Unahisi Kukata Tamaa? Fahamu Vitu Vitakavyokupa Motisha ya Kusonga Mbele.

Jun 23, 2016
12
95
Habari ndugu mpambanaji?
Pole sana na majukumu ya kila leo ya kutimiza ndoto zako. Hakika mungu yu pamoja nawe, matunda ya juhudi zako yataonekana, we endelea kusonga mbele.

Katika makala yangu ya "Hizi ni Njia 9 Bora za Kufanikiwa Katika Jambo Lolote" (Hizi ni Njia 9 Bora za Kufanikiwa Katika Jambo Lolote.) Nilieleza Kuto kukata tamaa kua moja ya siri hizo katika kutafuta mafanikio, lakini katika kusaka mafanikio watu wengi sana wanafika sehemu wanakata tamaa na kushindwa kuendelea kusonga mbele kama ni ndoto basi anaacha ipotelee angani. Hili usikate tamaa lazima ugundue ni vitu gani vitakupa motisha ya kuendelea kusonga mbele, vifuatavyo ni miongoni mwa vitu ambavyo ukivitumia vizuri vitakusaidia sana kusonga mbele katika harakati zako.

1. Dhamira kuu, Lengo au Ndoto yako.
Katika kutafuta mafanikio lazima kuna ndoto au lengo unalotaka kutimiza. Uwezi kufanikiwa bila kujua unataka kufanikisha nini. Icho unachotaka kufanikisha ndio Lengo, Dhamira na Ndoto. Ukipenda kwa dhati icho unachotaka kukitimiza na ukadhamiria kweli kutaka kutimiza, daima utokatishwa wala kurudishwa nyuma na jambo lolote.

2. Watu uliochagua kua sehemu ya maisha yako.
Dah.!! yaani sijui nizungumzeje hapa?maana ni sehemu muhimu sana kwasababu hawa watu awasaidii tu peke yake kukufanya usonge mbele bali pia ufanya uonekani kua ni mtu wa aina gani. Kuna baadhi ya watu ni vigumu kuwaepuka kuwa sehemu ya maisha yako, watu hao ni wazazi na ndugu ambao ni sehemu ya familia au ukoo mfano Shangazi, mjomba, bibi, babu na wengine wengi. Wala usijilaumu wewe kua sehemu ya hao watu ata kama ni Masikini, awajasoma, awanamuelekeo au wanatamaduni mbaya, kwasababu huo wote ni mpango wa mungu na kazi ya mungu haina makosa. Ila bado unayo nafasi ya kutengeneza watu bora ambao nao ni muhimu sana, ambao wana nafasi kubwa sana ya kukufanya usonge mbele au urudi nyuma katika maisha yako. Watu hao ni Mwenza(mpenzi) na marafiki. Kuwa makini sana juu ya hawa watu, ukichagua watu ambao awaendani kabisa na malengo yako na ni watu wa kukatisha tamaa hakika icho unachokitamani na kukiangaikia akitakua daima, na kama kikikua sio kwa kiwango unachotarajia. Maana ili binadamu tusonge mbele tunahitaji watu wakutupa faraja, kutufundisha, kutupa motisha na kututia moyo katika malengo yetu.

3. Taarifa tunazopata na kuziishi kila siku.
Hapa tunazungumzia aina ya taarifa tunazopokea kila siku kwa kuona, kusikiliza au kusoma. Mara nyingi sana usikiliza nini, unaona na unasoma nini. Hivi ni vitu vya msingi sana. Hivi vitakusaidia kua na mtazamo chanya juu ya malengo yako na maisha kwa ujumla. Hapa napo ni sehemu muhimu sana, unakuta mtu labda ana ndoto ya kutaka kuwa mfanyabiashara maarufu sana lakini unakuta muda mwingi taarifa anazozipata kwenye ubongo wake ni za umbea(Ubuyu), Mapenzi na udaku. Akilala udaku, akiamka udaku. Aki-view instagram, page alizo-follow zote za udaku. Akisoma magazeti anasoma udaku na burudani. Akiangalia Tv anaangalia vipindi vya Udaku na burudani, Akisikiliza radio anasikiliza vipindi vya Udaku na burudani, akiongea na marafiki zake wanazungumzia udaku. Embu angalia, mtu wa aina hiyo alafu anataka awe bilionea. Hakika itakua ni vigumu. Katika sehemu ambayo unatakiwa kua makini sana ni hii sehemu ya taarifa unazopendelea kupata kila siku, na hii inajumuisha ata na vitabu unavyosoma. Mifano iko mingi sana lakini hakikisha sana unakua makini sana. Jitahidi ukiwa unasoma, soma vitabu vizuri ambavyo vitakujenga na kukufanya usonge mbele, tumia vizuri "social networks" kwa ku-follow page zenye maana, ku-interact na watu mitandaoni wenye maana.

4. Watu wa kuwaiga(Role Models).
Kwakweli hakuna ndoto mpya chini ya jua. Icho unachoota kilishatimizwa na watu. Hivyo kuna wimbi kubwa la watu ambao walishatimiza ndoto ambayo wewe unaiota sasa hivi au kunawatu ambao wamefanikiwa katika field nyingine ila wanaweza kukupa motisha na wewe katika field yako. Hivyo basi kama unataka kusonga mbele bila kukata tamaa lazima uwe na mtu wa kumuiga ambaye kila leo ukiamka unaamini na wewe utaweza kufanikiwa kama yeye au zaidi yake. Hii aitakusaidia tu kwenye kukata tamaa peke yake bali ata katika menendo ya tabia zako, utahitaji ufanye kama alivyokua yeye. Kwa mfano kwa wale wanasiasa ambao Role model wao mkubwa ni Mzee Nelson Mandela(Mungu amlaze mahali pema), uwezi kua mtu mwenye Chuki na kutothamini utu alafu ukasema unataka kuwa kama Mzee Mandela.

5. Nukuu(Quotes) unazopenda kuzisoma, Kuzisikiliza na kuziishi.
Najua kua huu si utamaduni wetu mkubwa sisi waswahili, lakini tunatakiwa tujifunze. Kuwa na vipande vya kauli mbalimbali kutoka kwa watu mashuhuri, vitabu au vitabu vitakatifu ambavyo vitakua vinatutia moyo wa kusonga mbele. Kwa mfano mimi nina Nukuu nyingi ambazo nimeziandika kwenye karatasi na kuzibandika kwenye kuta ya chumba ninacholala na kwenye kitanda, Nukuu hizo nikilala nazisoma na nikiamka nazisoma. Moja ya nukuu ambazo nasoma sana na naipenda ni "Upo ulivyo kutokana na vitabu unavyosoma na marafiki ulio nao", hii nukuu inanisaidia kujiamasisha kusoma sana vitabu ambavyo vitanijenga na pia ku-interact na watu ambao binafsi wanamchango mkubwa sana katika kutimiza ndoto zangu. Nukuu wakati mwingine ata wewe unaweza kujitengenezea ya kwako ila iwe na sifa kuu ya kukuamasisha kusonga mbele.

Maisha ni kuchagua, kufanikiwa na kushindwa kuko mikononi mwako ila unasababu nyingi sana tena sana za kushinda kuliko kushindwa. Nikutakie mafanikio mema katika harakati zako.


Mwaveso Abdallah Mbwana
+255 659 442 505
amwaveso@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom