Unafiki wa TBC kwa jitihada za CHADEMA katika ujenzi wa Tanzania

TBC ilipokuwa chini ya TM ilijipambanua kama chombo halisi cha umma kilichokuwa na wajibu wa kuulisha umma habari za ukweli na uhakika, rejea mchakato majimboni, na kualikwa kwa wanaharakati katika vipindi vya moja kwa moja, hali kwa sasa ni tofauti kabisa, si upande wa habari za siasa pekee, tazama habari za michezo sielewi kimewakumba nn hadi Pendaeli na wenzake sitaki kusema kuwa morale imeshuka. Angalia usomaji wa magazeti chini ya kilaza Joe, sasa ukitizama hutaamini kuwa hii ni authoritative public media.
Cha msingi hapa ni kwa wabunge wetu kuhoji utenda kazi wa chombo hiki, umma unapaswa kupewa habari sahihi na si kufichwa habari na matukio yanayougusa umma
 
acha na hao majuha,tuijenge CHADEMA kwa hali na mali pia tutazishinda hila zao
 
Mbona tulishaacha kuhangaika na tv za bongo mkuu? Mtu mwenyewe Mshana unategemea afanye nini badala ya kuendeleza ile kazi ya sisiemu na zidumu fikra ya mwenyekiti wa ccm? usiwe na shaka iko siku tutakuwa na tv zenye kuwa na usawa!

Ha ha ha haaaaaa, waliona hiyo habari haina umuhimu bana ndio maana hawakuirusha . Kwani habari nyingi za cdm zimejaa majungu na unafiki bana
 
TBC ilipokuwa chini ya TM ilijipambanua kama chombo halisi cha umma kilichokuwa na wajibu wa kuulisha umma habari za ukweli na uhakika, rejea mchakato majimboni, na kualikwa kwa wanaharakati katika vipindi vya moja kwa moja, hali kwa sasa ni tofauti kabisa, si upande wa habari za siasa pekee, tazama habari za michezo sielewi kimewakumba nn hadi Pendaeli na wenzake sitaki kusema kuwa morale imeshuka. Angalia usomaji wa magazeti chini ya kilaza Joe, sasa ukitizama hutaamini kuwa hii ni authoritative public media.
Cha msingi hapa ni kwa wabunge wetu kuhoji utenda kazi wa chombo hiki, umma unapaswa kupewa habari sahihi na si kufichwa habari na matukio yanayougusa umma

Ha ha ahaaa, hamkuwaalika bana wangewezaje kuwarusha bana ! nasikia nyie mnaalika ile radio yetu ya ukatoliki bana
 
Ha ha ahaaa, hamkuwaalika bana wangewezaje kuwarusha bana ! nasikia nyie mnaalika ile radio yetu ya ukatoliki bana
Umenichekesha sana GB, wakiwa wanaalikwa kupata habari itakuwa ni ukasuku, ni kazi yao kutafuta habari kw gharama zao na ndiyo ikazi zao kusaka habari mkuu.
Hivi unadhani habari za ccm kutangazwa na radio quran, heri kunaifanya ccm kuwa chama cha waislam task your head, nilishatangaza maslahi mapema sana katika moja ya thread humu, mm ni mwanachama hai wa ccm na tunapoongelea kuhabarishwa kwa umma hatumaanishi habari za ccm, tunataka umma tulishwe na habri nyingine ili tuweze kuwa na uwezo wa kuhoji, kuwa mwanachama wa ccm sio kukosa uwezo wa kuhoji mambo ya msingi, Wana ccm sio makondoo ama maiti:phone:
 
Hii radio yetu sisi watz wote lakini sijui kwanini wanafanya upuuzi namna hii, na uyu mkurugenzi mpya ndio CCM kabisa, dawa yao inachemka.
 
Hawa watu wamesahau dhamana waliyopewa na wananchi. Wanasahau kilichotokea Misri miezi kadhaa iliyopita pale wananchi walipoandamana kwenda kwenye stesheni ya redio na televisheni ambapo vituo hivi vilitumika kama mashine za propaganda vya H. Mubarak. Watangazaji walipoona nguvu ya umma inashinda, wali-come out na kuomba samahani na kuweka siri zote nje jinsi walivyokuwa wakiendesha hivyo vituo.

Mubarak is in detention, siku watanzania wakikosa uvumilivu nao wanaweza kufanya kilekile kilichofanyika Misri. Kwa misingi hiyo, viongozi waliopewa dhamana wanatakiwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa katiba na si ushabiki wa vyama au bendera. Iko siku mtawajibishwa na wenye nchi.
 
Ha ha ahaaa, hamkuwaalika bana wangewezaje kuwarusha bana ! nasikia nyie mnaalika ile radio yetu ya ukatoliki bana

Nikweli miaka hamsini ya uhuru bado tuna watu wenye mawazo finyu kama haya?
kwanini kama huna cha kuchangia usiufiche ujinga wako moyoni mwako?
ninani anayetoa hukumu ya habari ya muhimu kama si mtazamaji pia?

Mtu mjinga kunapokuwa na hoja ya msingi hukimbilia kwenye dhana mfu
isiyosadifu logic,mfano udini,ukanda,na ukabila.

Tunacho hoji hapa kwa mapenzi mema,nichombo cha umma kuegemea zaidi
kutoa habari za chama tawala.Naungana na mchangiaji aliyesema tuwatumie wabunge
wetu kuhoji bungeni kuhusu tendaji wa tbc.

Lakini pia kwa mshikamano ule ule tuliouonesha kupinga malipo ya dowans
tunaweza pia tukadai utendaji wa uwiano kwa tbc.

Tanzania ni yetu sote,hatutaki kuachiwa makovu ya ubaguzi yanayoletwa na ccm
na kulelewa na tbc.
 
Huku arusha hotuba zote za dr, slaa zinazorushwa na itv hazina sauti kabisa hata jana taarifa ya habari sa mbili usiku ilikuwa haina sauti kabisa tbc hawakuonyesha pia star
hata wakiacha, tutasoma magezeti. Cdm wawe wanatembea na watu wa channel 10, itv na star tv. Hiyo waachane nayo. Wengine watasikiliza kipindi cha magazeti rfa na watapata ujumbe tu.
 
Wanajamvi kwa mara nyingine naleta maoni yangu hapa jamvini kuhusu shirika letu la
utangazaji TBC.

Mengi yamezungumzwa na tutaendelea kuyakemea mpaka kieleweke.
Baada ya kuzungumza sana na kuonesha kukerwa sana,leo tbc wamejitutumua
kuonesha mkutano wa CHADEMA ikiwa imechakachuliwa sana,na kilichonishangaza
mimi ni kuchagua na kurusha sehemu ambazo hazikuwa na mguso kwa jamii

Na chakushangaza zaidi hotuba ya Dr Slaa kuhusu upotevu wa bil 200 ilikatwa na hauoneshwa kabisa.
Wakati huo huo katika muhtasari wa habari,uchaguzi wa mwenyekiti wa uvccm uliwekwa katika habari zilizopewa uzito.

Wadau nauliza tena ninini kilicho nyuma ya tbc?
SAHIHISHO, "shirika letu la utangazaji la tbc" sentensi hiyo isomeke hivi: shirika la utangazaji la ccm. (cbc)
 
TBC ilipokuwa chini ya TM ilijipambanua kama chombo halisi cha umma kilichokuwa na wajibu wa kuulisha umma habari za ukweli na uhakika, rejea mchakato majimboni, na kualikwa kwa wanaharakati katika vipindi vya moja kwa moja, hali kwa sasa ni tofauti kabisa, si upande wa habari za siasa pekee, tazama habari za michezo sielewi kimewakumba nn hadi Pendaeli na wenzake sitaki kusema kuwa morale imeshuka. Angalia usomaji wa magazeti chini ya kilaza Joe, sasa ukitizama hutaamini kuwa hii ni authoritative public media.
Cha msingi hapa ni kwa wabunge wetu kuhoji utenda kazi wa chombo hiki, umma unapaswa kupewa habari sahihi na si kufichwa habari na matukio yanayougusa umma

Bahati mbaya sio mtoto wa mjomba:A S cry:
 
Ndio, wanafiki sana, si wazalendo, bado wanaishi enzi za USSR, yaani ni hovyo kabisa. Bahati mbaya na TV nyingine zinaiga TBC. Angalieni Aljazira, BBC, CNN NK. What is wrong with your thinking ability.:dance:
 
Back
Top Bottom