Unaitumiaje Diary yako,je diary inahitaji privancy?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,246
Ni lini mara ya mwisho kuitumia diary yako,je huwa unaandika matukio kwa mda mwafaka au leo unanunua diary halafu unakuja kuandika matukio ya miaka iliyopita.
au hamna umuhimu na je inahitaji privancy kama vile barua pepe au simu!
Mda mwingine nasahau diary yangu ila siku nikikuta kwenye kabati nikaanza kusoma niliyoyaandika naona kama mengine ni mpya na ninaanza kuona umuhimu wake.


Kama wewe ni mtumiaji wa diary je ni nini hasa au matukio gani yanapaswa kuandikwa kwenye diary?
 
hmm... bado sijaona umuhimu wa diaries, diary inagombanisha watu, diary inaweza ikamfunga mtu.. kuna girl mmoja alikua na bf wake chuoni, the girl had 5 diaries na alianza kuandika mambo yake katika diaries tangia akiwa kidato cha 3. sasa huko chuo walikosana kidogo na bf wake, msichana akajiua, sasa tatizo ni kile alichokiandika kwenye diaries, katika diary yake ya mwisho aliandika kwamba bf wake ndiye sababu ya yeye kujiua wakati on the first place, jamaa hakuwa na makosa, jamaa alishindwa kujitetea kwa sababu hakuwa na shahidi na maelezo yake hayakua na nguvu.
katika diary ya zamani, yule msichana aliandika "amenilazimisha kutoa mimba, mimi sikutaka, nimelia sana leo." na watu wakajua ni yule jamaa, kumbe girl alimaanisha bf wake wa kwanza kabisa. Jamaa akafungwa kizembe tu
 
Back
Top Bottom