Unafurahi Magufuli kubana, jioni unaniomba nikutoe hela

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,170
103,635
1. Unafurahi Magufuli kubana posho na maslahi kwa wafanyakazi, jioni unanipigia simu unaniomba nikutoe hata buku teni tu hali imekuwa mbaya.Halafu mwisho wa mwezi unataka nikuongezee nauli imepelea dogo aende shule.

2. Unasema watumishi wa umma tulikuwa tunaringa sana, bora Magufuli katukomoa, ukienda hospitali unaambiwa dawa hakuna na duka la binafsi inauzwa 30,000/= unanipigia simu unajanga nikusaidie

3. Unafurahi watumishi kubaniwa, jioni Unalalama kabiashara kako ka genge kanaenda ovyo, unashindwa kujua kama wateja wako watumishi wa umma tupo dhofli na purchasing power imekuwa chini sana. Tunanunua basic needs tu.

4. Unafurahi kibano wikend unanitumia sms mchango wa harusi, nitoe wapi sasa hela

Ndugu na jamaa waelewe kwamba ule uwezo kuliokuwa nao kuweza kusaidiana kama ndugu kwenye raha na matatizo ulitokana na maslahi mbalimbali ikiwepo posho, seminar, likizo nk. Kwa hiyo kwa kupigwa kwetu wamepigwa na wao pia.Mzunguko wa pesa kiasi kikubwa ulisababishwa na hayo. Kupitia kuungaunga huko tuliweza kusaidiana, kulipia madogo ada nk.

Kwa hiyo unapofurahia elewa kwamba, kwa kupigwa kwetu nawe umepigika
 
Kwani kukopa ni ajabu??hata Kwa Obama watu wanakopa na wanapigika kimaisha....mmeishiwa hoja
 
Yeah. Haya maumivu ni zaidi ya yale ya kupigwa kibuti. Mwenzenu menyu za kwenye hoteli za kifahari nimeshasahau zinafananaje! Kimbembe shemeji yenu analalamika mbona simtoi expensive dinners, anadai eti siku hizi simpendi kama zamani.
Hajui uchumi umeyumba!
Ripple effect is real!
 
Umenikumbusha rafiki zangu wanadharau kazi yangu cha ajabu wanapiga simu za kunikopa pesa.
Mara Mr naomba uniazime Tsh500,000 nitakulipa.
Wengine wamefunga biashara mimi naendelea na kazi yangu.
 
Hehehe hadi nyumba ndogo zimeyumba. Uzuri wake tutakaa sawa manake ecosystem nzima ita-adjust. UK nao wanaanza kuonja effect ya mabadiliko
Yeah. Haya maumivu ni zaidi ya yale ya kupigwa kibuti. Mwenzenu menyu za kwenye hoteli za kifahari nimeshasahau zinafananaje! Kimbembe shemeji yenu analalamika mbona simtoi expensive dinners, anadai eti siku hizi simpendi kama zamani.
Hajui uchumi umeyumba!
 
Potelea mbali, Ngoja hali iwe ngumu tu. tulikokuwa tunaelekea palikuwa panatisha kuna watu vyakula vilikuwa vinaoza wengine hawana. Je, Serikali hailipi mshahara, Nchi haiwezi kuendelea kwa kuwekeza kwenye warsha na semina elekezi, Badala ya kusafiri wataalamu kwenye ziara za kujifunza namna ya kukuza miji na kilimo cha kisasa na mambo ya technologia eti tulikuwa tunawapeleka wabunge wengine wameishia darasa la 7, wengine wamesoma lakini sio taaluma zinazowahusu kwenye taaluma husika. Hivi nyie hamkuwahi kusikitika kusikia Serikali inapewa mikopo na wafanyabiashara wa ndani tena sio kwajili ya maendeleo, ni kwaajili ya mishahara ya watumishi wake. Ngoja tu tulie wote, lakini kilio chetu hakitaenda bure
 
Chadema ni bora mngejikita kuhoji ni kwa nini Mbowe aliuza chama chenu???

Naamini bila mbowe kuuza chama msingekengeuka kiasi hiki.

Leo mnapinga kila kitu na kujidai mnadai democrasia wakati ndani ya chadema hamna hata tone la democrasia.
 
Hahahahaha dah! Hapa Nina kadi tano, na kila moja single 50,000 duh!
 
Chadema ni bora mngejikita kuhoji ni kwa nini Mbowe aliuza chama chenu???

Naamini bila mbowe kuuza chama msingekengeuka kiasi hiki.

Leo mnapinga kila kitu na kujidai mnadai democrasia wakati ndani ya chadema hamna hata tone la democrasia.
Kwani hapa anaongelea chadema? Wanaoisoma namba ni chadema tu?
 
Chadema ni bora mngejikita kuhoji ni kwa nini Mbowe aliuza chama chenu???

Naamini bila mbowe kuuza chama msingekengeuka kiasi hiki.

Leo mnapinga kila kitu na kujidai mnadai democrasia wakati ndani ya chadema hamna hata tone la democrasia.
Mbowe kaingiaje hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom