Unaikumbuka habari ya Mke wa LUTU kugeuka nyuma na kujikuta amekuwa NGUZO YA CHUMVI?

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Kuna mipango ya watu wengi kila siku inageuka nguzo za chumvi, kuna malengo mengi yameshindwa kutimia na kugeuka kuwa nguzo za chumvi kwenye maisha ya watu.

“DISTRACTIONS”- Mambo yanayokutoa kwenye mstari) ni moja ya vitu vinavyoweza kukuchelewesha sana kufika unakokwenda.Ukishindwa kukabiliana na “DISTRACTIONS” zinazokuja kila siku kwenye maisha yako na kuingilia ratiba yako ya kila siku itakuchukua muda mrefu kutimiza malengo yako.Mara nyingi “distraction” huja pale unapokuwa na MALENGO MAKUBWA au unapokaribia KUVUKA KIWANGO FULANI.

Ziko za AINA MBILI:

1)Huja kama WATU: Hawa watakuja aidha kukuanzishia ugomvi na malumbano yasiyo na kichwa wala miguu na usipokuwa mwangalifu utaanza kutumia rasilimali zako (Muda,Nguvu,Fedha)kupambana nao badala ya kusonga mbele.Wengine watakuja kukuonyesha namna unachotaka kufanya ambavyo hakitafanikiwa na wataanza kukupa mawazo mbadala ya kukutoa kwenye wazo kuu,uwe makini nao.Jifunze KUPUUZA (IGNORE) baadhi ya watu na wengine KUWAKWEPA.

2)Huja kama MATUKIO(Events): Hapa huwa ni yale MAMBO yanayotokea kwenye maisha yako ambayo ghafla unajikuta UMEKUWA BIZE nayo na yanakuchosha, unatumia rasilimali nyingi na unajikuta HAUNA MUDA wa kufanya mambo MAKUBWA uliyokusudia. Ukiyashtukia haya jitahidi kugawa MAJUKUMU (Delegate) ili uelekeze nguvu zako kwenye mambo MAKUBWA na MUHIMU.

Leo unapoanza siku utakuwa na “Distractions” za aina hizi mbili.Uwe makini zisije zikageuza MIPANGO na MALENGO yako yote kuwa NGUZO ya CHUMVI.

#Nanauka
 
Back
Top Bottom