Unafiki wa Wabunge: Matatizo ya Watanzania ndio Mtaji! Shame! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa Wabunge: Matatizo ya Watanzania ndio Mtaji! Shame!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 8, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Wabunge ni wanafiki sana. Sana!

  Matatizo ya wananchi ndio mtaji wao. Mwisho wa siku nia na madhumuni ni vyama vyao viendelee kuongoza. Hakuna wenye nia ya kuwasaidia wananchi kwa sababu wananchi wana matatizo bali kwa sababu wanataka kushinda.

  Kinachoendelea bungeni ni uthibitisho na kielelezo cha unafiki huu wa wabunge! Maslahi ya chama ndiyo yako mbele. UCCM na UCDM na UCUF na UTLP na UUDP ndio wanachojali.

  Mwananchi wa kawaida hawahusu. Wao sio wananchi wa kawaida. Hakuna mbunge ambaye mtoto wake anasoma shule ya kata, hakuna mbunge ambaye mtoto wake anakosa dawa zahanati, hakuna mbunge ambaye familia yake inalala njaa, hakuna mbunge ambaye nyumba yake haina umeme!!

  Narudia, ni wanafiki sana! Posho wanayoipata hakuna wanachofanya. Jiulize kwa umakini, kazi ya Mbunge ni nini? Mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kijiji na Mtendaji Kata ndio wanaofanya kazi lakini hawapewi hela ya mafuta, hawana posho ya vikao, hawana semina wala nini! Wao ndio watekelezaji wa shughuli za maendeleo. Inasikitisha na kukera kuona wabunge wanajidai wao ndio watetezi wa wananchi! Wanatetea nini? Miaka yote wabunge wapo, nchi imeliwa, wanafunzi wanafeli, umasikini unazidi, ujambazi, maradhi, miundombinu mibovu nk!

  Fedha zinazotumika kuwahudumia wabunge zingetosha kuleta mapinduzi makubwa ya elimu! Ukombozi wa kweli wa mtanzania!

  Wanachotufanyia sasa hivi ni usanii nakutuona sisi mazuzu! Ila ipo siku! Viwiliwili vyao na shingo zao!! Ishara ya kuchoshwa!
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  And this is why Africa will not develop with this trend!
   
Loading...