Unajisikiaje pale mtu akikupa au kupokea kwa mkono wa kushoto?

Salama waungwana!

Hii dhana ina maana gani?

Nimekuwa nikiona na kusikia wanajamii kuhusu jambo hili, wewe pia bila shaka umewahi kusikia na pengine kufikiria na pengine hadi kupata majibu.

Binafsi nimekuwa sijali sana kuhusu hilo, lakini kuna nyakati nimekutana na vizuizi nikitumia ‘kushoto' au kuonekana 'mimi' wa ajabu!

Hebu tusaidiane hili, kuna nini cha tofauti zaidi katika mikono hii kushoto na kulia katika kutoa ama kupokea?

Je, ni imani, ni ubaguzi tu wa viungo, ni mgawanyo wa majukumu au ni kitu gani hasa?

Let alone wale naturally left handed, japo nao wamekutana na vipigo sana tu hasa utotoni nyakati za kula chakula.


Karibuni.
'akikupa'? Akikupa nini wee Semenya wa Ukaldayo?

Mmejikita fikra zenu kwenye uchawi uchawi tuu
 
Binafsi I don't mind ila huwa najishtukia nikimpa mtu mwingine kitu kwa mkono wa kushoto, haswa nisiyefahamiana nae kwasababu tu anaweza akawa offended.

Ila kwangu fresh tu.

Binafsi I don't mind ila huwa najishtukia nikimpa mtu mwingine kitu kwa mkono wa kushoto, haswa nisiyefahamiana nae kwasababu tu anaweza akawa offended.

Ila kwangu fresh tu.

Nyie watu nimewakubali sana, mna mawazo sio tu yanafanana bali mnawaza kitu kimoja.... hongereni sana.
 
Ni imani tu hizo. Kumbuka yote ni mikono tu. Aliyeumba hii mikono hakuipa sheria hiyo na matumizi yake.
 
Ni unyanyasaji kwa watu wanaotumia mkono kushoto embu wewe unaetumia kulia jaribu kujilamisha kutumia mkono wa kushoto uone inavyoumiza
 
Back
Top Bottom