Unajifunza nini kutokana na kisa hiki!?

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kipindi Hitler alipokuwa madarakani, alifanya jambo moja ambalo liliwashangaza maafisa wake. Siku hiyo alikuja kwenye mkutano akiwa ameshikilia kuku mmoja mkononi. Mara akaanza kuvuta (Kunyonyoa) manyoya yake moja baada ya moja.

Kuku alilia kwa maumivu, damu zikitiririka kutoka kwenye zile sehemu zilizotolewa manyoya yake.
Kwa kweli yule kuku alikuwa kwenye maumivu makali sana.

Licha ya kilio cha yule kuku, lakini Hitler aliendelea bila huruma kukwanyua unyoya baada unyoya hadi kuku akabakia bila hata unyoya mmoja.

Baada ya kumaliza ndipo alipomwachia yule kuku kwa kumtupa chini, kisha akatoa mfuko wa chakula cha kuku na kuanza kumtupia yule kuku chakula.

Yule kuku maskini bila ya kufikiria au kutafakari alianza kudonoa kile chakula huku akifata mweleo wa Hitler alipo. Yule kuku alimfuata Hitler mpaka alipokuwa ameketi kisha akasimama chini ya miguu yake akiendelea kula kile chakula kutoka kutoka kwenye mkono wa Hitler.

Kisha Hitler aliwaambia wajumbe wa chama chake...

Kuku huyu anawakilisha watu, kwanza ni lazima uwafanye wanyonge, kwa kuwaondolea uwezo wa kiuchumi na kujiwezesha, kisha wafanyie unyama kwa kuwapiga na kuwatesa. Ukisha wafanyoa yote hayo ndipo uwape chakula wakiwa katika hali hiyo ya unyonge na kukata tamaa. Watakufuata tu kama vipofu kwa muda wote wa maisha yao na watakusifu kuwa wewe ni mtu shujaa na mwenye huruma sana juu yao. Watakuwa washasahau kwamba, ni wewe ndio ulio wasababishia madhira hayo yote. Na kuku atakaye kumbusha wenzie mchinje.

- Je umejifunza nini kutokana na kisa hiki!?

The best gift is knowledge

TAFAKARI CHUKUA HATUA!!
 
Kwa hiyo mkuu unataka utuambie kuwa kutokuongeza mishara, miaka mitano bila kutoa ajira, na mambo mengi yaliyoshamili katika awamu ya tano, zilikuwa ni mbinu za kutengeneza sinagogi za kumwabudu binadamu mwezetu.
 
Wewe ni mwongo mkubwa na ningekushuri kuuondoa uzi wako. Nimeishi na kusoma ujerumani zaidi ya miaka 35 hivi sasa na nimesoma na kusikiliza stories tofauti za Hitler, lakini Story kama hii sijawahi kuisikia na kuisoma kwokote kule. Wawe naona umejawa na fantasy ambayo haieleweki.

Hitler mwenyewe humjui na mambo aliyo yafanya huyajui, lakini kuandika uongo mitandaoni kuhusu matendo ya mtu hilo unliweza. Acha uongo na ona aibu!
 
Umesema ulisoma stories tofauti za Hitler ila siyo Stories zote siyo?
 
Wewe ni mwongo mkubwa na ningekushuri kuuondoa uzi wako. Nimeishi na kusoma ujerumani zaidi ya miaka 35 hivi sasa na nimesoma na kusikiliza stories tofauti za Hitler, lakini Story kama hii sijawahi kuisikia na kuisoma kwokote kule. Wawe naona umejawa na fantasy ambayo haieleweki.

Hitler mwenyewe humjui na mambo aliyo yafanya huyajui, lakini kuandika uongo mitandaoni kuhusu matendo ya mtu hilo unliweza. Acha uongo na ona aibu!
Miaka 35 umesoma ujermani halafu leo hii upo hapa jf unapiga umbea? Jipige kifuani na useme kwa sauti MIMI NI KENGE...

Nalog off...
 
Hitler hakuwa na muda wa kucheza na kuku na kumpa chakula. Unamjua vizuri au.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom