Unafikili nani alikubalika zaidi jimboni kwake kati ya Dr. Slaa na Lowassa?

cantonna

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,120
439
Wadau kama tujuavyo lowasa kabla ya kugombea Uraisi alikuwa mbunge wa Monduli kupitia CCM,na aliamua kuachia jimbo pale alipoamua kugombea Uraisi na kwa upande wa Dr. SLaa naye alishawahi kuwa mbunge wa jimbo la Karatu kupitia CDM na aliamua kuachia jimbo pale naye alipoamua kugombea urais mwaka 2010.

Hawa wote ni moja ya viongozi ambao walikuwa wanapendwa sana majimboni mwao..........lakini ni ukweli usiopingika sasa hivi hawa jamaa wawili ambao kwa kawaida huwa hawawezi kukaa kwenye zizi moja upepo wa kisiasa na nguvu zao za kisiasa zimeweza kutikisa vyama walivyoviacha, Lowasa kaikacha CCM na kuhamia CDM na Slaa kaikacha CDM na kaamua kustaafu siasa ya vyama kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe japo kiuhalisia anaonekana kana kwamba kaamua kurudi CCM ila anaona aibu kusema!!SASA NAJIULIZA KATI YA HAWA WATU WAWILI NI NANI ANAKUBALIKA ZAIDI KATIKA JIMBO ALILOWAHI KUONGOZA?

Maana nakumbuka mara tu Lowasa alivyotangaza kuhamia CDM viongozi wote wa CCM wilaya ya Monduli pamoja na madiwani wa wilaya ya Monduli kupitia CCM nao walihama kumfuata mtu wao ambaye wanaamini atawaletea #MABADILIKO kwa kujiunga pia na CDM.....Lakini hali ni tofauti kwa Dr.Slaa ambaye aliamua kujiudhuru na kutamka wazi kuwa watanzania wote wasiichague CDM kutokana na madhambi ya Lowasa lakini naona hata watu wake jimboni wamempuuza kwani sijaona hata kiongozi mmoja wa CDM kutoka Karatu aliyejiuzuru kumfuata Dr.Slaa wala mwenyekiti wa kijiji wa diwani....

Kama ameshindwa kuwashawishi watu wake wa Karatu wasiichague CDM anaweza kwa si wengine ambao hatuko jimboni kwake?Kifupi kwa upepo huu Dr.Slaa hakukubalika jimboni kwake ndo maana wanampuuza!!!Lowasa ndo tumaini la watanzania!!!
 

Attachments

  • ukaw.jpg
    ukaw.jpg
    39 KB · Views: 293
Hakuna mahali aliposema wasiichague CDM..we muongo..kisha upeo wa watu wa silaa na lowasa ni tofauti..watu wa silaa sio wa mihemko..ila utaona kwenye kura matokeo ya karatu..
 
usicheze na nguvu ya hela wewe. wengi wataenda na maji tutabaki wachache tu ambao ni sugu.

Wadau kama tujuavyo lowasa kabla ya kugombea Uraisi alikuwa mbunge wa Monduli kupitia CCM,na aliamua kuachia jimbo pale alipoamua kugombea Uraisi na kwa upande wa Dr. SLaa naye alishawahi kuwa mbunge wa jimbo la Karatu kupitia CDM na aliamua kuachia jimbo pale naye alipoamua kugombea urais mwaka 2010.Hawa wote ni moja ya viongozi ambao walikuwa wanapendwa sana majimboni mwao..........lakini ni ukweli usiopingika sasa hivi hawa jamaa wawili ambao kwa kawaida huwa hawawezi kukaa kwenye zizi moja upepo wa kisiasa na nguvu zao za kisiasa zimeweza kutikisa vyama walivyoviacha, Lowasa kaikacha CCM na kuhamia CDM na Slaa kaikacha CDM na kaamua kustaafu siasa ya vyama kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe japo kiuhalisia anaonekana kana kwamba kaamua kurudi CCM ila anaona aibu kusema!!SASA NAJIULIZA KATI YA HAWA WATU WAWILI NI NANI ANAKUBALIKA ZAIDI KATIKA JIMBO ALILOWAHI KUONGOZA?Maana nakumbuka mara tu Lowasa alivyotangaza kuhamia CDM viongozi wote wa CCM wilaya ya Monduli pamoja na madiwani wa wilaya ya Monduli kupitia CCM nao walihama kumfuata mtu wao ambaye wanaamini atawaletea #MABADILIKO kwa kujiunga pia na CDM.....Lakini hali ni tofauti kwa Dr.Slaa ambaye aliamua kujiudhuru na kutamka wazi kuwa watanzania wote wasiichague CDM kutokana na madhambi ya Lowasa lakini naona hata watu wake jimboni wamempuuza kwani sijaona hata kiongozi mmoja wa CDM kutoka Karatu aliyejiuzuru kumfuata Dr.Slaa wala mwenyekiti wa kijiji wa diwani....kama ameshindwa kuwashawishi watu wake wa Karatu wasiichague CDM anaweza kwa si wengine ambao hatuko jimboni kwake?Kifupi kwa upepo huu Dr.Slaa hakukubalika jimboni kwake ndo maana wanampuuza!!!Lowasa ndo tumaini la watanzania!!!
 
Dr anakubalika, alikuwa anapokelewa mpakani(mto wa mbu) na wananchi wakiwa na baiskel, mapikipiki na magari siku anaenda jimboni kwake
 
Back
Top Bottom