Mr Slim
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 1,875
- 3,354
Upo sahihi kwenye jogoo kucheza na muda,hakosei.Mkuu wiki iliyopita nilikuwa mkoani kumtembelea Babu, Sasa nikalala kwa hofu ya kupitiwa usingizi nisije kuachwa na bus maana nilishakata tiketi.
Tukalala, usiku nilishtushwa na sauti ya jogoo anawika kabla ya kuwasha simu yangu nikamuuliza Babu kumekucha niamke nijiandae?
Babu akajibu hapana muda bado sasahivi ni saa Tisa, kuangalia simu yangu kweli Ni saa tisa kamili ya usiku. Akasema jogoo wake huwika saa Tisa na saa kumi na moja Tena kamili. Nilishangaa sana jogoo anajuaje??!!
Mtaani kwetu yalikuwa yapokezana ikifika mida yao kuwika kama wanapiga stori au kupeana taarifa.aisee hata uwe mvivu unaamka.
Halafu kuku ukiwa unarudi home jioni kwa mguu unakuta kundi la kuku ambao ni wako, wako nyuma yako toka mbali ufungue geti nao waingie.wanakariri sura.