Unaijua ngoma ya mtingo? Je, unajua kwanini ngoma hii huchezwa kwa kushikana mikono?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Mtingo ni ngoma maarufu ya kiasili inayochezwa katika kabila la wachaga. Ni ngoma inayochezwa haswa wakati wa matukio mazito ya kijamii kama sikukuu mbalimbali na ugeni mzito.

Ngoma ya mtingo hujumuisha zana za Pembe kubwa (ambayo hutoa mlio kama mbiu), Njuga (ankle bells) na mtingo wenyewe (drums). Hizi huchongwa kama mti mrefu wenye shimo katikati na upande mmoja wa shimo hufungwa ngozi ambayo ndio hupigwa ili kupata sauti.

Ngoma hii huchezwa kama mduara fulani huku wachezaji wakiwa wameshikana mikono.

Wachunguzi wa mambo wamegawanyika juu ya sababu za kushikana mikono huko:

1. Kundi moja linadai kuwa kushikana mikono ilitokana na wachaga kutoaminiana. Kwamba kama usipomshika mwenzio mkono anaweza kukuchomolea pesa mfukoni bila kujijua.

2. Kundi lingine linadai sababu kubwa ni kuonyesha mshikamano na umoja miongoni wa wanajamii ya wachaga.
 
Bila kapicha mkuu??
Japo mimi siyo mchaga, point namba 2 inaweza kuwa na mashiko hasa ukizingatia historia ya jamii za wachaga,ambao ni muunganiko wa makabila tofauti tofauti kutoka kaskazini.wote wanatumia ngoma hiyo hiyo, hivyo kucheza kwa kushikana mikono kunaonesha umoja wao
 
Mtingo ni ngoma maarufu ya kiasili inayochezwa katika kabila la wachaga. Ni ngoma inayochezwa haswa wakati wa matukio mazito ya kijamii kama sikukuu mbalimbali na ugeni mzito.

Ngoma ya mtingo hujumuisha zana za Pembe kubwa (ambayo hutoa mlio kama mbiu), Njuga (ankle bells) na mtingo wenyewe (drums). Hizi huchongwa kama mti mrefu wenye shimo katikati na upande mmoja wa shimo hufungwa ngozi ambayo ndio hupigwa ili kupata sauti.

Ngoma hii huchezwa kama mduara fulani huku wachezaji wakiwa wameshikana mikono.

Wachunguzi wa mambo wamegawanyika juu ya sababu za kushikana mikono huko:

1. Kundi moja linadai kuwa kushikana mikono ilitokana na wachaga kutoaminiana. Kwamba kama usipomshika mwenzio mkono anaweza kukuchomolea pesa mfukoni bila kujijua.

2. Kundi lingine linadai sababu kubwa ni kuonyesha mshikamano na umoja miongoni wa wanajamii ya wachaga.
Hiyo sababu namba 1 haina logic? Hivi ukialikwa kwenye sherehe unabeba fedha? Na ni kiasi gani hata zitamanishe wizi?
Ingekuwa wanafanya hivyo wakiwa sehemu zinazohusiana na ubebaji wa hela nyingi kama benki nk ingekuwa logical.
 
Back
Top Bottom