Unajisikiaje ukikutana na mpenzi wa zamani?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506
Wakuu habari,

Katika mapenzi kunakuwa na utamu hasa pale penzi linapoanza ila penzi hilo huwa shubiri pale tu wawili hao wanapoachana.

Yawezekana ikawa kwa mwanamke kumuacha mwanaume ila maranyingi wanaume ndio wanaacha sana.

Pia kuna sababu nyingi tu zinazoweza kupelekea wapenzi hao kuachana na moja wapo ni uaminifu.

Sasa leo nataka kusikia kwa wanaume na wadada ambao waliowahi kupitia hayo.

Mimi binafsi sipendi kuonana na mpenzi wa zamani kwakuwa nakumbuka unyau aliyonifanyia.

Doncute
 
Niliwahi kukutana na demu wangu wa zamani baada ya yeye kunitema tena kwa haibu kubwa. Alipokuwa na mimi pia alikuwa na uhusiano na jamaa fulani ambaye ni muhasibu sehemu hivi hapa mjini. Demu baada ya kujua jamaa ana hela za wizi zisizoisha alikuwa na dharau sana kwangu tena alianza ghafla tu. Siku namtuata kazini tukale lunch nakuta kakumbatiwa na jamaa baada ya kuniona acha anitukane mbele ya yule jamaa na rafiki zake, sikuamini masikio na macho yangu.Niliumia sana na ilinichukua muda kumsahau japo ilipoteza network yangu for a while na nikawa sina hamu na mademu for that period. Mungu mkubwa jamani, baada ya miaka 3 nikaja kumuona katika mazingira ya kusikitisha. Demu alikuwa mze kupindukia yaani kama ni stress za maisha basi kweli zilimla mno. Demu aliniomba msamaha turudiane na yuko radhi anipe ninachotaka nikamwambia niko na wife kwa sasa. Kwa ujinga wake eti akataka nimpeleke nyumbani akamsalimiei wife, sikumkubalia. Kumbe demu aliachika toka kwa jamaa na kazi alifukuzwa na alikuwa hana pa kukaa hapa mjini anakaa geto na marafikize, alikuwa anajiuza usiku pale Kinondoni kwa Manyanya. Mwezi wa tano mwaka huu nikamuona tena mjini anatisha kama zimwi fulani hivi, aliponifuata tu kutaka kampani nikamwambia asinifuate naenda kwa wife akazidi kufuatana tu nami. Nikafika sehemu nikamkimbia.
 
Me kuna demu alinambia haiwezekani nimuache kirahisi rahisi hivyo must atanifanyia kitu mbaya daah!!
 
Back
Top Bottom