Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 211
Unaonaje unaposhuka hapo chini gorofani ukakuta HDD iliyobadilishwa katika computer yako juu iko mikononi mwa machinga anaiuza kwa bei chee , tena ina lebo yako kabisa MALKIA X DEAD , taarifa zinasema hiyo HDD Ilikufa au kupata madhara fulani ndio maana imebadilishwa .
Au wakati mwingine unapoenda mahakamani kujitetea na mtu mwingine usiyemjua anakuja na nyaraka ambazo zimetokana na HDD ya computer yako iliyobadilishwa kitambo si unaweza kupata kichaa ? ulifikiri ile imeshakufa , haipotena kumbe ulikosea .
Sasa hivi kila mtu anajitahidi kuficha au kuweka data zake katika sehemu salama , wengine wako busy kutafuta data hizi waweze kuzitumia katika mambo yao , mfano ni huo nilioutoa hapo juu .
Mwaka jana katika ofisi Fulani binafsi tulikuwa na kazi Fulani ya kuuza computer mpya na hizo za zamani zilipelekwa katika achieve ya hiyo office husika ni mbali kidogo na hapo sehemu yenyewe ni dereva wa kawaida tu ndio alikuwa akipeleka kwa usimamizi wa Administration .
Kwa kuwa mimi ndio nilikuwa mtu wa IT pale sikupenda hizi zile computer ziondoke na HDD zake kwa sababu ndio zenye data muhimu hata kama zikiwa formatted kuna tekinologia za kuweza kurudisha zile data na nilishuhudia wakati Fulani komputa moja ikiwa katika office binafsi ya mmoja wa wafanyakazi wale .
Nilichokuwa nafanya mimi ni kuondoa HDD zile na kuacha wapeleke computer peke yake huko zilipopelekwa sikuwa na uhakika nako sana kutokana na sababu hiyo , vile vile ni kufuatilia ile PRIVACY POLICY iliyokuwa ndani ya kampuni husika ile inayohusu data na taarifa zingine za kampuni .
Mwishowe nilikuja kugundua yule kinganganizi aliyekuwa anataka sana zile computer alikuwa na offisi yake amefungua alichokuwa anataka ni kutumia zile data kazi zile computer katika kuleta ushindani na kampuni yake aliyomlea .
Kule kwake zile computer zinaweza kuibiwa zikaingia mikononi mwa watu wengine katika uchunguzi zikaonekana zimetokea kwangu zikaenda kwa huyu kinganganizi ikawa balaa , je nani yuko tayari kuhatarisha DATA za watu ?
Hata hivyo kazi ilimalizika na data ziliendelea kuwa mikononi mwa kampuni husika , huo ni mfano mchache nilioutoa hapo juu .
Kwa sasa mjini dare s salaam kumetokea vijana wengi wanaouza vifaa vya computer haswa RAM , HDD ,CPU na hata computer zenyewe ukiacha laptops ambazo zimezoeleka lakini zaidi nitaongelea HDD ambako Data za watu hukaa mule na chochote kinaweza kutokea .
Siku moja niliwahi kujaribu tu kwenda sehemu moja kariakoo katika mizunguko yangu nilikutana na vijana Fulani hizo HDD wamezipanga katika meza zinauzwa kuanzia alfu 10 , 20 na 30 kutokana na ukubwa wake hizo sio bei ghali sana , siku hiyo ilinibidi ninunue bwana ili nikaone kunani .
Niliponunua kwenda nazo kuziangalia nikashanga zimetoka sehemu nyeti ya serikali na zina nyaraka binafsi na zingine muhimu za wizara husika , inawezekana hizi hdd ziliandikiwa zimekufa kwahiyo mtu akabadili tu na zile zingine akaenda kuuza
Au inawezekana walienda kutupa katika dustbin wale wazoa taka wakachukuwa wakazifuta na kupeleka sokoni kariakoo , hawa vijana hawajui ni vitu gani hivi hawajui umuhimu wake ndio maana wanauza kwa bei ile na kuzipanga hazarani vile .
Kama unavyoona hapo juu , data za wizara baadhi nimeshazipata mimi , mfano kama kungekuwa na vitabu mule au ripoti muhimu mimi ningeweza kuchukuwa na kuzitumia jinsi ninavyojua au kutaka mimi ikawa balaa kwa wengine .
..
Imefikia wakati sasa wizara na sehemu zingine za serikali kuhakikisha wana PRIVACY POLICY inayohusu DATA na vifaa vingine vya mawasiliano na ziwe wazi sio kwa watu wachache tu , sasa hivi kila mtu yuko busy anataka data kwa ajili ya kufanyia kazi zake .
Wanahabari wanataka DATA kwa ajili ya kuandika magazeti na mambo yao mengine , na mambo kama hayo , watu wasidharau data kiasi hichi wanaziacha wazi mpaka mtu anaenda kununua data ya dhamani kubwa kwa alfu 20 tu .
..
Najua kuna baadhi wa watu nimeona zaidi serikalini ambao wanapenda kufanya kazi na watu mmoja mmoja freelancer katika shuguli zao za kiufundi zinazohusu ICT , unapofanya hivi ujue ni makosa kisheria kwanza huyu mtu mmoja huna guarantee naye wakati wowote anaweza kukimbia au kufanya chochote kile na ni yeye peke yake tu .
Ilitakiwa kutangazwa tender na kampuni mbali mbali zinaomba tender hiyo inayoshinda ndio inafanya shuguli hiyo , katika kampuni kila kitu kinachofanywa kinakuwa na ripoti yake au taarifa yake na utahakikishwa usalama wa data zako na vitu vyako vingine .
Pia katika kampuni hizi wameajiriwa watu wanaojua fani hizi wako katika fani hiyo kwa muda kwahiyo wanajua vingi na wanaweza kusaidia katika mengi , kumbuka wanafanya kazi kama timu mmoja kumbuka KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA .
.
Ushauri kwa techs ambao hufanya shuguli hizi wahakikishe wanaandikishiana mikataba au mkataba na wizara au shirika husika kuhusu kazi na malengo ya wao kuwa katika sehemu husika kumbuka unafanya kazi na data za watu chochote kikitokea ni wewe utayashikwa na kujibu hizo shutuma .
Mfano mimi nilivyoenda kariakoo kununua hiyo HDD ningeamua kutumia zile data kwa mambo yangu halafu baadaye ije kuwa balaa , maana yake atafuatiliwa mtu wa kwanza kabisa aliyetoa hicho kifaa mpaka kupatikana kwa watu wasiohusika .
Bahati mbaya sana kampuni nyingi hapa jijini haswa hizi zenye shuguli za kiufundi hazina pia PRIVACY POLICY kwa ajili yake yenyewe na wafanyakazi wake , wafanyakazi wanaajiriwa bila mikataba , hawajui majukumu yake pale haswa utunzaji wa data na vitu vingine vya wateja ndio maana tunazikuta mitaani .
Kama inawezekana sasa vyombo vya usalama vianze kuwa macho kuanza kufuatilia nyufa hizi za data kabla ya kutokea balaa kubwa zaidi linalohusu data na vitu vingine vinavyohusiana na DATA ,lazima ifike sehemu sasa hivi vyombo vishirikiane na hizi workshop au wamiliki wa kazi hizi kuweza kutambua changamoto wanazopanda nazo na jinsi wanavyoweza kushirikiana katika kupunguza matatizo haya .