tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,490
Katika hotuba yake pale Bungeni wakati wa uzinduzi wa Bunge Rais Magufuli alitoa hotuba moja kali sana yenye msimamo kikazi na kutoa muelekeo wa Serikali atakayoiongoza akionyesha kuchukizwa kabisa na ufisadi na mambo mengine ya ovyo yaliyokuwa yanafanyika ndani ya Serikali zilizopita.
Moja ya mambo ambayo alionekana kuchukizwa nayo ni ufisadi ndani ya Serikali na kusababisha wananchi kutopata huduma inavyostahiki huku pesa nyingi zikipotea mikononi mwa watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali.
Ndio alipoibuka na mambo mengi sana ambayo tumeyashudia yakifanyika na kutolewa maamuzi kwanza kabisa ni kushughulika na viongozi wabadhirifu ndani ya Serikali na taasisi zake
Wafanyakazi hewa,Wanafunzi hewa,Vyeti fake,makotena yasiyolipiwa kodi,wizi wa mafuta bandarini,wizi ndani ya migodi ya madini mbalimbali, nk
Kwa kuanza na kushughulika na uhalifu ndani mifumo ya Serikali lazima kuna mambo mengi ambayo alikuwa anajua kuhusu mifumo mibovu iliyokuwepo ambayo ilikuwa inakwamisha mambo
Na mpaka sasa bado anapambano na mifumo ya kiuhalifu ndani ya Serikali.