Unahisi jambo gani ambalo silifahamu unaona shida kuniambia?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,590
2,000
Salaamu waungwana muwazima ndugu zangu

Well kichwa cha habari ilikua swali ambalo niliulizwa na mwenzangu kipindi cha nyuma kidogo wakati bado hatujafikia ndoa. Binafsi nilijiona kama mkosaji lakini pia nilipata nguvu ya kufunguka mengi yaliyo jificha kuhusu maisha yangu sababu sikuona mantiki ya kuweka siri tena ikiwa tu mwenzangu ametaka niwe muwazi kwake na ukizingatia nitakua nae rest of my life kama Mke.

So I had to dig deep ili tu asiwe na shaka na mimi na nitengeneze strong bond kati yetu, well haikua kazi rahisi lakini kiukweli nilifanikiwa kutua yote yaliyofichika sirini moyoni mwangu ili hata kama itatokea shida uko mbeleni isije kua big deal sababu ya price ya trust tuliyojijengea.

Hawa wenzetu ni watu muhimu sanaa hasa linapokuja swala la uhaminifu na kuaminiana katika ndoa sababu ni mstari unaotenganisha maisha ya u bachelor na ndoa.

Niweke wazi tu kuwa wanawake wengi wanaojielewa wanapenda kua confotable katika mahusiano hasa maisha ya ndoa ndio maana wengi wako selective sana tofauti na sisi watoto wa kiume tunaendeshwa kwa macho na miemko.

Niwasihi tu wenzangu ambao kweli mnataka kuoa na mfurahie ndoa zenu ndoa is so sweet hasa unapo oa umpendaye bila shinikizo au tamaa za mwili lakini pia mnapo fanikiwa kutengeneza trust yenye nguvu sana kati ya family yenu na mbele ya jamii kwa ujumla.

Kumbuka: Mke wako ni rafiki ako mkuu, mume wako ni rafiki ako mkuu usitafute wa ziada kumshirikisha mambo yako ya ndani zaidi ni yeye pekee anaekujua kwa karibu zaidi.
 

sam leon

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
892
1,000
Moja na vitu nimeshindwa ni kumwambia mwanamke kila kitu kuhusu mii.Sijui kwann ila siwezi aseeeee!!
 

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,590
2,000
Huwezi kuwa na mke mbaya. Ila ukibaniwa kama kawaida tunatafuta vipozeo . Wengine tunavieleza kuwa tumeoa ili visiwe na matumaini na wenzangu wanajaribu kuficha. UH mbaya jamani
Ukiamua kuoa kipozeo chanini kaka kinachokosekana ndani kitfutie suruhisho kinamna yako lakini sio mpango wa kando haujawahi kua njia sahihi

Haya mambo yana exist ukiwa huna Mke ukioa maana ake huna muda na upuuzi
 

-KANA-

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
3,969
2,000
For the very first time, nakutana na uzi wenye positive ideas about marriage!

Maana siku hizi kila Uzi huyu katendwa, huyu kafumaniwa, huyu anachepuka, yule kafanya vile!

Intact, mmekua mkituvunja moyo sisi ambao bado hatujaoa na mmekua mkituaminisha kua ndoa ni kamali.

Kila mtu anazungumzia mabaya ya ndoa as if hakuna mazuri. Hii ni mbegu mbaya for the young generation.

Thanx mkuu, atleast you said something positive!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom