Unahitajika ukaguzi wa dharura bodi ya mikopo ya elimu ya juu

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
378
500
Waziri anayehusika atoe amri ya ukaguzi wa dharura na kutumia vyombo vya usalama na TAKUKURU kwa kuwa kuna viashiria vikubwa ya matumizi mabaya ya fedha na utoaji mikopo mwaka huu licha ya serikali kusema kuwa imetenga bajeti kubwa zaidi kuliko miaka mingine.

1. Idadi ya wanafunzi walioomba mikopo wakakosa ni wengi sana na hata waliopata wengi wao ni asilimia 40 kushuka chini.

2. Msimu huu ulishuhudia kuongezeka kwa idadi kubwa ya waombaji walioomba kukata rufaa ya kunyimwa mikopo kulinganisha na miaka mingine.

Swali la kujiuliza hii pesa iliyotengwa imelipwa kwa nani?isije yakaibuka yale mambo ya kulipa waombaji hewa" Kama serikali haikutoa fedha ya kutosha basi taarifa iwekwe wazi.

Ushauri wa mwisho ni bodi kuchapisha majina ya waombaji mkopo hasas wa mara ya kwanza waliopata na kiasi walichopata kupitia gazeti la serikali au vyombo vingine.

Kama ilivyotolewa na chuo cha udaktari Bugando. Vyuo pia vitoe taarifa ya idadi ya wanafunzi waliodahiliwa na wale walioshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mkopo.

Nawakilisha.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,640
2,000
Nilishasema serikali ifute loan board na irudishe wizarani utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanachuo waliodahiliwa kwenye vyuo vya umma pekee kama ilivyokuwa mwanzo.......kwa sababu kuna watu huko wana ubia kwenye vyuo binafsi ndo utaona hili linakuwa gumu kutekelezwa.

Serikali ikiendelea na huu utaratibu wa kuwanyima au kuwapa kiduchu wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya umma itapelekea kuviua na kuishia kuvinufaisha vyuo vya binafsi na kuwanyima fursa watoto wa wanyonge wenye uwezo mkubwa wa kiakili waliodahiliwa kwenye vyuo vya umma........serikali iendelee na wajibu wake wa kufadhili elimu kwenye taasisi zake, ni kipi kigumu kueleweka hapa?​
 
adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,540
2,000
Mwaka huu madudu ni mengi sana kuliko miaka yote nashangaa kwa nini serikali mpaka mda huu haijatoa tamko lolote sijui kitu gani wanasubiri.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,163
2,000
Waziri anayehusika atoe amri ya ukaguzi wa dharura na kutumia vyombo vya usalama na TAKUKURU kwa kuwa kuna viashiria vikubwa ya matumizi mabaya ya fedha na utoaji mikopo mwaka huu licha ya serikali kusema kuwa imetenga bajeti kubwa zaidi kuliko miaka mingine.

1. Idadi ya wanafunzi walioomba mikopo wakakosa ni wengi sana na hata waliopata wengi wao ni asilimia 40 kushuka chini.

2. Msimu huu ulishuhudia kuongezeka kwa idadi kubwa ya waombaji walioomba kukata rufaa ya kunyimwa mikopo kulinganisha na miaka mingine.

Swali la kujiuliza hii pesa iliyotengwa imelipwa kwa nani?isije yakaibuka yale mambo ya kulipa waombaji hewa" Kama serikali haikutoa fedha ya kutosha basi taarifa iwekwe wazi.

Ushauri wa mwisho ni bodi kuchapisha majina ya waombaji mkopo hasas wa mara ya kwanza waliopata na kiasi walichopata kupitia gazeti la serikali au vyombo vingine.

Kama ilivyotolewa na chuo cha udaktari Bugando. Vyuo pia vitoe taarifa ya idadi ya wanafunzi waliodahiliwa na wale walioshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mkopo.

Nawakilisha.
bodi ya mikopo inahitaji kushughulikiwa. halafu wanachelewesha sana malipo kwa wanafunzi, wanafunzi wanajiuza mno dodoma pale na hapa dsm, hawana kitu na hawana namna. mnataka hao watoto wafe kabla hata shule hawajamaliza? kama hela hamna si mmwambie Rais atangaze tu kwamba hela za mikopo hakuna?
 
Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
573
1,000
bodi ya mikopo inahitaji kushughulikiwa. halafu wanachelewesha sana malipo kwa wanafunzi, wanafunzi wanajiuza mno dodoma pale na hapa dsm, hawana kitu na hawana namna. mnataka hao watoto wafe kabla hata shule hawajamaliza? kama hela hamna si mmwambie Rais atangaze tu kwamba hela za mikopo hakuna?
Bodi ya kisanii tu hiyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom