Unahitaji utulivu wa akili na umakini katika kufikiri ili kumuelewa Magufuli kelele za Covid-19: Hoja Sita!

Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona

Vibaraka wa mabeberu km wale wa ufipa wamekosa hoja
 
😥
2397479_2396248_20200511_084948.jpg
 
Unahitaji utulivu wa akili na umakini katika kufikiri ili kumuelewa Magufuli kelele za Covid-19: Hoja Sita!

Denis Mpagaze
___________________________
Katika kipindi hiki cha corona na propaganda za magharibi, tusipojipa muda wa kuusaka ukweli tutakuja kumuelewa Rais Magufuli akiishaoondoka madarakani kwa sababu ukweli unatabia ya kuchelewa lakini lazima ufike na unapofika unatabia ya kuwasumbua walioupuuza. Mzee Kikwete alipokuwa madarakani aliitwa dhaifu, leo ameondoka tunammis.

Burundi wanaendelea na kampeni za uchaguzi lakini hutosikia kelele, Tanzania kulegeza lockdown imekuwa agenda ya Dunia. Hapo ndo ujue wazungu wanahofu sana na Tanzania kwa sababu wanaujua mziki wake. Wakizubaa Afrika yote itakombolewa na Tanzania kama tulivyozikomboa nchi za Kusini mwa Afrika. Siku za wazungu kuiburuza Afrika zinahesabika. Andry Rajoelina wa Madagasca, Nkurunziza kiboko ya WHO na Mzee Magufuli baba lao wameonyesha uanaume kipindi hiki cha covid -19! Musiba yeye anakwambia tunatakiwa kuwa na World Bank ya Afrika! Musiba bwana! Kingereza chake kina hoja!

Ni kweli covid-19 inaua. Kila kona ya dunia tunazika! Huzuni ni kubwa! Mistake Afrika tuliifanya mwanzoni kabisa. Covid-19 ilipoanza kuwasumbua wazungu na wachina tulitakiwa kufunga mipaka fasta, no mzungu kuingia Afrika. Imagine janga lingeanzia Afrika kama kuna mtu angekanyaga kwao. Hilo hawakutushauri kabisa, wanatushauri tujilockdown! Anyway ngoja twende kwenye hoja zangu saba. Ruksa kuzichana!

Hoja ya kwanza:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini Magufuli ameipinga vikali kanuni ya “Stay home, protect your family,” na kuruhusu watu kuchapa kazi. Mzee alijua hili ni janga ambalo haliwezi kuisha leo wala kesho, hata ukimwi, surua, kansa na pepopunda vilianza hivi hivi na hadi leo vipo kwa sababu ni miradi ya wazungu! Ni tabia ya wazungu kutunga mitihani na kutuuzia majibu.

Walitengeneza virusi vya kompyuta ili watuuzie ant-virus, wakatengeneza ukimwi ili watuuziee barakoa za ukimwa, walitengeneza kansa ili watuuzie mionzi na dawa za kupunguza maumivu, walirutubisha mbu ili watuuzie net za Bill Gates, waliua ardhi yetu kwa mbolea na viwatilifu ili watuuzie mbolea, bila mbolea na dawa za kunyinyizia huvuni! Hii nayo ni kazi kubwa ya Monsanto!

Mtego wa “Stay home, protect your family,” umewanasa wasiojielewa. Unastay vipi home na wakati maisha yako ni ya riziki ya mbwa mdomoni? Stay home, protect your family, feed them stone to perish!

Leo dunia imemuelewa Magufuli kwa sababu ukweli unatabia ya kuchelewa, muda umefika WHO wamerudia maneno ya Magufuli, waliobana, waliobana wameanza kuachia! Yaani akisema mwafrika mwenzako huamini, akisema mzungu unaamini. Bure kabisa! Jamani siyo kila mzungu ni padre, wengine ni mashetani! Magufuli angekuwa mzungu leo angepewa tuzo ya utabiri na WHO ingekuwa genge la waafrika lingetozwa faini kwa kututabiria Afrika kufa sana.

Hoja ya Pili:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini Magufuli ameukwepa mtego wa kutatua kero ya corona kwa kutumia kero kama walivyofanya jamaa zetu. Full kuwatandika viboko waliokaidi kufia ndani. Afrika bila kutoka huli! Wahenga waliposema riziki ya mbwa iko miguuni hawakuwa wajinga. Mnazuia misongamano kwa viboko halafu mnagawa chakula kwa misongamano! Magufuli akiwapuuza mnamind! Kweli ujinga ni tishio zaidi ya covid-19.

Gonjwa lenyewe tangu lianze, limeishakula watu chini ya laki nne duniani kwa miezi 6 iliyo pita, wakati takwimu zinaonesha kwa mwaka watu zaidi ya milioni 40 wanakufa kila mwaka kwa magonjwa mengine sasa hii asilimia 1 ya vifo vya wazungu kibao na waafrika kiduchu ina maana gani hadi BBC kuifanya Tanzania kuwa agenda ya Dunia? Kwamba wazungu wanatupenda sana au? Kama wangekuwa wanatupenda siwangetuamrisha tufunge mipaka wazungu na wachina wasilete corona kwetu?Halafu unapomuweka ndani mtu muda wote kinga si ndo zitaisha kabisa?

Hoja ya Tatu:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini kelele za media hazimuondoi Magufuli kwenye reli. Anajua siri ya media. Ukisikiliza mikogo ya BBC huwezi kukaa Tanzania, maana wote tunaumwa. Majirani wameanza kutukataa. Rwanda akipita mtanzania wanaziba pua. Kenya, Uganda, Zambia ndo kabisa hawataki kutusikia kwa sababu BBC imesema tunanuka covid-19!

Halafu BBC inatumia watoto wetu, kutuchonganisha Afrika na wao hawashituki. Wanashitukaje na wakati mkono unaenda kinywani? Hata Mobutu Seseko Kuku wa Zabanga alishituka baada ya kuishiwa utamu wazungu wakamtema kama jojo!

Sasa ngoja niongee kama mwalimu niliyefundisha masuala ya media kwa zaidi ya miaka 10 pale St. Agstine University of Tanzania kabla sijaachana na ajira! Ni hivi, media ina weza kumfanya shetani kuwa malaika na malaika kuwa shetani kwa sababu hucontrol fikra za watu, ndiyo maana tawala zenye mashaka zinaogopa sana media. “Kama lengo lako ni kubadilisha dunia, silaha sahihi na ya haraka ni media” alisema Tom Stoppard,mwandishi wa mshairi kutoka London. Waandishi wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein wa gazeti la The Washington Post mwaka 1972 waliangusha utawala wa Richard Nixon, Rais wa Marekani, tukio linalojulikana kama Water Gate Scandal.

Naendelea! Waisrael wanamiliki uchumi wa dunia kwa sababu ya media. Walijipatia utajiri wakati wa vita ya kwanza ya dunia pale walipotangaza habari za uongo kwamba Uingereza inapigwa, matajiri wa Uingereza wakauza hisa zao kwa waisraeli kwa hasara kubwa, mwisho wa vita Mwingereza akashinda, matajiri wakaishi kama mashetani na waisrael wakaishi kama malaika, wakajiita taifa teule la Mungu na wewe ukakazana kuwabariki ukidhani hawa ndo wale wa kwenye Biblia.

Thomas Jefferson, rais wa tatu wa Marekani aliwahi kusema, “Ningeambiwa kuchagua kuwa na serikali bila magazeti au magazeti bila serikali nisingesita kuchagua jibu la mwisho”. Imani ya Jefferson ni kwamba vyombo vya habari vina nguvu zaidi ya serikali. Mwaka 1683, mfalme mmoja huko England aliamrisha maktaba ya chuo kikuu cha Oxford ichomwe moto, na ikachomwa kweli kwa sababu alimuogopa bwana Information is Power! Mwaka 1633, John Twyn, alikatwa vipande vipande hadi kufa baada ya kusambaza chapisho lilitowataka watu wauangushe utawala wa kifalme nchini Uingereza.

Corona inaua sana wazungu lakini kelele za BBC ni Afrika hasa Tanzania. Lengo ni kutuvuruga tu. Ona sasa tumeanza kubaguana sisi kwa sisi! Tunashindana kujifungia ndani ili wazungu watuuzie vyakula vya GMO, tuvile tuishiwe nguvu za kuzalisha watu na mali, waje watawale Afrika.

Sasa Magufuli anapojaribu kuzipuuza taarifa hizo wazungu wanakasirika na mamluki wao wanakuja juu ili wapewe misaada. Tangu lini mtu aliyemuua babu yako akusaidie? Anyway kwa wale mnaosomea maswala ya media hebu tafuteni kitabu changu, kinaitwa “Ethical Journalism: A voice of the Voiceless”, kinapatikana Amazoni, ukishindwa basi lipia kwa mpesa 0753665484 nikutumie sasa hivi. Unajua ili ufanye biashara utakiwa kuwa na akili kwanza, halafu pesa baadaye! Vijana wetu wanataka pesa kwanza ndo wakafanye biashara!

Hoja ya Nne:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na kasi ya kufikiri hatutaelewa kwa nini Magufuli aliamua kupeleka ndege ya serikali kuchukua dawa ya corona Madagascar. Alichofanya Magufuli ni kupambana na fikra kwamba hatuwezi kuishi bila wazungu, kumbe wao ndo hawawezi kuishi bila sisi.

Sisi tumeishi bila wao kwa zaidi ya miaka milioni nne iliyopita na tukafanya makubwa. Wazee wetu waliishi hadi miaka 100 wakitibiwa kwa mitishamba na matunda. Leo tumeacha dawa za asili, zilizopatikana kwa bure kabisa tukaparamia dawa za kizungu matokeo yake Afrika imejaa wagonjwa endelevu, wanaoishi kwa gharama kubwa kutajirisha viwanda vya mzungu. Ndo maana Rajoelina alivyogundua dawa hiyo WHO imekuja juu ati haina viwango na viongozi wa Afrika tukaamini propaganda hizo kwa sababu tumesahau historia yetu. Akivumbua mweusi hakifai, akivumvua mzungu kinafaa.

Jamani kuendelea kutibiwa kwa dawa za wazungu ni kuhalalisha kifo. Hakuna aliyewahi kupona kwa dawa za kizungu. Kelele za siku hizi malaria haiponi zimekuwa nyingi, taifodi na UTI ndo usiseme!

Jibu ni kurudi Afrika. Ni magonjwa mangapi yameshindikana hospitali za wazungu lakini yamepona kwa waganga wa jadi? Hatuhitaji kutumia hata senti tano kununua dawa za kizungu. Mungu anatushangaa na shetani anatucheka tunavyotumia pesa nyingi kuagiza dawa kutoka Ulaya kusiko na milonge, alovera na mayai ya nyoka.

Mzungu hawezi kukuletea dawa upone afunge viwanda vyake kwa sababu kufa kufaana. Walau sasa watanzania tumeanza kujifukiza, hii ni ishara ya kurudi Afrika. Mh. Jafo alitamani tuwe na wiki ya nyungu kabisa, watunga sera sidhani kama watamuelewa, ila siku ya ukimwi duniani wanaielewa. Jafo angekuwa mzungu tungepiga nyungu hadibadani.

Hoja ya Tano:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na kasi ya kufikiri tutajikuta kwenye mtego kumponda Magufuli kuwafurahisha wazungu ili watufadhili! Ati mzungu akufadhili, amekuwa mjomba wako? Kwanza mbele ya mzungu unaokena nyani tu halafu utake akufadhili. How? Mtu aliyekupiga na kukutenganisha na Mungu wako kwamba ni mshenzi na kusema usimuite Ngai, Imana, Kyala, Nguluvi, Mulungu badala yake umuabudu Yahwe, Allah na God hawezi kuwa mfadhili, mtu anayeziita nchi zetu third world countries na wakati Mungu aliumba dunia moja hawezi kukufadhili kitu, mtu aliyetupeleka mateka kwa miaka mia saba na kutufanyia ukatili wa kutisha hawezi kukufadhili kitu, mtu anayetudai kwa riba kubwa na wakati alitakiwa atulipe fidia kwa damage aliyotufanyia mpaka Afrika ikawa na umaskini wa kunuka ndani ya utajiri wa kutupwa hawezi kukufadhili kitu huyo. Huyo ni adui. Adui yako muombee njaa, adui yako mmalize ni maneno kuntu ya wahenga kuwaamsha waliolala. Nkurunziza wa Burudi amewatimu, Rejoelina amesema msitupangie, Magufuli kawaambia kama mnataka kuzisaidia nchi masikini zifutieni madeni acheni mbwembwe.

Mzee Robert Mugabe alisema mkoloni wa jana haweza kuwa rafiki yako, ukarimu wa mzungu ni sawa na ukarimu wa mchinja kuku, atamrushia mahindi ili amnase akamchinje! Mtu kakupeleka utumwani kwa pingu kama mwizi wa kuku, wamemuua ndugu yako Sankara, Lumumba na Gadafi halafu unasema ni ndugu zako, wameleta corona, ukimwi, presha, ebola, wameiba mali zetu, waliondoka na vichwa 2500 vya machifu wa Afrika halafu leo unadhani wanakupenda kwa jina la covid-19.

Unajikomba ili akupe misaada! “Lords of Poverty,” Mwandishi wa “Lords of Poverty” anasema misaada wanayotoa wazungu siyo kwa lengo la kusaidia Afrika bali kujisaidia wao ndo maana wanasambaza unga uliooza, waliwahi kuleta unga ambao hata ng’ombe wa St. Francisco walishindwa kula. Hivi kweli mtu anakuita ameshika kisu utakwenda? Hata mbwa hawezi kwenda!

Hoja ya Sita

Nasema hivi usipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hata haya mawazo yangu utayapiga rungu na wakati Mzee Kikwete alisema hoja hazipigwi Rungu! Hoja hupingwa kwa hoja nzuri zaidi, marungu waachie wanamgambo na washirikina.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hata kama wazungu ni wabaya,
Kwanzaa uwezi kuhukumu kizazi cha sasa hv kwa madhambi waliyofanya babu zao miaka 200+iliyopita,
Scandali za Richmond, melemeta, ufisadi wa kuuza nyumba za serikali,hazikufanywa na wazungu, kuna kada wa ccm alikuwa anazalisha ARV feki, sio mzungu.
South sudani,wanaochinja na kuua raia wa kawaida, sio wazungu!
Africa hatuta fika popote kama kila baya linalotokea tunasingizia wazungu,
Ili hao wazungu watuheshimu, lazima tuweke mchango wetu mezani, katika kila nyanja, sayansi, kilimo, tekinolojia, siasa, elimu
Mpaka leo, miaka 60+ baada ya uhuru, hatuwezi kuzalisha sukari ya kututosha,! Nafikiri tungeanzia hapa kwanza, kuriko kuleta "mijimwambafications"mingi mbele ya nchi za magharibi!
Wakati Ghadafi anakula kichapo, nchi gani ya kiafrika, ilileta fyoko! Si SA wala Nigeria, iliyopaza sauti,
Kama nchi kama Urusi, Iran, North Korea, na China, huwa wanashika adabu wakiwekewa vikwazo, sembuse sisi!
Hii vita sio ya kitoto, inahitaji weledi na mikakati madhubuti,sio mbwembwe za kutumbuana tu, mkipishana kauli, au kutuma wasiojurikana, waue, watese

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenikumbusha aya magonjwa Pepopunda, Surua, Tetekuwanga, Kisonono, Kaswende, Kifaduro, etc etc hivi na wazungu wanaugua aya magonjwa au ni sisi tu Africa

Sent from my iPhone using JamiiForums
ww unafikiria tukiwa na wapumbavu Kama ww kufikiria kila jambo la Wazungu ni jema kwetu?
 
Wewe unae andika huu upupu ndo huyo huyo utakuja na ngojera na serikali kujenga hospital nyingi awamu hii na kuongea budget ya madawa, consistency kwenu huwa haipo mnaenda na tune ya mwenyekiti
Tatizo kubwa naloliona wala si kwako peke yako, watu wengi hasa vijana mmefunga bongo zenu kiasi cha kudhani kila mtu lazima afuate msimamo au mawazo ya mtu mwingine. Hili si sawa hata kidogo
 
Suala la Covid 19 si la uficho liko wazi kabisa kila nchi inaweza kuact vile inaona itafaa zaidi wala si la kumzodoa mtu wakati kila ukifungua vyombo vya habari popote ulimwenguni hali ni tete dawa hakuna hadi sasa na waliofanya lockdown wote tumeona mwisho wake wameachia na hali ya kusambaa kwa virusi iko palepale ulifanya au hukufanya lockdown covid 19 imewafuata watu hadi majumbani mwao hili jambo la likimwengu watu tunaamka kila siku kumsema rais kana kwamba yy ndiye aliyetengeneza virus wa covid 19 na ukitaka kujua kwamba waafrika tunafeli sana kwenye siasa ndio hapa kwa sababu wazungu wamesema basi wote tunatakiwa kuingia shimoni na wala hatujiulizi kwa nn wenzetu wakisikia jambo letu zuri wanajitahid kwa hali na mali kulichafua.kinachohitajika ni kupata dawa na watu kupona kwa dawa hiyo,wenzetu Madagascar wamepata dawa na watu wanapona,sasa angalia tu tangu wametangaza dawa ile reaction ya WHO ikoje ni mambo yanayosikitisha sana kwa mtu mwenye kufikiri kwa utimamu kamili wa kiakili.kumbe jibu tunalopata hapa ni kwamba tunatakiwa kusubiri dawa kutoka Marekani na ulaya au Asia hivyo ni vema sana tukatafakari kwa undani na magonjwa tusiyageuze kuwa siasa watanzania na waafrika kwa ujumla tuna kazi kubwa kwanza ya kukombolewa kimawazo hilo ndio la kwanza kabisa maana tukifanikiwa kutoka hapo tutakuwa tumeondolewa ukuta mkubwa unaosababisha tusione upande wa pili kuna nn kinacho endelea.
 
Baadhi ya viongozi makini ktk nchi za Africa wanakataa kupangiwa nn cha kufanya na nchi za ulaya,bahati mbaya Africa ya leo viongozi hao ni wachache sana baada ya kuondoka akina kwame nkrumah,jommo kenyatta,JK Nyerere,Nelson Mandela,na wengine wengi,Afrika inarudi kwenye umaskini mkubwa wa kuendelea kuamini kwamba we are not the source of knowledge ni hatari kubwa sana na kuonyesha ujinga wetu zaidi tunamuwenga mtu mmoja huku tukisahau kuwa janga ni la ulimwengu mzima na walimwengu wote wanalia kila mtu kivyake na nchi nyingi duniani zinafanya trial and error kupata dawa lakini wapi kama ndio ulaya na marekani imeshindikana lkn Africa na China dawa zipo ile iliyopo Madagascar ndio hiyo iliyo wapa unafuu China na bahati mbaya China hawezi kumshirikisha hasimu wake Mmarekani anataka hadi akione cha mtema kuni.Ndugu zetu Madagascar wamefungua mashule na vyuo ss tumekaa kila kukicha tunamsema vibaya Rais wa nchi yetu badala ya kuonyesha dawa itakayo saidia.
 
Me nimefurahi sana, tangu wameqcha kutoa takwimu za wagonjwa wa korona na vifo hali mtaani imerejea kawaida.
Huu ugonjwa una ajenda ya siri, ndo maana wanang'ang,ania kutangaza habari mbaya tu kuhuusu.
Hawatangazi kwa nguvu kuwa watu wengi wanapona kuliko wanaokifa.
Hawatangazi kuwa watu wengi wanaoambukizwa hawaonyeshi dalili na wanapona.
Hawasisitizi kuwa vijana na watoto hawafi kwa ugonjwa hui.
Wamekaa kusisitiza habari mbaya ili kutia watu hofu. Na ukipata hofu kinga inapungua. Ukipata ugonjwa wowote utashindwa kupambama.
Ndo maana wanasisitiza kuhusu takwimu za vifo na wagonjwa.
 
Unahitaji utulivu wa akili na umakini katika kufikiri ili kumuelewa Magufuli kelele za Covid-19: Hoja Sita!

Denis Mpagaze
___________________________
Katika kipindi hiki cha corona na propaganda za magharibi, tusipojipa muda wa kuusaka ukweli tutakuja kumuelewa Rais Magufuli akiishaoondoka madarakani kwa sababu ukweli unatabia ya kuchelewa lakini lazima ufike na unapofika unatabia ya kuwasumbua walioupuuza. Mzee Kikwete alipokuwa madarakani aliitwa dhaifu, leo ameondoka tunammis.

Burundi wanaendelea na kampeni za uchaguzi lakini hutosikia kelele, Tanzania kulegeza lockdown imekuwa agenda ya Dunia. Hapo ndo ujue wazungu wanahofu sana na Tanzania kwa sababu wanaujua mziki wake. Wakizubaa Afrika yote itakombolewa na Tanzania kama tulivyozikomboa nchi za Kusini mwa Afrika. Siku za wazungu kuiburuza Afrika zinahesabika. Andry Rajoelina wa Madagasca, Nkurunziza kiboko ya WHO na Mzee Magufuli baba lao wameonyesha uanaume kipindi hiki cha covid -19! Musiba yeye anakwambia tunatakiwa kuwa na World Bank ya Afrika! Musiba bwana! Kingereza chake kina hoja!

Ni kweli covid-19 inaua. Kila kona ya dunia tunazika! Huzuni ni kubwa! Mistake Afrika tuliifanya mwanzoni kabisa. Covid-19 ilipoanza kuwasumbua wazungu na wachina tulitakiwa kufunga mipaka fasta, no mzungu kuingia Afrika. Imagine janga lingeanzia Afrika kama kuna mtu angekanyaga kwao. Hilo hawakutushauri kabisa, wanatushauri tujilockdown! Anyway ngoja twende kwenye hoja zangu saba. Ruksa kuzichana!

Hoja ya kwanza:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini Magufuli ameipinga vikali kanuni ya “Stay home, protect your family,” na kuruhusu watu kuchapa kazi. Mzee alijua hili ni janga ambalo haliwezi kuisha leo wala kesho, hata ukimwi, surua, kansa na pepopunda vilianza hivi hivi na hadi leo vipo kwa sababu ni miradi ya wazungu! Ni tabia ya wazungu kutunga mitihani na kutuuzia majibu.

Walitengeneza virusi vya kompyuta ili watuuzie ant-virus, wakatengeneza ukimwi ili watuuziee barakoa za ukimwa, walitengeneza kansa ili watuuzie mionzi na dawa za kupunguza maumivu, walirutubisha mbu ili watuuzie net za Bill Gates, waliua ardhi yetu kwa mbolea na viwatilifu ili watuuzie mbolea, bila mbolea na dawa za kunyinyizia huvuni! Hii nayo ni kazi kubwa ya Monsanto!

Mtego wa “Stay home, protect your family,” umewanasa wasiojielewa. Unastay vipi home na wakati maisha yako ni ya riziki ya mbwa mdomoni? Stay home, protect your family, feed them stone to perish!

Leo dunia imemuelewa Magufuli kwa sababu ukweli unatabia ya kuchelewa, muda umefika WHO wamerudia maneno ya Magufuli, waliobana, waliobana wameanza kuachia! Yaani akisema mwafrika mwenzako huamini, akisema mzungu unaamini. Bure kabisa! Jamani siyo kila mzungu ni padre, wengine ni mashetani! Magufuli angekuwa mzungu leo angepewa tuzo ya utabiri na WHO ingekuwa genge la waafrika lingetozwa faini kwa kututabiria Afrika kufa sana.

Hoja ya Pili:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini Magufuli ameukwepa mtego wa kutatua kero ya corona kwa kutumia kero kama walivyofanya jamaa zetu. Full kuwatandika viboko waliokaidi kufia ndani. Afrika bila kutoka huli! Wahenga waliposema riziki ya mbwa iko miguuni hawakuwa wajinga. Mnazuia misongamano kwa viboko halafu mnagawa chakula kwa misongamano! Magufuli akiwapuuza mnamind! Kweli ujinga ni tishio zaidi ya covid-19.

Gonjwa lenyewe tangu lianze, limeishakula watu chini ya laki nne duniani kwa miezi 6 iliyo pita, wakati takwimu zinaonesha kwa mwaka watu zaidi ya milioni 40 wanakufa kila mwaka kwa magonjwa mengine sasa hii asilimia 1 ya vifo vya wazungu kibao na waafrika kiduchu ina maana gani hadi BBC kuifanya Tanzania kuwa agenda ya Dunia? Kwamba wazungu wanatupenda sana au? Kama wangekuwa wanatupenda siwangetuamrisha tufunge mipaka wazungu na wachina wasilete corona kwetu?Halafu unapomuweka ndani mtu muda wote kinga si ndo zitaisha kabisa?

Hoja ya Tatu:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hatutaelewa kwa nini kelele za media hazimuondoi Magufuli kwenye reli. Anajua siri ya media. Ukisikiliza mikogo ya BBC huwezi kukaa Tanzania, maana wote tunaumwa. Majirani wameanza kutukataa. Rwanda akipita mtanzania wanaziba pua. Kenya, Uganda, Zambia ndo kabisa hawataki kutusikia kwa sababu BBC imesema tunanuka covid-19!

Halafu BBC inatumia watoto wetu, kutuchonganisha Afrika na wao hawashituki. Wanashitukaje na wakati mkono unaenda kinywani? Hata Mobutu Seseko Kuku wa Zabanga alishituka baada ya kuishiwa utamu wazungu wakamtema kama jojo!

Sasa ngoja niongee kama mwalimu niliyefundisha masuala ya media kwa zaidi ya miaka 10 pale St. Agstine University of Tanzania kabla sijaachana na ajira! Ni hivi, media ina weza kumfanya shetani kuwa malaika na malaika kuwa shetani kwa sababu hucontrol fikra za watu, ndiyo maana tawala zenye mashaka zinaogopa sana media. “Kama lengo lako ni kubadilisha dunia, silaha sahihi na ya haraka ni media” alisema Tom Stoppard,mwandishi wa mshairi kutoka London. Waandishi wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein wa gazeti la The Washington Post mwaka 1972 waliangusha utawala wa Richard Nixon, Rais wa Marekani, tukio linalojulikana kama Water Gate Scandal.

Naendelea! Waisrael wanamiliki uchumi wa dunia kwa sababu ya media. Walijipatia utajiri wakati wa vita ya kwanza ya dunia pale walipotangaza habari za uongo kwamba Uingereza inapigwa, matajiri wa Uingereza wakauza hisa zao kwa waisraeli kwa hasara kubwa, mwisho wa vita Mwingereza akashinda, matajiri wakaishi kama mashetani na waisrael wakaishi kama malaika, wakajiita taifa teule la Mungu na wewe ukakazana kuwabariki ukidhani hawa ndo wale wa kwenye Biblia.

Thomas Jefferson, rais wa tatu wa Marekani aliwahi kusema, “Ningeambiwa kuchagua kuwa na serikali bila magazeti au magazeti bila serikali nisingesita kuchagua jibu la mwisho”. Imani ya Jefferson ni kwamba vyombo vya habari vina nguvu zaidi ya serikali. Mwaka 1683, mfalme mmoja huko England aliamrisha maktaba ya chuo kikuu cha Oxford ichomwe moto, na ikachomwa kweli kwa sababu alimuogopa bwana Information is Power! Mwaka 1633, John Twyn, alikatwa vipande vipande hadi kufa baada ya kusambaza chapisho lilitowataka watu wauangushe utawala wa kifalme nchini Uingereza.

Corona inaua sana wazungu lakini kelele za BBC ni Afrika hasa Tanzania. Lengo ni kutuvuruga tu. Ona sasa tumeanza kubaguana sisi kwa sisi! Tunashindana kujifungia ndani ili wazungu watuuzie vyakula vya GMO, tuvile tuishiwe nguvu za kuzalisha watu na mali, waje watawale Afrika.

Sasa Magufuli anapojaribu kuzipuuza taarifa hizo wazungu wanakasirika na mamluki wao wanakuja juu ili wapewe misaada. Tangu lini mtu aliyemuua babu yako akusaidie? Anyway kwa wale mnaosomea maswala ya media hebu tafuteni kitabu changu, kinaitwa “Ethical Journalism: A voice of the Voiceless”, kinapatikana Amazoni, ukishindwa basi lipia kwa mpesa 0753665484 nikutumie sasa hivi. Unajua ili ufanye biashara utakiwa kuwa na akili kwanza, halafu pesa baadaye! Vijana wetu wanataka pesa kwanza ndo wakafanye biashara!

Hoja ya Nne:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na kasi ya kufikiri hatutaelewa kwa nini Magufuli aliamua kupeleka ndege ya serikali kuchukua dawa ya corona Madagascar. Alichofanya Magufuli ni kupambana na fikra kwamba hatuwezi kuishi bila wazungu, kumbe wao ndo hawawezi kuishi bila sisi.

Sisi tumeishi bila wao kwa zaidi ya miaka milioni nne iliyopita na tukafanya makubwa. Wazee wetu waliishi hadi miaka 100 wakitibiwa kwa mitishamba na matunda. Leo tumeacha dawa za asili, zilizopatikana kwa bure kabisa tukaparamia dawa za kizungu matokeo yake Afrika imejaa wagonjwa endelevu, wanaoishi kwa gharama kubwa kutajirisha viwanda vya mzungu. Ndo maana Rajoelina alivyogundua dawa hiyo WHO imekuja juu ati haina viwango na viongozi wa Afrika tukaamini propaganda hizo kwa sababu tumesahau historia yetu. Akivumbua mweusi hakifai, akivumvua mzungu kinafaa.

Jamani kuendelea kutibiwa kwa dawa za wazungu ni kuhalalisha kifo. Hakuna aliyewahi kupona kwa dawa za kizungu. Kelele za siku hizi malaria haiponi zimekuwa nyingi, taifodi na UTI ndo usiseme!

Jibu ni kurudi Afrika. Ni magonjwa mangapi yameshindikana hospitali za wazungu lakini yamepona kwa waganga wa jadi? Hatuhitaji kutumia hata senti tano kununua dawa za kizungu. Mungu anatushangaa na shetani anatucheka tunavyotumia pesa nyingi kuagiza dawa kutoka Ulaya kusiko na milonge, alovera na mayai ya nyoka.

Mzungu hawezi kukuletea dawa upone afunge viwanda vyake kwa sababu kufa kufaana. Walau sasa watanzania tumeanza kujifukiza, hii ni ishara ya kurudi Afrika. Mh. Jafo alitamani tuwe na wiki ya nyungu kabisa, watunga sera sidhani kama watamuelewa, ila siku ya ukimwi duniani wanaielewa. Jafo angekuwa mzungu tungepiga nyungu hadibadani.

Hoja ya Tano:

Tusipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na kasi ya kufikiri tutajikuta kwenye mtego kumponda Magufuli kuwafurahisha wazungu ili watufadhili! Ati mzungu akufadhili, amekuwa mjomba wako? Kwanza mbele ya mzungu unaokena nyani tu halafu utake akufadhili. How? Mtu aliyekupiga na kukutenganisha na Mungu wako kwamba ni mshenzi na kusema usimuite Ngai, Imana, Kyala, Nguluvi, Mulungu badala yake umuabudu Yahwe, Allah na God hawezi kuwa mfadhili, mtu anayeziita nchi zetu third world countries na wakati Mungu aliumba dunia moja hawezi kukufadhili kitu, mtu aliyetupeleka mateka kwa miaka mia saba na kutufanyia ukatili wa kutisha hawezi kukufadhili kitu, mtu anayetudai kwa riba kubwa na wakati alitakiwa atulipe fidia kwa damage aliyotufanyia mpaka Afrika ikawa na umaskini wa kunuka ndani ya utajiri wa kutupwa hawezi kukufadhili kitu huyo. Huyo ni adui. Adui yako muombee njaa, adui yako mmalize ni maneno kuntu ya wahenga kuwaamsha waliolala. Nkurunziza wa Burudi amewatimu, Rejoelina amesema msitupangie, Magufuli kawaambia kama mnataka kuzisaidia nchi masikini zifutieni madeni acheni mbwembwe.

Mzee Robert Mugabe alisema mkoloni wa jana haweza kuwa rafiki yako, ukarimu wa mzungu ni sawa na ukarimu wa mchinja kuku, atamrushia mahindi ili amnase akamchinje! Mtu kakupeleka utumwani kwa pingu kama mwizi wa kuku, wamemuua ndugu yako Sankara, Lumumba na Gadafi halafu unasema ni ndugu zako, wameleta corona, ukimwi, presha, ebola, wameiba mali zetu, waliondoka na vichwa 2500 vya machifu wa Afrika halafu leo unadhani wanakupenda kwa jina la covid-19.

Unajikomba ili akupe misaada! “Lords of Poverty,” Mwandishi wa “Lords of Poverty” anasema misaada wanayotoa wazungu siyo kwa lengo la kusaidia Afrika bali kujisaidia wao ndo maana wanasambaza unga uliooza, waliwahi kuleta unga ambao hata ng’ombe wa St. Francisco walishindwa kula. Hivi kweli mtu anakuita ameshika kisu utakwenda? Hata mbwa hawezi kwenda!

Hoja ya Sita

Nasema hivi usipojipa muda wa kuusaka ukweli katika utulivu wa akili na umakini wa kufikiri vizuri hata haya mawazo yangu utayapiga rungu na wakati Mzee Kikwete alisema hoja hazipigwi Rungu! Hoja hupingwa kwa hoja nzuri zaidi, marungu waachie wanamgambo na washirikina.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mungu ni mwema daima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom