Unaitambua fangasi ya mdomo?,suluhisho liko hapa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
oral_c1_d01.png


ziko sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hii ya kutokea kwenye kinywa, lakini chanzo chake kikubwa ni maradhi yanayosababishwa na fangasi.

Maradhi ya fangasi ya kinywa huweza kuathiri koo pia. Vijidudu vinavyoathiri hujulikana kama oral candidiasis na wale wanaoshambulia koo huitwa oesophageal candidiasis.

Inapotokea uwiano huu wa kinga ya mwili na vimelea aina ya bacteria kushindwa kuzuia ongezeko la vimelea hivyo vya fangasi ndipo hali huwa mbaya na kusababisha utando mdomoni.

Maradhi haya ni kawaida kuonekana kwa watoto wachanga. Maradhi haya hutokea kutokana na hali ya kutokuwa na uwiano sahihi kati ya kinga ya mwili wa mtoto na vimelea aina ya bacteria.

Inapotokea yakatokea kwa mtu mzima, basi mara nyingi huwa kuna viashiria hatarishi kama vile upungufu wa kinga.

Mfano ni watu wenye maradhi ya muda mrefu kama saratani, kisukari na ukimwi au mwanamke wajawazito, hali hiyo hushusha kinga zao.
Tatizo hili huwapata pia watu wanaotumia dawa kwa muda mrefu hususani dawa za vijiuasumu (antibiotic) au za maradhi yanayotibiwa kwa muda mrefu kama vile saratani.
Kinachoweza kusababisha hali hiyo pia ni msongo wa mawazo wa muda mrefu.

Maradhi haya kwa kawaida siyo ya kuambukiza ingawa mtoto mchanga mwenye maradhi haya huweza kuyaambukiza matiti ya mama yake.

Dalili ni utando mweupe ambao huonekana kwenye kinywa eneo la ulimi na mashavuni kwa ndani. Kwenye koo huonekana kwenye kuta zake.
Mara nyingi eneo lenye rangi nyeupe huzungukwa na eneo lenye rangi nyekundu na lililovimba kidogo. Hii hutokana na mashambulizi ya fangasi.

Maeneo haya yaliyoshambuliwa huwa hayana maumivu makali lakini huweza kutoa damu kama yakiguswa au kusuguliwa.
 

Attachments

  • fangasi ya mdomoni.png
    fangasi ya mdomoni.png
    123.2 KB · Views: 980
  • fangasi ya mtoto.png
    fangasi ya mtoto.png
    80.2 KB · Views: 643
  • mtoto mdogo.jpeg
    mtoto mdogo.jpeg
    7.5 KB · Views: 615
Back
Top Bottom