Unajisikiaje kuwa na mwanamke mwenye 'Wigi'

Kwanza mwanamke anayevaa wigi kisaikolojia ana matamanio ya kuwa mwanamke anayeakisiwa na wigi alilolivaa.

Sasa unaanzaje kumfukuzia mwanamke anayetamani kuwa kama mhindi, mzungu au msomali wakati kuna wahindi na wazungu kibao tunabanana nao hapa hapa?..
 
Nawaambiaga sana dada zangu kuwa mambo wanafanya wakidhani wanapendeza machoni kwa wanaume kumbe ndo wanatuchukiza mno
1.Kuvaa mawigi
2.Kucha bandia
3.Kope bandia
4.kujichubua
5.LIPSTICK
6.KUACHA MAPAJA WAZI

hivi vitu huwa vinanikera mno, sijui ni nani aliyewaambia wakiwa wasafi tu wa kawaida hawatongozwi
yaani hata marashi tu mtu anajipulizia utadhani anajiandaa kuzikwa ukikaa mita nne toka alipo tayari ushapata kipanda uso, warembo wa hivyo nakaa nao mbali kabisa
 
Wamekua brainwashed kwamba wanawake wenye nywele refu na laini ndio wazuri na wao wenye nywele ngumu za kipipili sio wazuri, mwanamke anapaswa kujiamini na kujikubali jinsi Mungu alivomuumba, kama mzuri ni mzuri tu, unaweza vaa wigi original la laki 5 na bado usivutie.
 
👊
 
Halafu hawajui tu! Mbona nywele ukizitunza shampoo kidogo, zikila na ufuta wa nazi mbona zinakuwa shega tu.

Kingine kinachokera wanajichubua mpaka bhasi! Na kuna wale wa manukato makali umbali wa mita 6 tayari umeshaanza kuyanusa.

Yaani wamezidi! wamekuwa kama majini, na mikucha yao ndiyo usiseme.

Na mi' make up yao bora tuhamie Neptune! Uso umejaa jaa mimng'ao kama vitumbua vilivyochomwa na mafuta mengi.
 
Back
Top Bottom