Unafiki wa wabunge huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa wabunge huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jul 30, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Baada ya kuona walimu kukomaa na kuanza mgomo nimeona wabunge wa CCM na upinzani wakisimama kujifanya wanataka kujadili mgomo wa walimu. Kwani kabla ya hapo hawakujua kama walimu wana matatizo hadi tulipoamua kugoma ndo wanajifanya wana uchungu "that is hypocricy"

  Unafiki zaidi ni pale wanapokubaliana kuchukua mshahara wa sh. 10000000 na posho nyingine kibao wakikopeshwa magari na kulipiwa mafuta katika nchi ambayo viongozi wanahubiri umaskini huku walimu tukiachwa katika hali ngumu ya maisha. Wabunge na serikali wajue kwa ubinafsi walionao waamini kuwa wanajikaribishia laana. Maana hawawezi kufanya dhambi kubwa namna hiyo halafu wakategemea baraka. WABUNGE NA SERIKALI MUOGOPENI MUNGU.

  kila baada ya miaka mitano wanapata kiinua mgongo cha 45000000, wakati mwalimu aliyefanyakazi kwa zaidi ya miaka 30 hupata 40000000 halafu leo wanajifanya wana uchungu na mgomo wa walimu. KWELI HUU NI UNAFIKI MKUBWA!
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,028
  Likes Received: 37,791
  Trophy Points: 280
  Ni wanafiki wakubwa kila bajeti wanapitisha.Wangekuwa na uchungu wangepitisha kima cha chini cha sh 170,000/=?
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  hivi bado mnaamini wabunge wana uchungu na nchi hii? kama ni kweli mbona wao ndio wachakavhuaji wazuri wa fedha serikalini mfano za tanesco ilihali ndio watoka povu wakubwa bungeni?

  binafsi nmchukia mbunge na waziri na natamani niamke kesho pale dodoma pawe pametitia kabisa kusiwepo na mbunge wala waziri atakayepona kwenye hiyo dhahama
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,028
  Likes Received: 37,791
  Trophy Points: 280
  Cha ajabu yamekariri kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja alafu yakisikia watu wanagoma yanakuja na unafiki wa muongozo na jambo la dharura.Hili bunge ni janga la kitaifa na linastahili kuvunjwa.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  UNAJUA mwl sisi tupo wengi sana takriban 185000 kati y watanzania wote so hao watu sijui 350 hawatutish kamwe kama wanataka kujaribu waje waone cha moto. Na ukweli ipo siku mbune atapigwa na wanachi wake wallah tena.
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wabunge wetu ni Mafisadi na wamekosa Uzalendo na ni wasaliti wakubwa, Nimepoteza imani na wabunge wetu
   
 7. n

  ngoshas JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanasiasa hawajawahi kukomboa nchi maskini, km we ni mwalimu utakumbuka kuwa tafsiri ya neno siasa ni U O N G O uliokomaa
   
 8. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  bunge ni COMEDY SHOW............. ts high time ifahamike ............ no 1 z thre 4 u
   
 9. c

  cyberspace JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 660
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mimi nawaheshimu wenyeji wa mikoa mitatu tu Kilimanjaro, Arusha na Kigoma hivi mlipochagua Magamba hamkujua kweli majuto ni mjukuu
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Kamwe hawawezi kuikwepa laana kuu ya kuwanyonya wanyonge
   
 11. n

  ngwenda ngulya Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  neno hilo wabunge wetu wamejisahau kabisa. Mungu tusaidie
   
 12. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Naungana na wewe. Hao ni wanafiki waliokubuhu. Wana-enjoy life wakati walimu wanahangaika. Walimu komaeni muifundishe adabu serikali.
   
 13. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  watajitia kuunda tume kama wakati wa mgomo wa serikali watajilipa maposho na baadae taarifa itafichwa kwa kifupi wanaosababaisha hii migomo ni wabunge kwani wakati serikali inashindwa kuongeza pesa sehemu nyingine wao wanazidi kujiongezea ndio maana watu wana hasira nao.hebu tujiulize ni sehemu gani wanapofundisha watu ili wawe wabunge na mbunge gani sasa hivi mtotot wake anasoma shule za kanumba tumeshashtukia unafiki wao
   
 14. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Pamoja na mafao yote hayo wanayokomba ndani ya kipindi cha muda mfupi bado yanapitisha sheria inayotaka sisi tupewe mafao baada ya kufa! Silly people indeed!
   
 15. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Hapa magamba wala kombati kinachozungumzwa hapa wabunge takribani wote ni wanafiki kwani hawana kimoja wanachokifanya zaidi ya kufikiria posho na kuibua hoja za kujipatia umaarufu kweli siasa ni mchezo mchafu
   
 16. D

  Determine JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wabunge wote 35 waliochangia kwa kuzungumza wamejikuta wakichangia yaleyale ambayo madaktari tumekuwa tunadai ambayo ni;upungufu wa vifaa tiba km xrays,ST-scan,MRI,upungufu wa dawa na ukosefu wa vitanda vya kutosha n.k.Haya ndiyo madai ambayo tumedai huku wao wakiwa wanaitetea serikali na wengine kufikia hatua ya kuomba tunyongwe(mf manyanya na maji marefu). kama wasingekuwa wanafiki wasingepitisha hiyo budget ya afya mpaka serikali iwarudishie lessen zao madaktari wapatao 318,maana hawa ndo wamefutiwa leseni zao kwa kusema yaleyale ambayo wabunge wameshinda kwa siku mbili wanayasema
   
 17. j

  jembe mwanaharakati Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umaarufu kisiasa unatafutwa kwa njia nyingi hata hii ni mojawapo kwa wabunge kuwanafikia wananchi
   
 18. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Niliwasikia wabunge wakiomba kuahirisha shughuli za bunge ili wajadili suala la mgomo wa walimu. Kama haitoshi wakataka pia wajadili swala la mabadiliko ya sheria ya mafao wakati ni hao hao waliopitisha loo!

  Maswali yangu;

  Kabla ya hapo hawakujua kuwa walimu wanalipwa mshahara mdogo na matatizo mengi? mbona wao wanalipana pesa nyingi sana?

  Walimu tumeamua kugoma ili kujitetea hivi kwanini wanalipwa kiasi kikubwa cha fedha wakati hawajui hata matatizo ya watanzania wakiwemo walimu

  wabunge wameingiza ufisadi Tanesco, wanaogopana hata kutajana.

  HILI BUNGE HALINA VIWANGO NA LIMEPOTEZA MVUTO KABISA KAMA RAIS ALIVYOPOTEZA MVUTO KWA WATANZANIA.

  RAIS ACHA UBABE WALIMU TUKO TAYARI HATA KUFUKUZWA KAZI KULIKO KUENDELEA KUONEWA NA KUWAONA WALE TULIOWAPA ELIMU WAKIENDELEA KUTUDHARAU AKIWEMO RAIS,MAWAZIRI NA WABUNGE.

  HATUKO TAYARI KUNYONYWA NA WCHACHE KATIKA NCHI YETU HURU.

  POLOLISI ACHENI KUTUTISHIA FUATENI SHERIA, HUU MGOMO UMEFUATA SHERIA, MTAJIPENDEKEZA HATA LINI HUKU BAADHI YENU MKIISHI KWENYE MABANDA NA MABATA YENU.

  NI BORA HALI YA MWALIMU KULIKO NYIE LEO MNAJIFANYA KIHELEHELE ETI KUWAKAMATA WALIMU KOMENI. NENDENI KULISHA BATA. MTAKUWA VIKARAGOSI VYA CCM MPAKA LINI? BADILIKENI DUNIA HUBADILIKA
   
Loading...