Unafiki wa kusubiri watu wafe tuwasifu unakera

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Imekuwa kawaida Sana pindi mtu anapofariki kupata sifa nyingi kutoka kwa wanajamii hasa wale waliomfahamu au hata kumsikia tu wakati wa uhai wake.

Kwa dunia ya sasa yenye Utandawazi uliokithiri ukichagizwa na maendeleo ya huduma za mitandao ya "internet" tabia hii nayo imehamia mitandaoni.

Kwa utafiti mdogo uliofanyika watu wengi kwa Sasa wamekuwa na kasumba ya kukimbilia mitandaoni pindi wanaposikia mtu fulani kafariki.

Machapisho mengi "Post" hutiririka kumsifia marehemu kwa kila tabia, upole, uaminifu, ucheshi na kadharika.

"Hujafa hujaumbika" wahenga walisema na ni kweli kwenye jamii hii tuliyonayo kuna tabia "kufa usifiwe" ambapo hata wale waliokuchukia wanaibuka kukulilia.

Wale ambao walikuwa hawakufahamu nao wanaiga mkumbo wa kilio na kuabudu pasipo kujua ni mtu wa namna gani aliyefariki.

Vuta picha unakuta post mtandaoni Imeandikwa "Pumzika kwa amani...hukuwa na baya na mtu" kwenye orodha ya waliotoa maoni kwenye hiyo post unakuta Kuna mtu anaulizia marehemu alikuwa ni wa wapi na ni nani mbona sikuwahi kumuona?

Muda si mrefu ukirejea tena mtandaoni unakutana na post nyingine kuhusu marehemu chakushangaza aliepost ni yule aliyekiri kuwa hakuwahi kumfahamu marehemu kwenye post ya kwanza, umeelewa hapo?

Ni kizungumkuti kwanini tabia hii inatamalaki namna hii tena tunawanafkia wafu.

"Binadamu wengi wanakupenda ukifa" anasema Tulizo Jeremiah kuonyesha kuwa binadamu hawana Urafiki na mtu akiwa hai wanasubiri afe kisha wampende.

Ukipita makaburini unaona rundo la maua limeyafunika makaburi hivi wewe binafsi umewahi kupokea maua kutoka kwa Marafiki zako Kama ishara ya upendo kwako?

Si hivyo tu ni Mara ngapi wewe umempelekea rafiki yako mapambo ya maua kuonyesha unampenda, unasubiri afe ukaweke juu ya kaburi lake?

"Upendo ni tiba" tunawathamini kiasi gani watu wetu wakiwa hai, huu ni mtihani mgumu kwetu.

Katika maoni yake Nikusekela Hezekia anasema tabia hii ya kusifu wafu ni unafki uliopindukia ambao haupaswi kufumbiwa macho jamii haina budi kubadilika ili kuwapenda watu wakiwa hai sio kusubiri wafe ndio wapendwe.

Kama ilivyoelezwa mwanzo wahanga wakubwa wa tabia hii ni watumiaji wa mtandao ambao muda mwingine hata shughuli za misiba hawaudhuriii kwenye jamii zao bali wamejipa majukumu ya Kupost picha za marehemu mitandaoni.

Tubadilike tabia ya kusifia wafu mitandaoni inakera.

peter Mwaihola


1654511636206.jpg
 
Back
Top Bottom