Unafurahi Magufuli kubana, jioni unaniomba nikutoe hela

Niliwaambia Madhara ya kubana sana itamuathiri mpaka aliyezaliwa jana, wakabisha.. Ooh, bora tuishi wote maisha ya usawa, Mimi najua hakuna usawa, Macho ya Binadamu hayafanani, viganja vya mikono havifanani, kuna mambo tunalazimisha lakini hayawezi kuwa vile. Sasa wale waliowasema wenzao wataisoma namba, wao wamekuwa wa kwanza kuandika namba, Mambo ya Uchumi hubeba jamii nzima. Yaani jirani yangu akiwa na njaa, automatically hata mimi nina njaa, Tuvumilie
 
Tutauza mpaka mashuka mwaka huu,jamaa yangu kamaliza magari yake yoote kabakiza brevis ,familia inayumba ndani hapakaliki
 
Potelea mbali, Ngoja hali iwe ngumu tu. tulikokuwa tunaelekea palikuwa panatisha kuna watu vyakula vilikuwa vinaoza wengine hawana. Je, Serikali hailipi mshahara, Nchi haiwezi kuendelea kwa kuwekeza kwenye warsha na semina elekezi, Badala ya kusafiri wataalamu kwenye ziara za kujifunza namna ya kukuza miji na kilimo cha kisasa na mambo ya technologia eti tulikuwa tunawapeleka wabunge wengine wameishia darasa la 7, wengine wamesoma lakini sio taaluma zinazowahusu kwenye taaluma husika. Hivi nyie hamkuwahi kusikitika kusikia Serikali inapewa mikopo na wafanyabiashara wa ndani tena sio kwajili ya maendeleo, ni kwaajili ya mishahara ya watumishi wake. Ngoja tu tulie wote, lakini kilio chetu hakitaenda bure
Hapa 2natengeneza equality of economy xababu gap lilkua kubwa sana.
 
Sio kila matu hali ni mbaya kama tunavyoeneza uvumi huo.
Kama ulikuwa huna nidham ya pesa huna tu,na wale wenye nidham ya pesa wanajua nini wanafanya.

We unalalamika ila watu bado maisha yanaendelea nawanapambana na kupiga pesa tu.
Nidham ya matumizi ndio inatakiwa,pesa inapokuja kirahisi na nidham yake inakuwa mbaaya kwa weng,Pombe na Madem,kuhonga kwenda mbele,matumizi kibaoo yasiyo ya lazima.
We jiulize rafiki yako anaelalamika alikuwa anatumia vipi kipato chake,na alikuwa amewekeza kwenye biashara gani hataka kama ni genge la Nyanya.
 
watu wanasema tumepigika wote huku kuna mtu kaalika watu futari juzi na kuwagawia na I phone wageni wake wote...

hapo ndio amefilisika eti
 
Huyu mtani wangu ni mtumishi wa umma,lakini ni ukawa damudamu,na tangu posho na safari za kikazi zipungue huko kwa mwanamehesabu mkuu,yaani amekosa amani kabisa..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom