua Kuweka Aya Mambo ya Mahusiano Alijua Kabisaa Kuwa Mtafanya Kazi Mtaangaika na Dunia Ila Kuna Wakati Na Muda Utafika Wa Wewe Kutulia na Unaempenda Ili Kusawazisha Misuli na Ubongo wako Ili Kesho Ukatafute Tena...

Ao Viongozi wenyewe Ikifika Muda Wanajifungia Chumbai Na Wake Zao...
Umeona ee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mafrika kumuonyesha mwenza wake anampenda anahisi amejishushia heshima..kuna njia nyingi za kuonyesha upendo na majukumu yako yakaendelea kama kawaida bila kuathili chochote.
 
Haswaaa ila inapendeza nyote mkiwa mnafanya sio mm ndo nifanye tu

wanawake wengi hayo tunafanya ila upande wa pili mmh kidogo sana.

Anyway nakumbuka baadhi ila no I4 nimeikumbuka zaidi. Maana wengine hachelewi kusema " nishatoa lock shuka au ingia ahaaa"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom