Unafungia harusi Mjini badala la Kijijini ulikotoka eti kisa washikaji

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Vijana wa leo 'brothen men' sana

Kila kijana anayefunga ndoa eti anafungia mjini anakoishi, anakofanyia kazi. Badala ya kurudi kijijini ulikozaliwa, ulikokulia ama ulikotoka na ndio kwenye baraka za wazazi, ndugu na jamaa wa ukweli ulikolelewa kuliko 'masnitch' wa huko mjini uliowakuta ukubwani.

Wazazi, ndugu na jamaa wanapata shida kusafiri kutoka huko kijijini Uvinza kuifuata sherehe yako huko Daslam, kisa eti hutaki kuwalet down washikaji na jamaa wengine 'wakuja' tu kwenye maisha yako.

Kijijini mzazi /ndugu/rafiki ajichange nauli, ashone sare, ajikusanye kizawadi na aandae hela ya kuja kulala Daslam kuhudhuria sherehe yako. Kisa tu masela wako eti.

Kijijini hela ni ngumu mno, kilimo hakina tija, wazee wamedunduliza wee kukusomesha mpaka umefikia hapo, leo hii tena unataka wajichange watoke huko kijijini wakufuate wewe mjini. Ni ujinga sana huu.

Kwanini usifunge harusi kijijini ? Hata watu back ( masela) wakiikosa siyo tatizo, kwanza ni baraka sana.

Inaumiza sana vijana wa leo unasababisha wazazi , ndugu wanajichanga huko kijijini kwa ajili ya kuja kuattend harusi yako mjini.

Nidhambi sana ndio maana ndoa hazidumu.
 
Mi nimeshaapa nitafanya Simple marriage ceremony ambayo itahudhuriwa ya watu 15 tu.

Siku hio naamka tunajiandaa tunafunga ndoa yetu kanisani... hapo tukiwa ndani ya mavazi nadhifu na ya kipekee sanaaa

Baada ya hapo natafuta hotel iliyo sehemu nzuri maeneo ya bagamoyo au zanzibar tunapunzika, jioni kutakuwa na katafrija kafupi mnoo ambayo itahudhuriwa na wazazi wa pande mbili, ndugu wa damu wa pande mbili na marafiki wachache wa pande mbili.. total haitozidi watu 15... yaani piga ua, afe nyani afe kenge...

Tunatafuta kijihotel kilichojitenga ambacho katakuwa maeneo ya pwani kenye nafasi ya wazi tunafanya tafrija yetu fupi ambayo haitozidi masaa 2...

Baada ya hapo kila mtu kwao

Note: Sitochangisha mtu yeyote
 
u

safi!!
 
Mimi niliachana kabisa na hii kasumba,washikaji zangu niliwaeleza kwa uwazi kabisa kuwa ndoa yangu itafungiwa kijijini kwetu atakayeweza kunichangia fine atakayeshindwa pia fine.

Changamoto kidogo ilikuwa kwa mke wangu ambaye kwa asili amezaliwa na kukulia mjini,nilipomueleza kuhusu mpango wangu huu alipatwa na mshituko mkubwa, lakini baada ya kumueleza kwa makini sana undani wa ndoa yetu kufungiwa kijiji alinielewa vizuri na baadaye alinishukuru sana kwa maamuzi yangu kwa namna sherehe alivyokuwa nzuri sana na hasa umati mkubwa wa wanakijiji wezangu waliohudhuria na kwa hakika ndoa yetu imekuwa ya baraka sana.
 
Vijana wa leo 'brothen men' sana

Kila kijana anayefunga ndoa eti anafungia mjini anakoishi, anakofanyia kazi. Badala ya kurudi kijijini ulikozaliwa, ulikokulia ama ulikotoka na ndio kwenye baraka za wazazi, ndugu na jamaa wa ukweli ulikolelewa kuliko 'masnitch' wa huko mjini uliowakuta ukubwani.
Kosa lako ni kuassume kila mtu katokea kijijini, wakati kuna 'watoto wa kariakoo, toka babu zao!.'
 
Back
Top Bottom