Unahitaji kuwa mshindi kwanza? Vitu vya kuzingatia katika uandishi

David M Mrope

Senior Member
Jul 13, 2021
115
72
Uandishi ni taaluma kama ilivyo taaluma zingine za ualimu,udaktari na nyingine nyingi sana ambazo wengi hukimbilia. Hii taaluma watu ambao hukaa darasani na kuisomea ni wachache sana japo ni miongoni mwa taaluma muhimu sana. Wengi hutumia mapenzi yao tu na kujikuta wakiandika makala mbalimbali bila kujua undani zaidi.

Sasa katika hili shindano ambalo limetuvutia watu wengi na kujikuta tunazama haraka haraka, nimeamua kukuletea baadhi ya sheria ambazo unatakiwa uzingatie wakati wa uandishi wako. Kwahiyo ili uandike hadithi au makala fupi ya kuvutia lazima uzingalie vitu vifuatanyo.

(i) JUMBE YAKO LAZIMA IWE NA SEHEMU KUU NNE
Kila jumbe ambayo unaiandika lazima iwe na sehemu hizi nne,kumbuka hapa unatakiwa uandike jumbe ambayo imeshiba ili msomaji apate kitu flani cha tofauti na wengine.

Sasa hakikisha unakuwa na kichwa,utangulizi,mwili na hitimisho. Kazi yako yoyote hakikisha unaichapisha kwa kuzingatia vitu hivyo vinne.

KICHWA
Hii ni sehemu ya kwanza ambayo huandikwa kwa maneno machache sana lakini yanayobeba dhumuni la jumbe yako.
Kichwa huwa katika mfumo wa fumbo au swali,hii husaidia kumvuta msomaji. Mara nyingi huwa mstari mmoja.

UTANGULIZI
Hii ni sehemu ya juu ambayo huelezea kichwa kwa maneno machache yasiyochosha. Utangulizi mara nyingi humaliziwa na sentensi inayokupa shauku ya kuendelea kujua kipi kinaendelea mbele.

MWILI
Hapa ndipo dhamira ya jumbe yako imelala. Kule mwanzo ulikuwa unamvuta msomaji tu ili asipuuze jumbe yako. Katika kipengere hiki hutakiwi kuweka mbwembwe zozote zaidi ya kushusha dhamira yako.

HITIMISHO

Hii ni sehemu ya mwisho ya jumbe yako ambayo huandikwa kwa mistari michache tu. Hapa unashukuru na kukazia ujumbe wako. Unaweza taja jina lako na mawasiliano yako pia.

(ii) MPANGILIO WA JUMBE YAKO

Msomaji anaweza soma jumbe yako yote vizuri,lakini akaelewa baada ya kurudia mara mbili au tatu. Hii hutokana na mpangilio wa ovyo.

Hakikisha unavyoandika jumbe unaiweka katika mpangilo wa kupokeana. Yaani unapomaliza kipengere kimoja unamaliza kwa sentensi ambayo inaipokea hatua inayofuata na kuiaga hatua unayoiacha.

Mfano; ...kwahiyo hizo ndizo sifa za uyoga,sasa twende tukaangalie tabia za uyoga ambazo ni;

(iii) ZINGATIA MATUMIZI YA LUGHA
Hiki kitu watu kufikiri cha kawaida tu na wengi wanachanyanya lugha ilimradi tu wamefikisha ujumbe. Lakini katika sheria za uandishi zinamtaka mwandishi kutumia lugha kuu moja tu. Na neno utaloandika kwa kutumia lugha za ziada lazima liwekewe alama za fungua semi na funga semi("....") au mabano (...).

Hakikisha neno lolote la lugha ya ziada unatakiwa ulitolee maana kabla ya kuliandika kisha unaliandika mbele.

(iv) ZINGATIA ALAMA ZA UANDISHI VIZURI

Ni bora ukakosa hili shindano lakini ukawa umepata kitu kipya katika uandishi wako. Hakikisha panapo hitaji mkato weka mkato,nukta weka nukta,funga semi weka funga semi,panapohitaji herufi kubwa weka herufi kubwa.

Hizi alama za uandishi ziliwekwa ili zitumike katika uandishi. Sasa inapotokea waandishi wenyewe hawafuati ni tatizo tena. Kumbuka sentensi moja isizidi mistari miwili.

(v)ZINGATIA KIWANGO CHA ELIMU YA MSOMAJI

Jambo la mwisho na muhimu sana ambalo ndio gumu kupita yote ni hili. Waandishi wengi hujisahau sana na unakuta jumbe zao zinakera wasomaji.

Lazima unapoandika jumbe ujue unawaandikia watu wa aina gani. Mfano huwezi andika ujumbe ambao unaendwa kusomwa na watu wenye shahada na ukaanza kuleta matani matani mengi yasiyo na maana,watautupa huko.

Sasa unapoandika jumbe yako hapa jamiiforums kabla hujaachia hadharani lazima ujiulize kweli mtu mwenye elimu yeyote anaweza kuisoma na kuelewa?.

Basi hayo yalikuwa machache kuhusu namna ya uandishi. Niwapongeze washiriki wote na tuendelee na kazi yetu pendwa ya uandishi.

DAVID M MROPE.
SUA.
 
Nashukuru Bwa Devi kwa kutupa elimu. Naomba tafadhali uniongezee ufahamu kwenye maneno haya "Ujumbe" na "Jumbe" nimeona hili la Jumbe umelitumia sana kwenye hii makala
 
Asante sana.
JUMBE-Wingi.
UJUMBE-Umoja.

Ni maneno yenye maana sawa.
 
Mbona naona kama kazi ya kupiga kura itakuwa ngumu sana labda mods wachambue makala kama 100 halafu ndizo tuzipigie kura
 
Back
Top Bottom