Unaifahamu PowerShake? Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi..

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Uwepo wa simu janja umekuwa na changamoto kadhaa hasa kwenye suala la simu janja kutokaa na chaji kwa muda mrefu na kutokana na changamoto ndio wazo la kushare chaji kwa Wi-Fi lilipozaliwa..

Njia za kuchaji simu janja zimezidi kuongezeka kila leo kwani siku hizi tunaweza kuchaji simu janja kwa kutumia “Power bank“, kwa kutumia umeme wa Jua ambazo zinakuwezesha kuchaji simu ingawa utumiaji wa vitu hivyo vinaongeza uzito katika ubebaji na vinahitaji umakini ili kuvilinda kutoharibiwa kwa sababu ni rahisi kuharibika. Watafiti wa mambo ya kiteknolojia wamekuja na teknolojia inaitwa “PowerShake“.

PowerShake ni nini?!
PowerShake ni teknolojia inakuwezesha kushare chaji na mwenzako ili kuweza kuchaji simu ambayo imeishiwa na umeme. Ili kuweza kufanikisha ili simu zote mbili lazima ziwe simu janja, Wi-fi iwepo “On“.

wireless-charging.jpeg

Simu janja ikichajiwa kwa kutumia Wi-Fi



Watafiti wanasema kuwa changamoto wa teknolojia hii ni kwamba nguvu inayotoka kwenye simu janja ni mara mbili zaidi kuliko na chaji inayoingia kwenye simu janja inayochajiwa. Ukichaji simu kwa muda wa sekunde 12 kwa kutumia teknolojia ya PowerShake inaweza unaweza kuongea kwa dakika moja ya ziada. Na kama ukichaji kwa muda wa dakika 2, unaongea kwa njia ya video kwa muda wa dakika nne.

charge.jpg

Simu janja inayochajiwa Kwa kutumia Wi-fi ambayo ni shared

Majaribio ya awali yanaonyesha kuwa teknolojia hii itasaidia sana kwani itakuwezeha kushare chaji na mtu na kuchaji sehemu yoyote na wakati wowote.

Je, unadhani teknolojia hii itadumaza soko la chaji za simu janja?!

(Makala kwa hisani ya TeknoKona)
 
Itakua ngumu mpaka mfahaiane na kujaliana, mfano sio rahisi safarini ujinadi kuishiwa chaji na kuchajiwa kwa njia hiyo.
 
Watu wapo radhi kukusaidia vocha hata ya 5000 ila sio charge, fikiria mtu anaesafiri kitu cha kwanza anafikiria simu yake ijae charge halafu ndio ulete pua yako eti akupunguzie juice :D:D.
 
Back
Top Bottom