Unajifunza kiigereza na ungependa 'kuota kiingereza'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unajifunza kiigereza na ungependa 'kuota kiingereza'?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by theophilius, Sep 1, 2012.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaojifunza lugha ngeni, mf. Kiingereza, kwa vyovyote vile hawewezi kuimudi iwapo hawatafanya mambo yafuatayo: kusikiliza, kuongea, kusoma, na kuiandika kwa lugha hiyo ngeni. hii ni kwa mujibu wa waalimu wa lugha.
  Hata hivyo nimekuwa nikifikiria, ikiwa unaweza kuongeza, KUOTA kwa lugha hiyo ngeni, ili isaidie kuifahamu/kuimudu zaidi, ikikumbukwa kwamba hapo lugha itakuwa inajichimbia zaidi katika bongo ya anayejifunza, kwani si tunaota ndani ya bongo zetu!.

  Sasa swali linaweza kuwa ufanyeje uweze KUOTA kwa Kiigereza kwa mfano! fuatilia maelekezo haya, ujue kumbe hata wewe unaweza kuota kwa kiingereza, kwa maana nyingine hata kama kiingereza kinakataa kuingia kwenye bongo yako, lazimisha kwa 'kugandamizia'

  Binafsi sikuwahi kusumbuliwa na swali hili, kiasi cha kutaka kufanya utafiti, maana nilijua kuwa haiwezekani, mtu kupanga uote nini, achilia mbali kwa lugha gani.

  Kwa vyovyote ikitokea ukaota, maana si mara zote unapolala unaweza kuota, utaota kwa lugha ile unayoifahamu vizuri, mfano kinyambo au kinyakyusa, ikiwa wewe ni mtu uliyejifunza kiswahili shule ya msingi, au waweza kuota kwa kiswahili na hata kiingereza kama unamudu na unatumia lugha hizo barabara, au kwale ambao, kwao lugha ya 'mama' ni lugha hizo, hawakubahatika au wanaona aibu kutumia lugha asili- wao wanaita kilugha.

  Kwa bahati tu, kama ilivyotokea kwa yule mwanasayansi nguli (mnamfahamu) ambaye aligundua 'principal of gravitation - mvutano wa dunia' alipokuwa amejipumzikia chini ya mti wa matunda, mara tunda lililoiva likadondoka na kumpiga usoni/kichwani.

  Badala ya kuamka na kujiendea zake, kama wengi ambavyo tungefanya, tunasimuliwa kwamba baba wa sayansi huyo, kuanzia hapo alianza kujiuliza kwa nini hilo tunda lilipomong'onyoka toka mahali pake kwa nini halikupaa mbinguni, na badala yake likaanguka chini, akaingiwa wazo ambalo alilifanyia utafiti na hatimaye kubaini kwamba kuna mvutano chini ya ardhi.

  Hata mimi bwana,.. nimewahi kuwachekesha wenzangu ofisini kwamba nimeota hili na lile.. kumbe ni kweli limetokea, na ninapohakikisha kwenye magazeti ya siku ile nakuta kweli limetokea na hivyo kushangaa inakuwaje naota habari hizo zinazokuwa magazetini.

  Hata hivyo nilikuja kugundua kwamba huwa naziota zinapokuwa zinatangazwa redioni kwenye kipindi cha 'tuzungumze magazeti' maana nina tabia ya kuamka na kuwasha redio kisha kulala tena hivyo magazeti yanapotangazwa sisikilizi - maana si ninakuwa nimelala - lakini naota karibu kila kitu kinachotangazwa - ajabu eh.

  kilichonistaajabisha siyo kwamba, naota nasikiliza redio, la! naota kwa mfano rafiki yangu amon ananipa michapo kwamba unajua, kuna mtu kauawawa na polisi kwenye maandamano ya chadema, na ananipa dondoo zote za tukio kama ilivyo kwenye magazeti yaliyosomwa.

  Sasa juzi ilitokea nikasaahu kuzima tv, na mara ya mwisho nilicha chaneli ya BBC ndiyo iko hewani, nilipolala, wacha niote karimu matukio yote yaliyotangazwa na BBC usiku huo nikiwa nimelala, tena siyo kwamba kuna mtu, mswahili ananisimulia, bali mimi mwenyewe niko huko naongea na watu mbalimbali wananipa michapo ya matukio hayo. unajua ni kwa lugha gani? Kwa kiingereza si ndiyo, ilikuwa inatangazwa.

  asubuhi nusura nishangae inakuwaje naota kiingereza ambayo ni lugha yangu ya tatu baada ya kiswahili! ndo nikagundua kwamba nilisahau kuzima TV na kweli BBC ndiyo walikuwa hewani, na baada ya kufuatilia, si unajua huwa wanarudiarudia habari zao, nikagundua matukio niliyoota nashuhudia au naongea na mashuhuda, kumbe yalikuwa yakitangazwa kwenye BBC - ajabu eh.

  basi nawe waweza kujaribu, usizime TV na weka channel ya lugha unayojifunza, kama ni kichina weka CCTV D na kama ni kama ni kiispania unajua utaweka channel gani ikitokea ukaota, endelea baada ya muda unaweza kupima matokeo. na si vibaya tukawasiliana ili kuendeleza/kufanikisha ugunduzi huu.

  Nani kakwambia hakuna cha kugundua dunia hii!
   
 2. b

  babacollins JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 879
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Stop dreaming and start practising.................
   
 3. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,566
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mweeh :eek2:
   
Loading...