Unaijua Google Translate?

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Moja ya tekinologia nzuri na ya kipekee katika tovuti ya google ni hii inayoitwa google translate , unaweza kutumia google translate katika kutafsiri maneno toka lugha moja kwenda nyingine bila matatizo yoyote ingawa sio lugha zote unaweza kutafsiri .

Siku hizi sio ajabu kumkuta mchina anashiriki forum ya wakenya au ya watanzania bila shida yoyote , utajiuliza tu huyu mchina anajuaje lugha yetu na mambo yetu ? ni rahisi yeye pembeni anatumia programu maalumu ya kutafsiri maneno kwenda katika lugha yake kisha anarudisha kwa lugha yako anakupa majibu .

Kwa ufupi google translate ni huduma inayotolewa na google kutafsiri neno , sentensi au kurasa kwa lugha nyingine kwa kufuatia idadi ya paragraph , na baadhi ya maneno ya kitekinologia , kwa lugha nyingine mtaka huduma anaulizwa kutoa mawazo yake zaidi kwa maendeleo ya baadaye ya huduma hii .

Kama huduma zingine za kutafsiri Babel Fish, AOL, Yahoo na MSN, Huduma ya Google Translate kwa sasa inatumia SYSTRAN.
Version inayofuatia itatumia mfano unaoitwa statistical machine translation mfumo huu unatumiwa na mtaala wa nyaraka za umoja wa mataifa unaoitwa Corpus , Corpus ni mtaala uliokuwa na maneno zaidi ya bilion .
JE GOOGLE TRANSLATE INAFANYAJE KAZI
Fungua http://www.google.com/translate_t?hl=en kurasa yako itafunguka kuna vipande kama

1 ) TEXT and WEB hapo unaweza kuandika neno moja kutafsiri kwenda lugha nyingine kama kiarabu , kichina na kurudisha kwa lugha yako asili angalia idadi ya lugha zilizokuwemo . pia huduma hii inaweza kupatikana katika tovuti ya yale www.yale.edu/swahili kuna kamusi maalumu .

2) Translated search – hapo unaweza kutafuta kitu kilichofanyiwa tafsiri katika google hiyo hiyo au tovuti zingine ambazo zinatumia lugha husika na ambazo zina huduma ya lugha .

Inafanyaje kazi hii ?
A ) Tafuta mfano Dubai Tours kutoka kiingereza kwenda kiarabu
B ) ukurasa wako utatafsiriwa kwenda "جولات دبي" na utapata majibu yako kwa lugha ya kiarabu
C ) Na mwisho unaweza kufsiri kurasa hiyo ya kiarabu kwenda kiingereza

VITU VINGINE UNAVYOWEZA KUTAFUTA

St. Petersburg restaurants - (Санкт-Петербург рестораны) katika kurasa za kirusi
Beijing apartments - (北京公寓) Katika kurasa za kichina

Kwa msaada zaidi wa lugha na tafsiri unaweza kutembelea

http://www.google.com/language_tools

Au tovuti ya Kiswahili katika chuo kikuu cha yale

www.yale.edu/swahili

Pia kuna mradi wa Kiswahili Linux www.kilinux.org hapo unaweza kupata maneno mengi ya kisayansi na tekinologia
Kwa kumalizia kama wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili basi usikose kujiunga na baadhi ya group hizi katika yahoo ambazo zina wazungumzaji wengi wa kiswahili na walimu pia
www.groups.yahoo.com/kiswahili
www.groups.yahoo.com/swahili
 
Back
Top Bottom