Unahisi kwanini huyu anapendwa na Watanzania kwa sasa?

the deadline

Member
Sep 26, 2013
62
106
Dar es Salaam.Tarehe na mwezi kama wa leo miaka 67 iliyopita alizaliwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Leo Jumamosi akiwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa salamu mbalimbali zimetolewa kumtakia heri na maisha marefu.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa wanasiasa na wasanii hawakuwa nyuma kumtumia salam za heri, kiongozi huyo aliyesifika kuwa karibu mno na wasanii wakati wa uongozi wake.

Julius Mtatiro ni miongoni mwa walimtakia heri, ujumbe wake ulisomeka, “Happy birthday Mr President. Ulitufundisha huko nyuma kuwa siasa si uadui. Ulifanya makosa mengi kwenye uongozi wako, ulifanya mazuri mengi pia. Kwa sasa tunachoweza ni kukutakia umri mrefu,”

Muigizaji Jacob Stephen (JB) amendika, “Wasanii wa fani mbalimbali wanakupenda mno kwa sababu ulionyesha upendo wa dhati… na hilo lilisababisha watu wote kuwaheshimu wasanii..Mungu akubariki, akupe haja ya moyo wako Rais mstaafu Jakaya Kikwete,”

Jackline Wolper ameandika, “Dady kabisa wa Taifa leo kazaliwa… happy birthday mshua tunakuzimia na kukukumbuka juu,”
 

Attachments

  • Kikwete+pic.jpg
    Kikwete+pic.jpg
    20.1 KB · Views: 75
Wanaomaifia ni wanafiki tu....hakuna raisi wa Tz anayestahili sifa maana mikataba yote ya kipuuzi wameisign wao wakiwa na akili timamu..

Labda wasanii ndio wamsifie JK maana wote tulishuhudia alivyokuwa anawapa favor wasanii..

Kwa wanasiasa kumsifia JK ni unafiki na uzandiki tu
 
Unaona umuhimu wa mtu pale anapoondoka kwenye nafasi,usishangae hata uncle wakaja kumkumbuka.
 
Back
Top Bottom