Unafiki wa wanasiasa na siasa za Tanzania

MWONA MBALI

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
460
610
Ni hapa tu tanzania utaona mpinzani anaongea hili leo kesho anaongea lingine. Safari ya vyama vya siasa bado ni kubwa, hata wale wenye maono ya kubadili mfumo wa siasa tulio nao wanamezwa na ushabiki na kuutafuta umaarufu. Upinzani wa tanzania bado hauna dira, hawana ajenda kwa wananchi.

Kwenye chama kimoja kuna vyama vingi humohumo ndani, sawa tu na ccm nyingi ndani ya ccm moja. Tukubali tu kuwa watanzania tu waoga na wapenda sifa, vyama vyetu vina wanafiki wengi kwa kujali maslahi binafsi.

Mifano ya unafiki wa wanasiasa wa tanzania ni kama ifuatavyo:

1. Kesi ya kikatiba kupinga kufutwa mikutano ya hadhara
2. Operation ukuta
3. Lowassa ni fisadi
4. Nchi imeoza inahitaji kiongozi mkali ainyooshe:

Utashangaa leo wanasiasa waliotamka hayo wapo kinyume chake.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hao unaowaabudu miaka 55 wameachieve nini zaidi ya kuifilisi nchi.
 
Mbona hueleweki kama unaongelea vyama, upinzani au Watanzania!? Kwa hiyo unavyosema upinzani hauna dira je chama tawala kina dira!? Kama unaona kina dira mbona kila awamu inayokuja inabadilisha mfumo wa elimu!? Mbona kila awamu inaiponda iliyoitangulia? Na kikubwa kabisa mbona umasikini na ujinga unazidi!?
 
HEADING INASEMA UNAFIKI WA WANASIASA NA SIASA ZA TANZANIA, MIFANO NILIYOISEMA NI MICHACHE TU. KWANI WALIOKUWA NANASEMA LOWASSA NI FISADI NI WAKINA NANI? NA WAKINA NANI WALIKUWA WANAMTETEA wakati huo? JE LEO WAKINA NANI WANASEMA LOWASSA NI FISADI NA WAKINA NANI WANAMTETEA? HUONI KUWA MAKUNDI YANABADALISHANA MITAZAMO KIMASLAHI? huo ndio unafiki wenyewe.
 
Hivi mfano wanavyosema Daudi ndiye fulani na anamiliki vyeti fake akitokea hadharani na kuonyesha vyeti halisi ni nani atakuwa na mashaka tena!?
Hoja ya kutuhumiwa ufisadi kama mhusika alitokea hadharani na akasema mwenye ushahidi aulete na hadi leo hakuna, si tunasahau na kuendelea!? Kumbuka sisi ni binadamu na sio kama mawe ambalo ukiliacha sehemu hata miaka mia unaweza kulikuta. Kama ufisadi mkubwa aliotuhumiwa nao ulikuwa Richmond na hadi leo tangia ajiuzulu pesa zinaendelea kupigwa kwa jina hilo hilo na mtuhumiwa wala hashitakiwi si tunakubaliana na kwenda mbele!
 
Mwona Mbali unaungwa sana mkono ila nasi tuongeze kusema kwamba kuanguka kwa taifa huanza na hao wanafiki, si watu wema, ni wa kuogopwa kama ukoma!! Muhimu sana wasipewe uongozi wa nchi.
Tanzania yetu, kipenzi chetu, daima dumu iwekwe kwenye mikono salama kwa sababu wananchi tunataka amani na usalama kwanza lakini wanafiki, tena wengine eti wasomi, hawapendi! Lakini pia eti wanataka uongozi wa nchi. Ajabu!
[HASHTAG]#UsirudieKosa2020kupigiaKuraUpinzaniOvyo[/HASHTAG]!
[HASHTAG]#MtotoWaTANUnaASPniCCM[/HASHTAG].
[HASHTAG]#MzaziWakoNani[/HASHTAG]?
 
Back
Top Bottom