Raha ya mtoto wa kike kutongozwa na fahari ya mwanaume kutongoza!

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,335
3,652
Habari za asubuhi wana MMU.

Nafikiri hili ni suala linalozua gumzo sana, hasa hivi karibuni kwenye hiki kizazi chetu cha dijitali ambapo wanawake pia hawapo nyuma kwa kutaka kufanya mambo yanayofanywa na wanaume pia.

Kwa hali hiyo basi siku hizi hata baadhi ya wadada hawaoni hatari kumtongoza mwanaume wanayeona anawasumbua akili yao, wengine wanamwambia moja kwa moja, wengine wanatumia mitego mbalimbali mpaka mwanaume anajikuta kaingia laini, wengine wanatumia marafiki wa karibu kufikisha ujumbe kwa mwanume husika yaani la msingi ujumbe umfikie mhusika.

Lakini jambo hili limekuwa na uvutano kwa pande zote mbili yaani me na ke,wapo wanaoona ni sawa tu kwa ke kumtongoza me na wapo wanaolipinga hilo kwa nguvu zao zote.

Kwa mtoto wa kike kumtongoza mwanaume kuna hasara kama tatu hivi ninazozijua mimi:

1.Wanaume wengi hulichukulia hili kama ishara ya kukosa aibu ya kike na hivyo kumchukulia mwanamke huyo kama kicheche.

2.Wanaume wengi wakiingia kwenye ndoa na wanawake waliowatongoza,mwanamke anakuwa hana sauti,wala hawezi hata kumtisha mwanaume kuwa anaondoka na kumwacha,majibu yao huwa hivi ``we nenda tu kwanza sikukupenda wewe ndio ulinilazimisha/ulinitongoza, kwa hiyo hata muda wa kukubembeleza anakuwa hana na hata akikubembeleza huwa ni kidogo sana na majibu ya kukatisha tamaa hufuata akiona umeshikilia msimamo wako.

3.Wanaume wengi huwa na huruma kuelekea wanawake na hivyo kujikuta wakiwakubalia ombi lao hata ikiwa kwa kweli hawajavutiwa nao au kuwapenda na yote hii hutokana na huruma ya kuwakatalia, na hilo hutokeza mume kuingia kwenye ndoa bila kuwa na lepe la upendo kwa mkewe? Unajua ndoa isiyo na lepe la upendo kwa upande mmoja ikoje? Simuliwa tu wala usiombe yakukute.

Kwa binafsi yangu nafikiri raha na haiba ya mtoto wa kike kutongozwa banah,mwanaume akuhangaikie,akubembeleze,akupigie misele mpaka akupate au mnasemaje wadada?

Na kwa wanaume mnasemaje?Mnaonaje mdada anapokusarandia ili uwe wake? Ungependa utongozwe au wewe ndo utongoze? Ni fahari kwako kutongozwa au kutongoza? Ukitongozwa na ke unajionaje/jihisije?

Wana MMU hayo ni maneno yangu tu na maoni yangu tu ambayo wala si sheria kwa hiyo karibuni wote tutoe maoni yetu kuhusu suala hili.

=========

1582779860616.png


Kutongoza ni kitendo cha mtu kumshawishi mwingine au kueleza hisia zake za kimapenzi kwa mtu anaempenda au kumuhitaji kimapenzi ili waweze kuanzisha mahusiano ya kimapenzi.

Kwa upande wa wanaume wao kutongoza ni jambo la kawaida kabisa na limekuwepo tangu enzi hivyo haitashangaza dunia kuona mwanaume anamtongoza mwanamke, ila ni jambo la fedheha pale mwanaume anaposhindwa au kukosa ujasiri wa kumtongoza mwanamke anaemtaka au kumpenda.

Zifuatazo ni njia zinazoweza kuwasaidia wale wasioweza kutongoza

1. Kuwa na sababa za uhakika
Kabla ya kuanza chochote, inafaa kujiuliza kwa nini unataka kumtongoza huyo mwanamke /mwanaume. Najua hautaki kumtongoza kwa sababu ya muonekano wake ama kwa sababu unataka kujionyesha kuwa wewe ni bingwa wa kutongoza zaidi, maana yake ukifanya hivyo utakuwa umejidhalilisha mwenyewe. Pia usijaribu kutongoza ili kumuonyesha mpenzi wako wa zamani kuwa hatoshi mboga.

Pili unafaa kufahamu japo kidogo tabia ya mtu unaye mtongoza, yaani kuyajua maisha yake, vitu anavyovipenda, na pia je mkiwa pamoja mnaweza kuunganika. Ukihakikisha kuwa sababu zote unazo za kumtongoza mwanamke huyu, basi sasa unafaa kuruka kwa step ya pili.

2. Kuwa mtu unaejiheshimu mbele za watu
Ni lazima utumie ujanja wa kuwa mnyenyekevu kwa kila mmoja. Usiwe mtu ambaye unaropoka na kutusiana na watu ovyo ovyo. Inafaa ujaribu kadri uwezavyo kuheshimu kila mtu. Hii itamfanya mtu unaemtaka kuona kuwa wewe unadalili za kuwa mpenzi au mchumba bora zaidi kwake.

3. Kuwa mcheshi
Wanawake na wanaume hupenda watu wacheshi, yaani mtu ambaye anaweza kumfurahisha na kujisikia ana furaha wakati wote.

Najua kwa upande wa wanaume wapo ambao ni vigumu wao kumchekesha mtu lakini hiyo si sababu ya kuwa hautakuwa na nafasi ya kumpata mwanamke wa ndoto zako.

Hakikisha hata kama ni mara moja unahifadhi baadhi ya vitu ambavyo kwa hakika vitachekesha. Na amini usiamini, wakati ambapo utakuwa ukimfurahisha, itakuwa rahisi kwako kuwa na nafasi rahisi ya kuuteka moyo wake.

4. Kuwa karibu naye
Hapa simaanishi kuwa kila mahali atakapokuwa unamfuata nyuma nyuma, la. Kile ambacho namaanisha hapa ni kuwa uhakikishe kuwa atleast una company na yeye. Hii inaweza kufanikishwa kiurahisi kama wewe ni rafiki wa rafiki yake.

Unaweza kuitisha kikao na rafiki yako halafu umwambie amkaribishe rafiki yake (huyo mnayemzimia). Hapo itakuwa rahisi kwako kueneza mbinu ya 3 hapo juu kwa urahisi.
Onyo: Usianze kumtongoza papo kwa papo...anza na kumfanya akuzoee halafu mengine yatakuja baadae.

5. Kujiamini
Kujiamini ni lazima bila kujiamini huwezi kufanikiwa... Wewe unatakiwa kumchukulia kama binadamu wa kawaida japo unampenda ili uwe na ujasiri mbele yake inabidi umuone wa kawaida sawa na watu wengine. Ukishafanya hivyo, itakuwa rahisi kwako kwani utakuwa umejitenga na wale wengine wanaompenda ila ni waoga hivyo kujipunguzia mashindano.

6. Muonyeshe uzuri wako
Hapa lazima umuonyeshe talanta yako yeyote ambayo unayo. Aidha unaweza kuwa unakipawa cha kuimba, kuchora, kudensi, kubenjua maungo nk. Ooo utajiuliza kwa nini unafaa umuonyeshe talanta yako.

Jibu ni rahisi wewe hautakuwa peke yako kumtamani ama kumtongoza, so lazima uje na kitu ambacho kitakutofautisha na wengine ili asikusahau. Ukimwonyesha kipawa chako labda anaweza kukukubali na akapenda mambo yako na kumfanya kutamani kuwa na wewe mara kwa mara.

7. Tafuta udhaifu wake
Kila mtu anaudhaifu wake katika vitu na mambo tofauti tofauti. Hakikisha umejua udhaifu wake vizuri. Kama anampenda mwanamziki flani, sehemu fulani ama chochote kile, hakikisha umejipatia nafasi ya utafiti ili wakati mwingine utakapokutana na yeye unazua stori kuhusu jambo analolipenda.

Atachangia na wewe ujazie. Hii itakufanya wewe kuweza kukupenda kwani ataona kuwa kuna mfanano kati yenu kwa vitu mnavyopenda.

8. Makinika na akili yake na wala si muonekano wake
Kile ambacho unachohitaji kushungulikia zaidi ni kumsifu kwa mambo ambayo anayoyafanya na kupitia akilini mwake. Baada ya kuongea na yeye katika maongezi tofauti tofauti, atakufungulia moyo wake kwa urahisi ambapo hapo utatumia nafasi kumjua kiundani kumhusu. Akitaja kitu ambacho kimekupendeza unaweza kutumia nafasi hio ya kumsifu na kumwambia kuwa umependezwa sana kwa kutaja au kugusia swala fulani.

9. Jaribu kuja na kitu tofauti
Kama imetimia ule muda wako ambao unaona kuwa umefikia level ya kumfungilia moyo wako na kumwambia kuwa unampenda, jaribu kufanya kitu tofauti ambacho hajawahi kufanyiwa na yeyote.

Usijaribu kumpelekea maua kwani hio inaweza kuwa si mara yake ya kwanza kupokea maua so kama ni wewe ungefanya uchunguzi na kitu ambacho bado unaona hajawahi kuletewa so ukifanikiwa kumsaprize vizuri, una nafasi kuu ya wewe kufanikiwa kumpata yule aliye ndotoni.

Ukitumia ujanja ambao ni tofauti na watu wengine una nafasi kubwa ya kufaulu. Kutumia ujanja wako vizuri na kujiamini ni kama mkuki kwa unaemtaka, ukiurusha haukosi kutoboa.

Michango ya wadau:

Kwa muono Wangu Mimi mwehu ndama Mdau mwenzenu nasema Kuzaliwa mwanaume ni bahati kwake mwanaume lakini pia kuzaliwa mwanamke ni fahari Sana Kwa jamii.

Naam kuwa mwanaume kunatupa fursa adhimu yenye kuvutia Inayojenga dhana nzima ya utu wetu uliopewa utukufu mwingi na muumba wetu aliyetukuka.

Fursa hii si nyingine Bali ni Ile ya Sisi kujipima makali yetu na kujifua Kimbinu mbele ya wanawake naam mbele ya mapambo yetu haya tuliyoumbiwa na mnyezi Mungu ili kuweza kuyamiliki kifikra na hata kuyatafuna kimwili pale inapobidi

Hakika kumtongoza mwanamke ndio starehe kubwa yenye msisimko mwingi na hakishi tele kuwah kutukia katika maisha yetu wanaume.

Kutongoza kuna Raha kubwa isiyokifani kunatujengea watongozaji Hali ya kujiamini mara baada ya ombi lako kukubaliwa na kutupa nguvu yakuendelea kutongoza kila mara lakini pia harakati hizi za kutongoza zinajenga msisimko mkubwa Sana wa kupenda maisha sababu walau kunakupa sababu ya kupenda kuiona kesho ili kupata jibu, unaweza ukatumia utongizaji kama Tiba ya msongo wa mawazo sababu kutongoza kutakupa changamoto mpyaa.

Mwanaume kukaa bila kutongoza ni dhambi kubwa Sana na kunazeesha haraka sana, hivyo tujenge mazoea yakutongoza mara Kwa mara ili Ku update mbinu zetu, tena kuoa au kuwa kwenye mahusiano kusitukatishe tamaa." ni lazima tutongoze Sana tena hovyo hovyo Kwa ajili ya akiba ya baadae Naam lazima tujifunze kuweka viporo vya wanawake Kwa ajiri ya dharura za usaliti na hii itasaidia hata kupunguza Mori zetu na hasira Kali mara tunaposalitwa.

Basi Kwa hayo machache niwatakie utongozaji wenye umakini na ustadi mkubwa

NB:
usiangalie mazingira ,tongoza popote pale na mda wowote mwanamke hapewi nafasi ya kufikiria nikurusha makombora Tu, mpaka jibu liwe positive nibora umtongoze milele kuliko kukubali jibu la hapana.

Sent using Jamii Forums mobile app
----
Hii mada imenigusa sana, maana nilikuwa domo zege na vibuti nilikuwa nachezea vibaya mno.

Kuna mtu mmoja alifundisha vizuri sana, namna nzuri ya kuongea na wanawake, jaribu kutengeneza dialogue make her comfortable around you. First impressions matter, usilete topic/maswali yenye "Yes/No". Sio unafika tu, "Dada nimekupenda, naomba namba yako ya simu", akisema hana simu gearbox inakuwa imeingia kokoto.

Kuna manzi nilikuwa nasoma naye chuo, wakishua, halafu ana akili kinoma. Ana jamaa yake ana mpunga kweli kweli. Siku moja nikakutana nae mtaanai, nikamsalim then nikamwabia something simple, "Unajua kila nikikuona huwa najiuliza maswali mengi sana", alipotaka kujua ni maswali gani, nikamwambia "never mind".

Tukabadilishana namba, usiku alikuwa wa kwanza kunipigia (nilitengeneza the need to know, na binadamu hapendi kutojua), anataka ajue ni maswali gani hayo? bahati nzuri sana nilikuwa na safari, tukaongea/chat sana. Actually I was surprised, hakuwa na nyodo kama tulivyokuwa tunadhani; nilivyorudi nikwambia nimekuletea zawadi(uongo mtupu).Zawadi gani, nikamwabia siri yangu, njoo home uchukue, alivyokubali tu, mimi huyo Mwenge vinyago kuchukua zawadi kutoka "Arusha"
The rest is history....

Talk to her about anything without direct requests, mpaka atakapojisikia huru na wewe; Angalia mazingira, unawezaje kumfanya awe comfortable na wewe hapo mlipo?. Kuna demu mmoja nilimpataga kiulaini Mlimani City. Nimekutana nae Mr Price, nikamsalimia, nikajitambulisha [Respectfully]. Then nikamwomba msaada (Point to note: surprisingly wanawake wanapenda sana kutoa msaada), anisaidie kutafuta zawadi nzuri ya birthday ya dada yangu wakati sina dada wala birthday.
Nikawa nimeua ndege watatu kwa jiwe moja

1. Nimetengeneza dialogue without looking like an jerk.
2. Kwa kumuamini na kumpa kazi ya kutafuta zawadi, nimetengeneza trust between us; inaondoa natural defenses za mwanamke
3. Nimeonyesha kwamba I do care (kumtafutia zawadi sister yangu)
The rest is history....

Kuna actions wanawake wanazipenda naturally mfano taking care of children. Siku moja moja toka na vitoto vyako or vya any close relative, approach any lady, lazima moyo wake u-melt; anaanza kumuona baba wa watoto wake wakati wewe ni fisi tu. (Msije anza kuzungusha juani watoto wa ndugu zenu)

Kutongoza ni science. Wanaume tujue wanawake wanatongoza kila siku na kila mtu; how do you stand out? Nini kitamfanya asikusahau wewe? Jifunze, practise, utafanikiwa.
----
Habari wana jamii.
Kuna hii tabia ya vijana wa kiume kuogopa kutongoza hasa kwa kuhofia kua watakataliwa. Kwanza ni kosa kuhofu au kua na mawazo ya kukataliwa au kushindwa katika maisha.

Jambo la pili na kubwa zaidi ni kwamba kutongoza ni sehemu ya kutimiza majukumu yako kama mwanaume. Huna haja ya kuhofu kutimiza majukumu yako hata kama utakosea.

Ukizaliwa tu mwanaume, kutongoza ni sehemu ya majukumu yako makuu kwenye Job Discription(JD) yako.

Tongoza kila mwanamke unaedhani au kuona unaweza kutongoza, tongoza kadri uwezavyo au upendavyo, usihofu kukataliwa, hofu kutokutongoza ila sio kukataliwa. Jisikie mwenye hatia kutokutimiza wajibu wako kuliko kujisikia hofu ya kukataliwa katika kutimiza wajibu wako.

Jifunze hata kwa ndege na wanyama, jogoo hutongoza kila tetea anaemuona bila kujali atafanikiwa au la, akifanikiwa hewala, akikosa alikua anafanya mazoezi ya kukimbia na kuweka mwili sawa.

Lakini pia usiogope kutongoza mwanamke mzuri kwa kuhofu kua lazima atakua na mume/mpenzi, wewe tongoza, sio kila mwanamke mzuri basi ana mume, wengi hua ni vacancy, ukijaribu unaweza kufill hiyo nafasi. Tongoza mahala popote u apojisikia au kuona kuna mtu unaweza kumtongoza na muda wowote.

Ni ushauri tu na kukumbushana majukumu.
----
Blue G,
Kumkatalia....!!!I dont think ni neno sahihi labda uulize nitamchukuliaje?Imeshanitokea mara 3, mara ya kwanza High School, Ya pili Chuo na kazini! High school alikuwa ni best yangu sana, alikuwa anapenda kuja uwanjani kuniangalia ninavyocheza na mda mwingine kutaka nimfundishe (volleyball), but walikuwa wengi wanataka niwafundishe hivyo sikuwahi kudhani ananifeel, until siku moja mbele ya rafiki zake akanichana tena nikiwa naongea na lady captain wa volleball akaja na kuanza kama anamsimulia mwenzake "...basi huyu kaka nampenda, napenda anavyocheza volleball, kila siku naenda uwanjani kumuangalia, na marafiki zangu wote nimewaaambia nataka awe bf wangu lakini yeye hata sijui kama ananifikiria...."!

Big suprize I didnt know what to do, beautiful girl of course alikuwa na viskendo uchwara pale school!Unataka kujua nili react vipi! Nilimwambia nampenda pia lady captain akaanza kunitania nikakosa pozi, nikayeyusha na kuondoka!Mpaka namaliza shule sikumjibu zaidi ya kusmile nikimuona!

"Do you think I did hurt her?!! wow sorry!!!Huyu wa chuo alikuwa tofauti kidogo yeye hakumwaga mchele hadharani, alitafuta namba yangu ya simu akaniita chumbani kwake na kunieleza ukweli wake!I respected her feelings, but nilikuwa na GF tayari!Akaniambia anafahamu na hajali! To be honest with you hapa nilipata mteremko, I ended up cheating with her!It was always cool!

Mpaka leo tunaheshimiana sana!Wa kazini was a crush.. she wasnt from Tanzania, na mie sikuwa bongo!Hii nilianza kuisimulia humu JF kama true stori watu hawakugonga like wakaleta majungu nikawapotezea!But we ended up on bed honestly!
 
Imekua bahati mbaya sana,mwanake sikuhizi hutongoza mwanaume kwa kangalia wallet yake na c uanaume wake.
 
Siku hizi hawa wa kutongaza na kukupigia misele watatoka wapi???

kidigital zaidi sku hizi

mapenzi yenyewe watu wanalia ni short time wewe utongoze miezi.........
 
Weka hilo pembeni mkuu bilachenga tujadili tu hili kwa upande wako liko vipi?una maoni gani kuhusu hili?raha yako wewe ni ungependa iweje kwako utongozwe na ke au we ndo umtongoze?na ukitongozwa na ke unahisije?unamwonaje ke anyetongoza?
imekua bahati mbaya sana,mwanake sikuhizi hutongoza mwanaume kwa kangalia wallet yake na c uanaume wake.
 
Last edited by a moderator:
Dada ICHANA tuseme hayo ya kizazi hiki tuyaweke pembeni na tongelee jinsi mambo yanavyotakiwa kuwa,wewe una maoni gani kuhus hilo,unafikiri haiba ya mtoto wa kike inamruhusu kumtongoza me?unafikir ni kitu kizuri tu?kama sio nini madhara yake?
siku hizi hawa wa kutongaza na kukupigia misele watatoka wapi???

kidigital zaidi sku hizi

mapenzi yenyewe watu wanalia ni short time wewe utongoze miezi.........
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo wapo mkuu hata kama ni wachache lakini la msingi ni kuwa wapo,kwani we hujawahi kutongoza au mwenzetu ushaoa zama zile?
Kumbe siku hizi kuna watu bado wanatongozana?
 
Mbona poa tu au,,,, kama amekukubali we. me mwenzangu hujui ,, si anakupa real.,. napenda initokee demu anisomeshe
 
dada ICHANA tuseme hayo ya kizazi hiki tuyaweke pembeni na tongelee jinsi mambo yanavyotakiwa kuwa,wewe una maoni gani kuhus hilo,unafikiri haiba ya mtoto wa kike inamruhusu kumtongoza me?unafikir ni kitu kizuri tu?kama sio nini madhara yake?

MWANAMKE HAIBA na USO WA SONI

ina madhara makubwa sana kwa mwanamke kumtongoza mwanaume...na hayo mahusiAno hayatadumu na wala hayatakuwa na amani
 
Penye red hapo dada ICHANA nimeipenda sana hiyo na ndivyo inavyotakiwa asiee japo wengi siku hizi wameendekeza udijitali na ukisasa,na kwa kweli mahusiano ya namna hiyo ni ngumu sana kudumu na hata ikitokea yakadumu mwanamke sikuzote atapata taabu mno ten sikuzote za uhusiano wao,asante sana kwa mchango wako.
MWANAMKE HAIBA na USO WA SONI

ina madhara makubwa sana kwa mwanamke kumtongoza mwanaume...na hayo mahusiAno hayatadumu na wala hayatakuwa na amani
 
Last edited by a moderator:
Na kwa wanaume mnasemaje?mnaonaje mdada anpokusarandia ili uwe wake?ungependa utongozwe au wewe ndo utongoze?ni fahari kwako kutongozwa au kutongoza?ukitongozwa na ke unajionaje/jihisije?

Mimi ilishanitokea kwanza niliona aibu na huruma mtu kufikia hatua ya kukutamkia japo sikula matunda,
Ningependa nimuanze mwanamke siyo yeye.
kwa kweli akikuanza unaanza kuhisi kama ni malaya maana katika mazingira ya kawaida haiwezekani mwanamke ambaye siyo mzoefu kwenye mambo haya kukuanza.
 
Asante kwa jibu lako mkuu,hata mimi nahisi hivyo aisee,nafikiir inapendeza sana na inaongeza mvuto wa kimapenzi endapo mtoto wa kike atakuwa na aibu kiasi hawezi thubutu kufungua kinywa chake kukueleza kuwa anakupenda,kinyume na hapo hata mvuto unapotea kuona mtoto wa kike kapata ujasiri wa kumwimbisha mwanaume,kwa kweli kwa hapo unaona kabisa mtoto huyo wa kike hana mvuto na haiba ya kike kwa kweli.@ng`wana ong`wa kulwa,
 
Blue G kwa kweli inapendeza nikimuanza mimi hata kama yeye alishaonyesha hizo dalili za kunipenda ila lile tamko nilitoe mimi na sio yeye aanze maana naona kama amejirahisi sana kunitamkia ananipenda

Na itakapotokea tatizo lolote kama ulivyosema nitaishia tuu kumwambia au kuumumiza kuwa ulinitaka wewe na hukuwa chaguo langu nasikukupenda ila ulijileta

Japo wapo wanaoonyesha ishara za wazi kuwa wanakupenda ila hata kama zipo hizo ishara iishie mwanaume aje aweke hisia zake mwenyewe na sio mwanamke aanze kuweka hisia zake
 
Last edited by a moderator:
Mimi nionavyo mwanamke kukutamkia nakupenda asilimia kubwa huwa ni kicheche kwa ambae sio mzoefu hawezi kukutamkia live bila chenga ni sawasawa unamtongoza mtoto wa kike mara moja anakubari na ukimuomba mfanye mapenzi anakubari mara nyingi huwa kunatatizo kama ulikua unampango wa kumuoa inabidi ukae chini ufikirie
 
MWANAMKE HAIBA na USO WA SONI

ina madhara makubwa sana kwa mwanamke kumtongoza mwanaume...na hayo mahusiAno hayatadumu na wala hayatakuwa na amani

Mimi naona raha sana pale napoanza kukutongoza halafu ukazingua kidogo mpaka siku tukienda gest unakuwa na ile staki nataka. Hapo inakuwa mzuka kishenz. Lakin sio wale unamwomba namba ya sim tayar katoa bila hata kipingamiz unampiga saund hata hakatai hata kidogo mnaenda gest yeye ndio wa kwanza kuvua anashinda na kyupi tu. Aaghrrr hata mzuka hakuna hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom