Unajisikiaje pale mtu akikupa au kupokea kwa mkono wa kushoto?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,378
26,700
Salama waungwana!

Hii dhana ina maana gani?

Nimekuwa nikiona na kusikia wanajamii kuhusu jambo hili, wewe pia bila shaka umewahi kusikia na pengine kufikiria na pengine hadi kupata majibu.

Binafsi nimekuwa sijali sana kuhusu hilo, lakini kuna nyakati nimekutana na vizuizi nikitumia ‘kushoto' au kuonekana 'mimi' wa ajabu!

Hebu tusaidiane hili, kuna nini cha tofauti zaidi katika mikono hii kushoto na kulia katika kutoa ama kupokea?

Je, ni imani, ni ubaguzi tu wa viungo, ni mgawanyo wa majukumu au ni kitu gani hasa?

Let alone wale naturally left handed, japo nao wamekutana na vipigo sana tu hasa utotoni nyakati za kula chakula.

Karibuni.
 
Dhana hii ni pana sana mkuu. Ila kidini "UPANDE WA KULIA" una thamani yake. Mfano hata Yesu alisema anakaa upande wa 'kuume' au kwa kiswahili rahisi ni upande wa kulia.

Dhana hii imepelekea hata sisi wengine
Nb nimeelezea kwa wakristo .
Sijajua kwa waislamu

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakupata vema mkuu, upande wa kuume/kulia huo ni 'upande'.... hoja mezani ni mkono.

Na kwa mfano wako huo basi, kama maana ya 'kuume' ni heshima... vipi wanawake ambao waliumbwa kwa ubavu wa kushoto, au ndo asili ya mfumo dume na ubaguzi kijinsia?
 
Kaka hapa umeniweza labda kama kuna mtu aweza nitetea hoja hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nadhani kuna ishu mbili(kwa ufahamu wangu) kulingana na changamoto ambazo nami pia niliwahi kuzipata.
1. IMANI.
Kuna watu wanaamini tofauti kwa matumizi ya mkono wa kusho. Mfano, kulipa/kutoa/kupokea pesa kwa mkono wa kushoto wanaamini kuna ushirikina nyuma ya pazia. Labda unatumia ushirikina katika utafutaji wako ikiwemo mambo ya chuma ulete.
2. MATUMIZI YA MKONO KATIKA MAISHA YA KAWAIDA.
Nimewahi kukutana na watu fulani wakiamini baadhi ya vitu hutakiwi kufanya kwa mkono wa kushoto. Mfano kupika. Hii inatoka na kutumia mkono wa kushoto kwenye kujisafisha chooni baada ya kujisaidia.
 
Nakupata vema mkuu, upande wa kuume/kulia huo ni 'upande'.... hoja mezani ni mkono.

Na kwa mfano wako huo basi, kama maana ya 'kuume' ni heshima... vipi wanawake ambao waliumbwa kwa ubavu wa kushoto, au ndo asili ya mfumo dume na ubaguzi kijinsia?
Hata jeshini, mkuu anakuwa kulia. Ili apige na kupokea salute. Sijui kuna uhusiano gani Kati ya kulia na heshima
 
Salama waungwana!

Hii dhana ina maana gani?

Nimekuwa nikiona na kusikia wanajamii kuhusu jambo hili, wewe pia bila shaka umewahi kusikia na pengine kufikiria na pengine hadi kupata majibu.

Binafsi nimekuwa sijali sana kuhusu hilo, lakini kuna nyakati nimekutana na vizuizi nikitumia ‘kushoto' au kuonekana 'mimi' wa ajabu!

Hebu tusaidiane hili, kuna nini cha tofauti zaidi katika mikono hii kushoto na kulia katika kutoa ama kupokea?

Je, ni imani, ni ubaguzi tu wa viungo, ni mgawanyo wa majukumu au ni kitu gani hasa?

Let alone wale naturally left handed, japo nao wamekutana na vipigo sana tu hasa utotoni nyakati za kula chakula.

Karibuni.
FYI... Ustaarabu huu ni miongoni mwa Tabia zilizojengwa itikadi za Dini.... na walioleta ni WAARABU ktk kuwafundisha wakazi wa pwani ya Afrika Mashariki mwenendo wa hadhi kati jamii....
 
Binafsi natumia mkono wa kushoto lakini sijawahi wala siwezi kumpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto. Huwa napata tabu pale mtu anaponipa kitu ama kunirudishia hela kwa mkono wa kushoto huwa nahisi kuwa amenidharau kwa kiwango cha mwisho.
Mwanzoni nilikuwa hata kama mtu akinipa kitu au akipokea kwa mkono wa kushoto nilikuwa napokea kwa mkono wa kulia wala sibadilishi lakini kwa sasa nimejifunza mambo mawili:

1. Mtu nikiwa nampa kitu akiwa anataka kupokea kwa mkono wa kushoto na mimi nabadilisha mkono nampa kwa mkono wa kushoto.
2. Mtu akiwa ananipa kitu kwa mkono wa kushoto nami napokea kwa mkono wa kushoto.
 
Binafsi I don't mind ila huwa najishtukia nikimpa mtu mwingine kitu kwa mkono wa kushoto, haswa nisiyefahamiana nae kwasababu tu anaweza akawa offended.

Ila kwangu fresh tu.
 
Back
Top Bottom