Unajali Data Zako ??

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Unaonaje unaposhuka hapo chini gorofani ukakuta HDD iliyobadilishwa katika computer yako juu iko mikononi mwa machinga anaiuza kwa bei chee , tena ina lebo yako kabisa MALKIA X DEAD , taarifa zinasema hiyo HDD Ilikufa au kupata madhara fulani ndio maana imebadilishwa .

Au wakati mwingine unapoenda mahakamani kujitetea na mtu mwingine usiyemjua anakuja na nyaraka ambazo zimetokana na HDD ya computer yako iliyobadilishwa kitambo si unaweza kupata kichaa ? ulifikiri ile imeshakufa , haipotena kumbe ulikosea .

Sasa hivi kila mtu anajitahidi kuficha au kuweka data zake katika sehemu salama , wengine wako busy kutafuta data hizi waweze kuzitumia katika mambo yao , mfano ni huo nilioutoa hapo juu .

Mwaka jana katika ofisi Fulani binafsi tulikuwa na kazi Fulani ya kuuza computer mpya na hizo za zamani zilipelekwa katika achieve ya hiyo office husika ni mbali kidogo na hapo sehemu yenyewe ni dereva wa kawaida tu ndio alikuwa akipeleka kwa usimamizi wa Administration .

Kwa kuwa mimi ndio nilikuwa mtu wa IT pale sikupenda hizi zile computer ziondoke na HDD zake kwa sababu ndio zenye data muhimu hata kama zikiwa formatted kuna tekinologia za kuweza kurudisha zile data na nilishuhudia wakati Fulani komputa moja ikiwa katika office binafsi ya mmoja wa wafanyakazi wale .

Nilichokuwa nafanya mimi ni kuondoa HDD zile na kuacha wapeleke computer peke yake huko zilipopelekwa sikuwa na uhakika nako sana kutokana na sababu hiyo , vile vile ni kufuatilia ile PRIVACY POLICY iliyokuwa ndani ya kampuni husika ile inayohusu data na taarifa zingine za kampuni .

Mwishowe nilikuja kugundua yule kinganganizi aliyekuwa anataka sana zile computer alikuwa na offisi yake amefungua alichokuwa anataka ni kutumia zile data kazi zile computer katika kuleta ushindani na kampuni yake aliyomlea .

Kule kwake zile computer zinaweza kuibiwa zikaingia mikononi mwa watu wengine katika uchunguzi zikaonekana zimetokea kwangu zikaenda kwa huyu kinganganizi ikawa balaa , je nani yuko tayari kuhatarisha DATA za watu ?

Hata hivyo kazi ilimalizika na data ziliendelea kuwa mikononi mwa kampuni husika , huo ni mfano mchache nilioutoa hapo juu .

…………………………………………………………………………………………

Kwa sasa mjini dare s salaam kumetokea vijana wengi wanaouza vifaa vya computer haswa RAM , HDD ,CPU na hata computer zenyewe ukiacha laptops ambazo zimezoeleka lakini zaidi nitaongelea HDD ambako Data za watu hukaa mule na chochote kinaweza kutokea .

Siku moja niliwahi kujaribu tu kwenda sehemu moja kariakoo katika mizunguko yangu nilikutana na vijana Fulani hizo HDD wamezipanga katika meza zinauzwa kuanzia alfu 10 , 20 na 30 kutokana na ukubwa wake hizo sio bei ghali sana , siku hiyo ilinibidi ninunue bwana ili nikaone kunani .

Niliponunua kwenda nazo kuziangalia nikashanga zimetoka sehemu nyeti ya serikali na zina nyaraka binafsi na zingine muhimu za wizara husika , inawezekana hizi hdd ziliandikiwa zimekufa kwahiyo mtu akabadili tu na zile zingine akaenda kuuza

Au inawezekana walienda kutupa katika dustbin wale wazoa taka wakachukuwa wakazifuta na kupeleka sokoni kariakoo , hawa vijana hawajui ni vitu gani hivi hawajui umuhimu wake ndio maana wanauza kwa bei ile na kuzipanga hazarani vile .

Kama unavyoona hapo juu , data za wizara baadhi nimeshazipata mimi , mfano kama kungekuwa na vitabu mule au ripoti muhimu mimi ningeweza kuchukuwa na kuzitumia jinsi ninavyojua au kutaka mimi ikawa balaa kwa wengine .

…………………………………………………………………………………………..

Imefikia wakati sasa wizara na sehemu zingine za serikali kuhakikisha wana PRIVACY POLICY inayohusu DATA na vifaa vingine vya mawasiliano na ziwe wazi sio kwa watu wachache tu , sasa hivi kila mtu yuko busy anataka data kwa ajili ya kufanyia kazi zake .

Wanahabari wanataka DATA kwa ajili ya kuandika magazeti na mambo yao mengine , na mambo kama hayo , watu wasidharau data kiasi hichi wanaziacha wazi mpaka mtu anaenda kununua data ya dhamani kubwa kwa alfu 20 tu .

……………………………………………………………………………………………..

Najua kuna baadhi wa watu nimeona zaidi serikalini ambao wanapenda kufanya kazi na watu mmoja mmoja freelancer katika shuguli zao za kiufundi zinazohusu ICT , unapofanya hivi ujue ni makosa kisheria kwanza huyu mtu mmoja huna guarantee naye wakati wowote anaweza kukimbia au kufanya chochote kile na ni yeye peke yake tu .

Ilitakiwa kutangazwa tender na kampuni mbali mbali zinaomba tender hiyo inayoshinda ndio inafanya shuguli hiyo , katika kampuni kila kitu kinachofanywa kinakuwa na ripoti yake au taarifa yake na utahakikishwa usalama wa data zako na vitu vyako vingine .

Pia katika kampuni hizi wameajiriwa watu wanaojua fani hizi wako katika fani hiyo kwa muda kwahiyo wanajua vingi na wanaweza kusaidia katika mengi , kumbuka wanafanya kazi kama timu mmoja kumbuka KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA .

…………………………………………………………………………………………….

Ushauri kwa techs ambao hufanya shuguli hizi wahakikishe wanaandikishiana mikataba au mkataba na wizara au shirika husika kuhusu kazi na malengo ya wao kuwa katika sehemu husika kumbuka unafanya kazi na data za watu chochote kikitokea ni wewe utayashikwa na kujibu hizo shutuma .

Mfano mimi nilivyoenda kariakoo kununua hiyo HDD ningeamua kutumia zile data kwa mambo yangu halafu baadaye ije kuwa balaa , maana yake atafuatiliwa mtu wa kwanza kabisa aliyetoa hicho kifaa mpaka kupatikana kwa watu wasiohusika .

Bahati mbaya sana kampuni nyingi hapa jijini haswa hizi zenye shuguli za kiufundi hazina pia PRIVACY POLICY kwa ajili yake yenyewe na wafanyakazi wake , wafanyakazi wanaajiriwa bila mikataba , hawajui majukumu yake pale haswa utunzaji wa data na vitu vingine vya wateja ndio maana tunazikuta mitaani .

………………………………………………………………………………………………

Kama inawezekana sasa vyombo vya usalama vianze kuwa macho kuanza kufuatilia nyufa hizi za data kabla ya kutokea balaa kubwa zaidi linalohusu data na vitu vingine vinavyohusiana na DATA ,lazima ifike sehemu sasa hivi vyombo vishirikiane na hizi workshop au wamiliki wa kazi hizi kuweza kutambua changamoto wanazopanda nazo na jinsi wanavyoweza kushirikiana katika kupunguza matatizo haya .
 
mzee nimesoma Thread yako kwa makini na ikanichoma.
Kimsingi ni kuwa hili ni tatizo kubwa sana kwa sasa sio tu kwetu sisi bali hata nchi iliyoendelea kwaninakumbuka kipindi nasoma mambo ya Computer Forensic(Ingawa hili somo haliruhusiwi kufundishwa watu wasio wafanyakazi wizara nyeti)ila huku Uchinani tunapeta tu hata sisi Undergraduate ni special kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye Vyombo vya usalama kama Usalama wa Taifa,CIA,FBI..,yule Mtoa hoja(Ambaye alialikwa na Chuo hapa kwetu) ambaye alijigamba kuwa yeye ndio mwalimu wa maafisa wa FBI,CIA nk alisema kuwa kwa takwimu waliyonayo ni kuwa hadi sasa in USA 48% ya makampuni hayajui kama Data zao zimetumiwa kinyume cha Sheria na 10% wanajua ila hawajui jinsi ya Kuyarudisha so hili suala ni suala nyeti mno,Kwakuwa nina Imani Kwa nchi kama Zetu ni watu wachache mno wenye uwezo wa kufuta Data moja kwa moja toka kwenye Cylinder so njia ya rahisi ni kuwa kwa sasa ifike wakati watu wafahamu kuwa Computer huwa haifuti data kuirahisi kama tunavyozani by(Shift+Delete) au Format,partition..
Mimi ninasoftware ambayo ina uwezo wa kuzichanganya hizo Data from cylinder so kwa mtu ambaye ana knowledge ya kubebabeba ya IT hawezi kuzirecover hizo data kiurahisi so kwa mwenye kuhitaji anaweza kunitumia request ila kwa masharti kuwa lazima atoke Tanzania na awe na knowledge ya IT ili kupunguza matumizi ya Holela. So nimeacha accesslist kwa IP zote zinazotokea Tanzania TU kwa wiki moja ili kuwawezesha kutuma request zenu nitalisten kwenye hiyo port niliyoiacha,(Hii ili kuhakikisha ni wale wenye knowledge tu ndio wanapata access)
TZ-China
 
Hello Wakuu

Katika topic hii ya Unajali data zako..nimeguswa sana na kuhusu utunzaji wa data..wa kuwa mie niko kwenye mambo ya database and software oversee most of my time.

Just a quick question niko na computer nataka niweke restriction katika kua access baadhi ya folder bila kuwa na passoword ya kuingia kwenye folder hizo.Hapa na maana kuwa mimi mwenyewe hata kuingia kwenye folder hizi iwe natumia password.How do i do that?

Kwa mfano kwenye hard drive yako umeweka movie folder hutaki liwe access bila ruhusu yako.Is there any way kuweka password kwenye folder?

Good day

Buswelu
Mwanza
 
Hii thread ni muhimu sana
ninaunga mkono kwa wadau kulinda data zao kwa ushauri wa bure uliootolewa humu
Ila angalizo ni kwa wale walio ktk idara nyeti kutumia mafundi wa mtaani ktk kufanya maintenensi ya pc au systems zao za kiserikali. Na hii imechangiwa na kutojali kwa serikali kwa masuala muhimu nyeti kama haya.
Ila kwa upande mwingine ndo maana ufisadi hauishi kwani wanaopata data hizi wengi huzitumia kinyume......
TZ-China na SHy hongereni kwa posts zenu
 
Hi Njia rahisi zaidi ni ku hide hizo folder hiyo haihitaji programu yoyote ile maalumu , au kama uko shared then unaweza kuset users ukawapa permision na mambo kama hayo

Pia kuna programu za kulock hizo file zako tatizo lake ni kwamba siku computer ikicrash kupata hizo file ni ngumu sana kama ulitumia programu ya kulock kwa sababu hizo permision huweza ku inherit ( hili ni somo refu kidogo )

Mwisho , laptop na computer nyingi siku hizi zinakuja na bios programu ambazo zinaweza kulock harddrive kwa pwd kwahiyo jaribu kuangalia bios yako inauwezo kuwa kulock HDD ??

ahsante
 
mzee nimesoma Thread yako kwa makini na ikanichoma.
Kimsingi ni kuwa hili ni tatizo kubwa sana kwa sasa sio tu kwetu sisi bali hata nchi iliyoendelea kwaninakumbuka kipindi nasoma mambo ya Computer Forensic(Ingawa hili somo haliruhusiwi kufundishwa watu wasio wafanyakazi wizara nyeti)ila huku Uchinani tunapeta tu hata sisi Undergraduate ni special kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye Vyombo vya usalama kama Usalama wa Taifa,CIA,FBI..,yule Mtoa hoja(Ambaye alialikwa na Chuo hapa kwetu) ambaye alijigamba kuwa yeye ndio mwalimu wa maafisa wa FBI,CIA nk alisema kuwa kwa takwimu waliyonayo ni kuwa hadi sasa in USA 48% ya makampuni hayajui kama Data zao zimetumiwa kinyume cha Sheria na 10% wanajua ila hawajui jinsi ya Kuyarudisha so hili suala ni suala nyeti mno,Kwakuwa nina Imani Kwa nchi kama Zetu ni watu wachache mno wenye uwezo wa kufuta Data moja kwa moja toka kwenye Cylinder so njia ya rahisi ni kuwa kwa sasa ifike wakati watu wafahamu kuwa Computer huwa haifuti data kuirahisi kama tunavyozani by(Shift+Delete) au Format,partition..
Mimi ninasoftware ambayo ina uwezo wa kuzichanganya hizo Data from cylinder so kwa mtu ambaye ana knowledge ya kubebabeba ya IT hawezi kuzirecover hizo data kiurahisi so kwa mwenye kuhitaji anaweza kunitumia request ila kwa masharti kuwa lazima atoke Tanzania na awe na knowledge ya IT ili kupunguza matumizi ya Holela. So nimeacha accesslist kwa IP zote zinazotokea Tanzania TU kwa wiki moja ili kuwawezesha kutuma request zenu nitalisten kwenye hiyo port niliyoiacha,(Hii ili kuhakikisha ni wale wenye knowledge tu ndio wanapata access)
TZ-China

Hi Kilongwe mimi nina omba hiyo programu

Ahsante
 


Kwa mfano kwenye hard drive yako umeweka movie folder hutaki liwe access bila ruhusu yako.Is there any way kuweka password kwenye folder?

Good day

Buswelu
Mwanza

Mkuu kama uko katika network na hilo file lako haliko shared ni ngumu kidogo kwa mtu wa pili kuweza ku access labda atumie njia mbadala lakini katika computer hiyo kutakuwa na firewall kwahiyo ni rahisi kuwa blocked .

Lakini kama hilo folder liko shared , narudia ile point ya kwanza kwamba unaweza kuweka permissions mbali mbali kwa watu wengine wanaotembelea au unaweza kutumia programu maalumu kulock hilo folder lako au unaweza kuhide .
 
Mzee Shy nitumie email yako kwenye my email ambayo nadhani nimetoa kwenye thread nyingine then nitakutumia hako kafile,ila kama bado unatumia Antivirus kuna baadhi ya anti virus huwa zinadelete hili file kwani limekaa kirusirusi(haha) so inabidi uende uifanyie configuration hiyo antiv yako ili iitrust.Then baada ya kuinstall nenda kabadilishe registry (Hakikisha ni 1 sio 0) ili isiwe na uwezo wa kuaccess network kwani kuna wajinga wataitumia kuaccess PC yako,si unajua hakuna cha Bure muzee,lazima ulipe hata kama ni indirect. Alunta Kontinua....
 
Back
Top Bottom