Unahitaji kiasi gani kumsaliti mpenzi wako uliyenae sasa?

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,045
2,821
Habari zenu wote.
Tuje katika mada, kuna mdada mmoja takribani hii ni wiki ya tatu sasa naomba mapenzi kwake ila kaniwekea ngumu, kumuuliza kasema sio siri yeye anampenda sana mpenzi wake aliye nae na afikirii kumsaliti kwa mazingira ya kawaida labda alogwe. Kiukweli hata Mimi nipo katika mahusiano ya kupika na kupakua sema tu wanaume tuna tamaa sana na huyu naona kama ni upgrade wa niliyenae sasa. Mtusamehe wake zetu.

Nilipolichunguza jibu lake nikafikiri kuna majambo naweza fanya kumpata huyu mtu. Jibu la kwanza amesema kulogwa ila sikuafiki kumloga mwanamke katika dunia ya sasa, nikapuuza. Alternative yake nikasema pesa inaweza kuwa mchawi na mlozi mkuu kwake. Hili nikaliona ndio liwe wazo la kwanza. Nikalisave kulipitisha.

Nikarudi zangu kwa Mara nyingine kwa yule mdada, ohh Candy unajua nakupenda sana, sasa nakuomba nisaidie kiasi gani kinatosha kupoza maumivu ya kum cheat your man? Kainama akacheka mwisho akasema acha apate muda afikiri. Usiku wa kuamkia Leo kanitumia message angalau 250k, hii angalau anunue kitu kidogo cha kudumu cha ukumbusho wa usaliti wake.

Tangu message ile bado nawaza, kumbe kuna kiasi kila binadamu akipewa chatosha kusaliti mahusiano yake kulingana na status yake, hasa kwa wadada maana wanaume hawana dau bure yatosha. Sasa naomba kufaham je wewe binafsi kiasi gani kucheat mahusiano yako hasa kwa mtu uliempenda kutoka moyoni?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mapenzi haya sijui aliyeyaumba alichanganya na nini?

Upendo wa dhati haupo tena kabisa ndani ya mioyo ya wapendanao. Umebaki upendo wa kulinganisha na vitu au pesa!

Fikiria mpenzi wa huyo dada ,yawezekana kawekeza upendo kwa huyo binti na haelewi wala haambiwi kitu. Ila fikiria 250k zimemtoa kwenye reli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadunia kako kasi haka,, kwahiyo mnauziana dhambi?? Je hiyo pesa itakidhi shida zake zote milele na milele??
 
Ni kweli hiyo pesa sio ndefu.
Niawaweza kumpa kiasi chochote ni mpendaye sawa hali yangu...hata 15m nakuendelea, lakini napata taabu kununua ngono hata kwa 5k.
Hisia hakuna
Mahaba hakuna.
Yesu tuhurumie
Kadunia kako kasi haka,, kwahiyo mnauziana dhambi?? Je hiyo pesa itakidhi shida zake zote milele na milele??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mapenzi haya sijui aliyeyaumba alichanganya na nini?

Upendo wa dhati haupo tena kabisa ndani ya mioyo ya wapendanao. Umebaki upendo wa kulinganisha na vitu au pesa!

Fikiria mpenzi wa huyo dada ,yawezekana kawekeza upendo kwa huyo binti na haelewi wala haambiwi kitu. Ila fikiria 250k zimemtoa kwenye reli!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijajua hata mimi, ila nahisi alichanganya na super glue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom