Unafiki wa seif hamad

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Seif akipata shida imekwisha wengine wakionewa hilo si tatizo kwani mambo ni tofauti.


Tanzanian opposition legislators walk out over accord

Posted by africanpress on April 9, 2008
Publisher: Korir, api africanpress@getmail.no source.apa
Some 44 opposition lawmakers, out of whom 32 are from the Civil United front (CUF), 11 from Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) and one from the United Democratic Party (UDP), staged a walkout in Parliament in central region of Dodoma in protest of a proposal by Tanzania ruling party Chama cha Mapinduzi (CCM) to call a referendum on the political future of Zanzibar.

The Leader of the Official Opposition Civil United Front (CUF), Hamad Rashid Mohamed told APA Wednesday that opposition legislators would not participate in the ongoing National House business in a move aimed at protesting and putting pressure on the ruling party to sign the accord reached between two parties known as Muafaka.

Hamad said that the CCM and CUF delegates came to the talks aimed at ending the protracted political rift in Zanzibar, which has pitted the two rival parties, but did not deliberate on the proposed referendum as a condition for creation of a coalition government.

�Opposition legislators have walked out of the House to express dissatisfaction over the way the CCM-led government has handled the muafaka talks,� he said, thanking the rest of the opposition camp in the House for supporting them.

However, Hamad has declined to say how long they would stay away from the on going National assembly business.

On his part the Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta has said that he is going to consult and advise them(the opposition) to go for talks, and not otherwise, since Tanzanians believes in dialogue.

The walkout involved Member of parliaments from both CUF, whose rejection of the results of the 2000 and 2005 general elections in the Isles led to the standoff, and other opposition political parties.
President Jakaya Kikwete promised in his inaugural speech to the National Assembly soon after assuming power in late 2005 that he would leave no stone unturned in finding a lasting solution to the Zanzibar political impasse.

The Tanzania National Assembly which started its business Tuesday currently has a total of 321 legislators.


Tofautisha na hii hapa chini.

Wabunge CHADEMA wamsusa Kikwete


na Waandishi wetu


amka2.gif
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana waliandika historia kwa kuondoka bungeni mara Rais Jakaya Kikwete alipoanza kuhutubia Bunge mjini Dodoma, hatua hiyo ilimkera Rais Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema waliondoka kutilia mkazo wao kutotambua mchakato uliompa Kikwete urais, na kusisitiza mabadiliko ya Katiba na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mbowe, ambaye ndiye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisisitiza kuwa urais wa Kikwete umetokana na mfumo mbovu wa uchaguzi unaoendekeza wizi wa kura, chini ya uratibu wa vyombo vya usalama wa taifa.

Wakati wanaondoka Bungeni, Rais Kikwete alikatiza hotuba yake, akanyamaza huku uso wake ukisononeka; akawa ameduwaa, akakohoa kidogo, huku wabunge wa CCM wakipiga makofi kuwazomea CHADEMA; na baadaye alitoa kauli ya kejeli akisema, "Hata wasionichagua hawana serikali nyingine ni hiihii. Watakwenda, watarudi, hawana mwingine wa kumwomba yao yatimie zaidi ya serikali ya CCM ambayo mie ndiye rais wake."

Naye Pinda, wakati anaahirisha Bunge aliwakejeli wapinzani akisema, "Hata waliotoka nje wako kwenye runinga wakiangalia, ile ilikuwa geresha tuu… lakini kuna baadhi ya vyama vimeanza kuonyesha mwelekeo usio sahihi. Tuukatae!"

Lakini Mbowe alipozungumza na waandishi wa habari baadaye alisema CHADEMA wanachotaka ni mabadiliko ya Katiba na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi ambayo haitokuwa na upendeleo kwa chama tawala kama ilivyo hivi sasa.

Alisema wanatetea mabadiliko ya Katiba na sheria ambayo inawanyima fursa watu wanaopinga matokeo ya kura za urais mara yanapotangazwa na NEC, tofauti na matokeo ya ubunge yanayoweza kulalamikiwa na kupingwa mahakamani.

Aliongeza kuwa vyama vya upinzani haviwezi kuhatarisha amani, bali CCM ambayo inatumia vyombo vya dola kudhibiti matakwa ya umma na kuminya haki za wananchi.

Alisema madai ya kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na mabadiliko ya Katiba si ya siku za hivi karibuni bali ya muda usiopungua miaka 15 lakini CCM wamegoma kuyafanyia kazi.

"Watu wanafikiri kuwa madai haya ni mapya,.... hapana yalianza siku nyingi, hawa wenzetu waligoma kuyafanyia kazi, sasa sisi tunaonyesha kutokubali matokeo yaliyomuingiza Kikwete madarakani tunaonekana ni watu wa ajabu.

"Tunajua Kikwete amehuzunika kwa sisi kutoka pale ukumbini, tunafurahi kwa sababu ujumbe umemfikia na tuko tayari kuzungumza na wadau mbalimbali wa siasa juu ya ubadilishwaji wa Katiba na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi," alisema.

Aliongeza kuwa ni lazima viongozi walioko madarakani wajue kuwa Watanzania wa sasa si wale wa miaka 10 iliyopita, kwani wameendelea zaidi na wanazijua haki zao hivyo ni vema viongozi wakapunguza vitisho na kuangalia namna ya kutatua mambo kwa njia za mazungumzo.

Aliongeza kuwa jambo hilo ni ukandamizaji wa haki za binadamu na udidimizaji wa demokrasia kwa sababu katika mazingira ya sasa NEC na vyombo vya usalama vimekuwa vikishiriki kupika matokeo, ili kukipa chama tawala ushindi.
Alisema wanafanya hivyo si kwa faida yao tu bali hata kwa vizazi vijavyo ili demokrasia iweze kuchukua mkondo wake.
Naye Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya upinzani, Tundu Lissu, alisema wabunge wa CHADEMA hawajavunja kifungu chochote cha sheria au Katiba kwa uamuzi wao wa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Alisema ibara ya 100 ya Katiba kifungu cha kwanza na cha pili kinaeleza bayana haki za mbunge za kutoshtakiwa kwa kupinga jambo asilokubaliana nalo kwa njia zisizovunja sheria.

Alibainisha kuwa utaratibu huo ni wa kawaida kwa nchi zenye kujali demokrasia ambapo upande wa wachache una haki ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na utawala uliopo au jambo fulani.

Alisema hata Chama cha Wananchi (CUF) kiliwahi kufanya hivyo kwa kutowatambua marais wa Zanzibar ambapo walianza na Dk. Salmin Amour na baadaye kwa Amani Abeid Karume ambaye walimkataa kwa karibu miaka 10.

Alisema utaratibu huo ni mgeni kwa Tanzania Bara lakini ni njia muafaka kwa upande unaoonekana kuonewa au kutokubaliana na jambo fulani.

Miongoni mwa wanasiasa waliobeza hatua ya CHADEMA ni Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, aliyesema kuondoka kwa CHADEMA ukumbini ni fedheha kwa chama hicho na wafuasi wake.

Alidai Rais Kikwete, yuko tayari kusikiliza madai ya CHADEMA, lakini utaratibu walioutumia si wa kiungwana.
Hata hivyo, Maalim Seif, alipoulizwa kwa nini anawakosoa CHADEMA wakati CUF nao waliwahi kuchukua hatua kama hizo, alidai kuwa wakati huo ni tofauti na huu wa sasa.


Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Azaveli Lwaitama, aliwaunga mkono CHADEMA akisema madai yao ni ya msingi kwa kuwa yamejengwa katika mtazamo wa kisiasa, si kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa wanafalsafa, Dk. Lwaitama ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, alisema madai ya CHADEMA juu ya ushindi wake si wa kubezwa, kwani jamii kubwa ya Watanzania bado ina shata juu ya ushindi wa Kikwete.
"Hata angekuwa mtu mwingine yeyote yule mwenye akili timamu raia wa nchi hii, lazima ahoji kwa nini watu wana shaka juu ya ushindi wake, na CHADEMA wanamkataa Kikwete kwa mtazamo wa kisiasa na wala si kisheria,'' alisema.

Dk. Lwaitama alisema Katiba ya nchi inampa raia uhuru wa kutoa mawazo ambayo hayawezi kuhatarisha amani ya nchi, hivyo madai ya CHADEMA ni ya msingi.

Alisema endapo CHADEMA wangeamua kupinga ushindi wa Kikwete kwa kuandamana, ni wazi kwamba wangekuwa moja kwa moja wanapinga sheria za nchi zilizowekwa kwa misingi ya Katiba.
Aidha, alisema aliishauri serikali kuunda tume huru itakayochunguza sababu ya wananchi wengi kushindwa kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

Alisema kulingana na taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC), miongoni mwa watu milioni 20 waliojiandikisha, waliopiga kura ni asilimia 42.8, jambo linalotia shaka.

Akitolea mfano alisema walitegemea kuona idadi ndogo ya wapiga kura mara baada ya vita vya Iddi Amin kutokana na ukweli kwamba bado watu walikuwa na hofu ya kutokuwepo amani, lakini badala yake asilimia 85 walijitokeaza kupiga kura; na uliofuata waliopiga kura ni asilimia 84.

Aidha alisema ipo sababu pia ya tume hiyo itakayoundwa kuchunguza ni kwa nini vijana wengi wamejitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi huu, na wengi wao wamepigia vyama vya upinzani.

Katika hotuba yake, Kikwete aliahidi kuunda Baraza la Mawaziri la wachapakazi na hodari.

"Nawahakikishia ujio wa serikali yenye wachapakazi na hodari watakaoweza kuondoa urasimu serikalini. Watu watakaoshirikiana vema na wabunge bila kujali vyama vyao.

Katika hali ya kushangaza, Rais alisisitiza kuwa ufa wa udini umeanza kujengeka nchini katika kipindi cha utawala wake na kwamba ulionekana katika uchaguzi huu.

"Uchaguzi wa mwaka huu umeacha ufa hatari wa kidini ambao lazima tuchukue hatua thabiti kuzuia vinginevyo hakuna nchi… hatutakuwa tofauti na wenzetu wanaopigana huko. Nitashirikiana na viongozi wenzangu pamoja na wale wa dini kuinusuru nchi katika vita ya udini," alisisitiza.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanasema hoja za udini zimekuwa zinaibuliwa na makundi ya wafuasi na makada wa CCM, na baadhi yao walizisambaza kwa kasi kupitia ujumbe mfupi wa simu wakati wa kampeni.
Mmoja wa wanaharakati mahiri nchini, Gema Akilimali, akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), alishangazwa na kauli ya rais kuhusu udini, akisema mambo mengine yanasababishwa na viongozi wenyewe; akahoji sababu ya rais mwenyewe kuteua wabunge watatu wa awali (walioteuliwa jana) kati ya 10, ambao wote ni Waislamu.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliainisha mambo 13 yatakayoshughulikiwa na serikali yake katika miaka mitano ijayo ambayo ni kuimarisha umoja, amani, usalama wa nchi na Muungano, kukuza uchumi, kuboresha uwekezaji na biashara.

Alisema atawawezesha wananchi wa makundi yote hasa wajasiriamali kupata mikopo, kujenga na kuimarisha sekta binafsi, kutumia jiografia ya nchi kuwa lango kuu la biashara, kutunza rasilimali za taifa kwa maslahi ya umma.

Mambo mengine ni kuboresha mapato ya taifa, kupanua fursa za elimu kwa ngazi zote, kuboresha huduma muhimu za kijamii, kuimarisha utawala bora wa kidemokrasia, kuendeleza uhusiano wa kimataifa na kuongeza marafiki.

Kadhalika, kuongeza juhudi za kuboresha mazingira, kulinda mafanikio na kukamilisha mazuri yote yaliyopatikana kupitia serikali ya CCM.



Chanzo: Tanzania Daima
 
Seif kashakabidhiwa mrija ananyonya taratiiibu, ameanza kulewa mvinyo wa serikali ya umoja wa kitaifa mapema. Kama asingeingizwa serikalini angekuwa wa kwanza kupinga ushindi wa Dr. Shein lakini kwakuwa kapata ulaji basi ndio hivyo tena anajifaragu. Kusema kwamba wakati ule ni tofauti na sasa ni upofu wake tu kwani inajulikana muafaka wa sirisiri waliufikia mwaka jana mwishoni, sasa huo wakati ulio tofauti sijui ni upi. Amewasaliti wananchi wa zanzibar waliouwawa tarehe 26 & 27 Jan 2001 labda angetamani chadema nao waige staili yao lakini ukweli ni kwamba cuf na chadema wanatofautiana sana kuanzia muundo, ubora wa viongozi hadi ubora wa sera.
 
mbio zote zilizogarimu jasho la wazenji wengi na wanacuf wengi, zilikuwa anatafuta cheo, maslahi binafsi, ameshayapata, sasa wananchi msimsumbue, ameshabadilike yule si wa kwetu tena, anatumikia cheo na anatetea maslahi ya cheo, hamjui kuwa anapata mshahara mnono pale, nyie mnapata kwani? mnafikiri atawakumbuka kwa lolote pamoja na kwamba mlipigwa mabom pamoja naye
 
mbio zote zilizogarimu jasho la wazenji wengi na wanacuf wengi, zilikuwa anatafuta cheo, maslahi binafsi, ameshayapata, sasa wananchi msimsumbue, ameshabadilike yule si wa kwetu tena, anatumikia cheo na anatetea maslahi ya cheo, hamjui kuwa anapata mshahara mnono pale, nyie mnapata kwani? mnafikiri atawakumbuka kwa lolote pamoja na kwamba mlipigwa mabom pamoja naye
Ni mtu wa kumuogopa sana kwani yeye siku zote hupigania maslahi yake na katu si ya nchi. Yeye akipewa kitu basi Zanzibar imepata. Mwaka 1995 alisema kaibiwa lakini akasema wizi haukufanyika bara wakati ilikuwa wazi kuwa Mrema aliibiwa kura zake. Ni mtu mnafiki na hastahili heshima hata kidogo.
 
CUF ni waroho wa madaraka na wanakufa kama ifuatavyo damu ya wazenji na kura za wazenji zilizochakachuliwa zitawahukumu hakuna upinzani zenji
 
Jibu la Seif ndilo limeniacha hoi.
Eti wakati ule sio sawa na wakati huu!
Shame on him.
 
Seif Shariff Hamad si mafiki tatizo lenu nyie wabongo mtu akiwa mstaarabu mnamuona mnafiki na najua wengi wenu wanachama wa chadema hamumfurahii zitto kutokana na ukomavu wake wa kisiasa. Inakera kuwa na watu wanaopenda siasa za chuki. Hamjui kuwa siasa si ugomvi?
 
Seif Shariff Hamad si mafiki tatizo lenu nyie wabongo mtu akiwa mstaarabu mnamuona mnafiki na najua wengi wenu wanachama wa chadema hamumfurahii zitto kutokana na ukomavu wake wa kisiasa. Inakera kuwa na watu wanaopenda siasa za chuki. Hamjui kuwa siasa si ugomvi?

Unafki ya Seif ni kwamba yeye alishawahi kufanya kitendo kama walichofany chadema cha kutomtambua rais.
Leo yeye anawaona chadema wa ajabu sana kisa kapewa cheo.
Huo ndio unafki wenyewe.
 
Seif Shariff Hamad si mafiki tatizo lenu nyie wabongo mtu akiwa mstaarabu mnamuona mnafiki na najua wengi wenu wanachama wa chadema hamumfurahii zitto kutokana na ukomavu wake wa kisiasa. Inakera kuwa na watu wanaopenda siasa za chuki. Hamjui kuwa siasa si ugomvi?

Inawezekana ndugu yangu hutaki kusoma na kuelewa mantiki ya makala hizo hapo juu. Nimeonyesha kuwa mwaka 2008 Chadema waliwaunga mkono CUF kupigania kumalizwa kwa mgogoro wa Zanzibar. Je huoni kuwa Chadema walifanya hivyo kuwaunga mkono wenzao ambao walidai kuwa wamedhulumiwa? Je, kulikuwa na maslahi binafsi kwa Chadema katika hilo? Hapana ila utaifa na imani kuwa "dhuluma popote ni dhuluma pote".

Sasa wewe unadai kuwa Seif ni mstaarabu neno ambalo kwangu silikubali kwetu sisi Waafirka neno sahihi ni Wastaafrika au "Waraiika'. Seif miaka yote ametanguliza maslahi yake mbele. Yeye asipopata kile anachokitaka kadhulumiwa ila mwenzake mwingine akidhulumiwa yeye ukimbilia kusema kuwa yule hakudhulumiwa. Sijui suala la Zitto linatokea wapi hapa. Tunazungumzia msimamo wa Chadema ulionyeshwa jana.
Chadema wanadai haki yao na wametumia njia ambayo imekwisha kuwa utamaduni wa nchi yetu na kwa kweli wa wanademokrasia duniani ya kupinga dhuluma ikiwa ni pamoja na kumsusa na kumuabisha yule anayekudhulumu. Kua ndugu yangu Tanzania ya leo sio ile ya jana!
 
Dhambi ya kuwa mnafiki huwa mtu analipwa hapahapa duniani haisubiri ufe. Kama Seif anabisha amuulize Sita. Huyu bwana ni mnafiki wa kutupwa. subiri wapemba watutakapo pata hekima na wakajua kuwa naye ni msanii kama wasanii wengine tu wa kisiasa hapo ndipo patachimbika. What a fool?
 
Seif Sharrif Hamad ni msaliti na mroho tu wa madaraka aliyekubali kuolewa na CCM kwa kupewa umkamu wa rais. Akumbuke pia kuwa maiti za watu waliokuwa wanapigania maslahi na haki ya CUF na zanzibar kwa ujumla January 2001 ndio zilizomfikisha hapo. CHADEMA wanadai haki kwa njia ya amani na utulivu kabisa!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom