""unafiki Wa Sumatra Tumeuchoka''''

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,851
18,951
NDUGU WATANZANIA NAFIKIRI HIZI SROTI ZA HII SUMATRA KILA MTU AMECHOKA KUZISIKIA EMBU WASOME KIDOGO HAPO CHINI

SUMATRA kuwakomesha wanaopandisha nauli kiholela


Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, SUMATRA, imekanusha kupandisha nauli za daladala Jijini Dar es Salaam na kuonya kuwa dereva na kondakta watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Meneja Ufundi na Usalama wa mamlaka hiyo, Bw. Aron Kisaka, ameliambia Alasiri kuwa wao bado hawajapandisha nauli za daladala na kuwataka watakaotozwa zaidi kuwasilisha malalamiko yao Polisi ama katika ofisi za mamlaka hiyo.

Hivi karibuni, mamlaka hiyo iliitisha mkutano na wadau wa usafiri huo kujadili maombi ya kupandisha nauli yaliyotolewa na wamiliki.

``Bado hatujapandisha nauli, tukipandisha tutatangaza... ushirikiano wa abiria unahitajika katika kuwadhibiti wavunja sheria. Bila wao kutoa taarifa, ni vigumu kufahamu kuwa wanatozwa nauli zisizostahili,`` akasema.

Bw. Kisaka akawataka wanaotozwa nauli hizo kubwa kuhakikisha kuwa wanafikisha tiketi katika ofisi zao na kwamba, kama makondakta hawatoi tiketi zilizoandikwa nauli waliyotoza, basi wapige simu nao wao watatuma maofisa wao kuchunguza.

Akasema faini kwa daladala litakalopatikana na hatia ya kupandisha nauli kiholela ni kati ya shilingi 100,000 hadi shilingi 250,000.

Hata hivyo, akasema ushahidi ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa wanaofanya hivyo wanaadhibiwa na kuwataka abiria kutoa ushirikiano wa kutosha pindi wanapobaini kuwa sheria inakiukwa, ikiwa ni pamoja na kutozwa nauli isiyokuwa ya halali.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya daladala hutoza abiria kwa nauli za juu, hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Mwandishi amebaini kuwa sehemu mojawapo ambayo daladala huwatoza abiria nauli kubwa ni kutoka Kariakoo kwenda Ubungo na Mbezi kwa nyakati za jioni, ambapo mabasi mengine hutoza kati ya Sh. 700 na 1,000 Pia nauli za juu hutozwa katika ruti za Mwenge-Posta, Mwenge-Kariakoo na Mwenge - Mbagala.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa na madereva na makondakta za kutoza nauli isiyohalali ni kupanda kwa gharama za uendeshaji wa utoaji wa huduma hiyo.

Kwa upande wa bei ya mafuta ya dizeli ambapo hivi sasa lita moja inauzwa Shilingi 1,950 wakati petroli ni shilingi 1700.

Hivi karibuni Serikali imepitisha kanuni mpya za leseni za usafirishaji abiria ambapo wamiliki, madereva na makondakta wakorofi hushtakiwa kwa makosa ya jinai.

Pia mmliki wa leseni ya usafirishaji anayetaka kubadili nauli kwenye njia yoyote ni lazima atoe ilani na kupeleka maombi kwa mamlaka ya kubadili nauli kwa muda usiopungua siku 10 akielezea mazingira yanayosababisha ulazima wa kubadili nauli

HAYA NI MANYANYANGU NYANGU YA KILA SIKU HAKUNA LOLOTE ZAIDI YA KUKAMATA MADALALA NA KUOMBA HONGO KAMA MAASKARI!!!!
WAMEKUWA WAKIMPINDISHA SHERIA KILA SIKU!!!WAKATI WA SIKUKUU WATU WALIPANDISHA NAULI WAKATAFUTA WANAHABARI WAKAWAPIGE PICHA!!!!BAADA YA KUONEKANA KWENYE TV..WAKAKIMBIA PALE UBUNGO STAND MCHEZO UKARUDI TENA SIJUI KULIKUWA NA WAKWE ZAO WANASAFII SIKUHIYO!!!!!!OMBI LANGU EMBU WEWE DIRECTOR KUWA SERIOUS NA MAISHA YA WATU WACHA KUVIFIKIRIA VILE VIPANYA VYAKO,,,JAMANI UBUNGO----G'MBOTO NAULI USIKU 1000,,NA NIKAJARIBU KUMPIGIA MZEE MMOJA WA SUMATRA ANASEMA KIJANA ANADIKA NAMBA TUTAFWATILIA MPAKA KESHO!!!!NKAAMUA KUMWAMBIA DHIKI ZITAWAUA!!!!NAFIKIRI HIKI KITENGO KINATAKIWA KUBADILISHWA KABISA!!!LINGINE WAKIKAMATA GAI WAKIAMBIWA HIRI RA TIBA!!!HIRI RA MAHITA WANAKIMBIA KAMA PANYA AMEBANWA!!!!EMBU WAWE MAKINI JAMANI MTAWAUMISA WATANZANIA

MAGARI HAYAMALIZI RTE KILA SIKU TWASEMA MMELALA NA WAKE ZENU HATA WAKATI WA KAZI TEMBEENI BARABARANI

WAKO

MWANA!!!!'S
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom