Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Jana nilibahatika kusikiza kwa kiasi fulani taarifa ya habari ya saa bili usiku kupitia TBC1. Nilianza na taarifa iliyokuwa ikimgusa Prof. Lipumba. Ilianza kwa mtangazaji wa TBC1 kujikanyaga-kanyaga na baadae akapisha clip ya Lipumba isikike. Wakati Prof. Lipumba akiongea mambo mepesi-mepesi, mawimbi yalikuwa yakisikika vizuri tu. Alipoanza kuponda uozo wa CCM na serikali yake, mara signal ikawa inakatika katika na akawa hasikiki tena, na hamu niliyokuwa nayo ya kusikia ikanitoka kabisa.
Akaja Rais mteule. Dr. Wilbroad Slaa. Hapo TBC1 wakaendelea na propaganda. Safari hii Dr. Slaa alikuwa akisikika, lakini kamera yao ilikuwa ikimulika utitiri wa watoto waliokuwa kwenye kampeni (ili kuihadaa jamii kuwa mikutano ya Dr. Slaa huwa inajaa watoto ambao hata hawana sifa ya kupiga kura). Wizi mtupu!!
TBC acheni unafiki.