Unahisi kuishiwa nguvu? Kabla hujakata tamaa, tutete hapa

Eliah Geofrey Kamwela

Senior Member
Dec 30, 2018
181
491
Mara nyingi maishani huwa tunafikia point ya kujihisi kuishiwa nguvu kabisa, hasa pale mambo yanapoonekana kugoma kwenda licha ya Juhudi tunazo Fanya. Hii hupelekea moyo kushuka na wengine hujiona si wa thamani tena na kujidharau na kujikatia tamaa. Wengine hufikia pabaya na kutamani kujiua!

SIKILIZA HABARI HII NJEMA!
Katika maeneo yote ya maisha, kabla kufanikiwa na kuinuka, hutanguliwa na kipindi cha kushindwa, kufeli na kuumizwa. Unafikaje kwenye hatima yako, inategemea sana na unatokaje katika kipindi kigumu kwako.

Matatizo na changamoto ni Kama tu msuguano(friction) katika barabara. Msuguano hupinga mwendo wa vitu kama magari, watu nk, na inahitaji nguvu kuushinda. Hata hivyo, msuguano usipo kuwepo, mwendo hushimdikana au huwa mgumu( kama huamini kajaribu kukimbia kwenye matope au barafu halafu utaleta mrejesho hapa).
Matatizo na changamoto huja ili kutusukuma tusonge mbele. In fact, akili ya binadamu hufanya kazi kwa kiwango cha juu kabisa kipindi cha matatizo!

Jambo la hakika ni kuwa mwisho wa siku, usiku utakwisha tu na kutakucha! Giza lisikuzuie kuchukua hatua ndogo ndogo ili kunapo kucha, uamkie ukiwa umesogeza mwendo .
Naamini MUNGU, hatakuacha ufie hapo.
Kutapambazuka tu na wale walio kuwa hodari kwa kiwango cha kutumia tochi au mshumaa ili waendelee kutembea watakuwa mbali kutakapo pambazuka.
USIOGOPE,MUNGU YU PAMOJA NAWE.

#Divine_Solutions_Carrier
 
Sawa mtumishi ila na nyie watumishi wa Mungu msiwe sehemu ya kuongeza stress kwa wananchi sadaka kumi kidogo mnataka mnategemea nini..

Mwishowe ndio tunayoyaona haya siku hizi watu wanatoa sadaka kwa pesa za bandia.
 
Hahaha, mkuu, Mie ni muumini tu wa kawaida kanisani, ila najua nguvu ya sadaka ikitolewa kwa ufahamu na kulingana na neno la Mungu. Jifunze kwanza kuhusu sadaka,ukielewa Ndio uanze kutoa. Pia sadaka yoyote ukihisi unasikia maumivu au utapeli Fulani USITOE kwa sababu utakua umeipoteza tu.
 
Mara nyingi maishani huwa tunafikia point ya kujihisi kuishiwa nguvu kabisa, hasa pale mambo yanapoonekana kugoma kwenda licha ya Juhudi tunazo Fanya. Hii hupelekea moyo kushuka na wengine hujiona si wa thamani tena na kujidharau na kujikatia tamaa. Wengine hufikia pabaya na kutamani kujiua!

SIKILIZA HABARI HII NJEMA!
Katika maeneo yote ya maisha, kabla kufanikiwa na kuinuka, hutanguliwa na kipindi cha kushindwa, kufeli na kuumizwa. Unafikaje kwenye hatima yako, inategemea sana na unatokaje katika kipindi kigumu kwako.

Matatizo na changamoto ni Kama tu msuguano(friction) katika barabara. Msuguano hupinga mwendo wa vitu kama magari, watu nk, na inahitaji nguvu kuushinda. Hata hivyo, msuguano usipo kuwepo, mwendo hushimdikana au huwa mgumu( kama huamini kajaribu kukimbia kwenye matope au barafu halafu utaleta mrejesho hapa).
Matatizo na changamoto huja ili kutusukuma tusonge mbele. In fact, akili ya binadamu hufanya kazi kwa kiwango cha juu kabisa kipindi cha matatizo!

Jambo la hakika ni kuwa mwisho wa siku, usiku utakwisha tu na kutakucha! Giza lisikuzuie kuchukua hatua ndogo ndogo ili kunapo kucha, uamkie ukiwa umesogeza mwendo .
Naamini MUNGU, hatakuacha ufie hapo.
Kutapambazuka tu na wale walio kuwa hodari kwa kiwango cha kutumia tochi au mshumaa ili waendelee kutembea watakuwa mbali kutakapo pambazuka.
USIOGOPE,MUNGU YU PAMOJA NAWE.

#Divine_Solutions_Carrier
I needed this words today.Thank you brother..

#Muungwana_John
 
Back
Top Bottom