Unafiki wa viongozi kwenye misiba ya wanaharakati huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa viongozi kwenye misiba ya wanaharakati huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwinukai, Jul 10, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ITAKUMBUKWA kuwa alipofariki marehemu Sylvester Rwegasira Viongozi wa Nchi walitoa ushirikiano mzuri sana, mpaka watu wakawaona viongozi hawa kuwa na utu na heshima kwa raia wanaowaongoza. Ushirikiano wa kwanza ulitilewa na Waziri Kabaka aliyevua uwaziri wake na kulala pale msibani, licha ya hivyo Raisi aliweza kushiriki katika hatua zote hadi mazishi na aliweza kumwahidi mjane wa marehemu kuwa wapo pamoja na watamsaidia ili kupunguza majonzi ya kufiwa na mumewe.

  Cha ajabu na cha kushangaza mara baada ya msiba sisi majirani tukiwa mashaidi serikali inamzungusha hata kwa haki zake za msingi kisheria hajazipata anazungushwa zungushwa tuu. Mbaya zaidi kumekuwa na watu waojiita wanatoka serikalini wakiomba baadhi ya nyaraka ambazo wanaamini marehemu anazo.Hivi huu ushirikiano wa viongozi waliouonyesha si unafiki au kejeli?

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  [TABLE="width: 1235"]
  [TR]
  [TD]
  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
  [h=4]Fax: 255-22-2113425[/h]
  [/TD]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [TD]
  PRESIDENTÂ’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
  [h=5][/h][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Omar Nundu kufuatia kifo cha ghafla cha Sylvester Rwegasira, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kilichotokea tarehe 4 Aprili, 2011 kutokana na maradhi ya moyo.

  Rais Kikwete amesema kuwa kifo cha Sylvester Rwegasira kimeleta simanzi kubwa siyo kwa familia yake tu, bali pia jumuiya ya wafanyakazi hapa nchini kwani Marehemu Sylvester alikuwa mtetezi mkubwa wa wafanyakazi hususan wale wa Reli ambao yeye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama chao, kwani alijitoa kwa moyo wake wote kutetea maslahi yao.

  Kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi, Rais Kikwete ametoa pole nyingi kwa familia ya Marehemu Sylvester Rwegasira kwa kupotelewa na kiongozi muhimu wa familia, hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Rwegasira.

  Wakati huo huo, Rais Kikwete amewaomba wanafamilia ya Marehemu Rwegasira kuwa watulivu, wavumilivu na wenye subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao, huku akiwahakikishia kuwa yeye binafsi yuko pamoja nao katika muda wote wa maombolezo ya Marehemu Sylvester Rwegasira.

  Mwisho.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  05 Aprili, 2011
   
Loading...