Unafiki wa JIDE na MWANA FA kwenye misiba,wa ngwear waliahirisha shoo wa LANGA wamepiga shoo.

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
Ni jambo la kustaajabu na kusikitisha kwa wasanii JIDE NA MWANA FA ambapo wakati wenzao wakiomboleza na kulala kwenye msiba wa LANGA wao wanapiga show za nguvu.
uko wapi utu waliouonesha kwenye msiba wa ngwear walipotangaza kuahirisha shoo zao.TAARIFA ZA MSIBA ZILIKUWEPO TOKA JUZI JIONI.huu ni ubaguzi na dhahiri inaonyesha wanachagua msiba,kifupi binafisi naona HAPA WAMEKOSEA PAKUBWA NA WANAPASWA KUOMBA RADHI.
R.I.P LANGA
r.i.p langa
R.I.P LANGA
 
Si wao tu, hata vyombo vya habari hawajaupa umuhimu msiba huu, haujapata coverage hata robo ya walichofanya kwa Ngwair.
 
Jamani mimi siwalaumu jide na FA tu, bali hata mimi sijashtuka sana nlipopata habari za kifo cha langa lakini kifo cha Ngwair nilishtuka sana, hii ishu ni ya watanzania wote hatujaupa uzito msiba wa Langa, media ndo usiseme. Kuna uwezekano mkubwa Ngwair alikuwa na mtandao mkubwa sana kuliko Langa wakati wa uhai wake, pia vibao vyake vilibamba sana kuliko vya langa..
 
Tatizo wanaweza kuhairisha alafu kabla show tene ikatokea TID au Mr Blue kavuta.
Si unajua sembe sasa hivi inamaliza vijana kama ugojwa wa kideri. Mitaani ndio usiseme, vijana wanapuputika tu.
 
Pamoja na yote, ukweli ni kwamba ilibidi wahairishe tu, kwa sababu hakuna tofauti yoyote ya Ngwair na Langa; wote ni wasanii wa Bongo Flava. Kiukweli hawajafanya uungwana!
 
langa alikuwa msanii mkali but hakuwa msanii mkubwa kama Ngwea..pia hakuwa mtu wa watu kiivo ata impact yake kwenye game haifikii ata robo ya ngwea..nafikiri iyo ndio sababu kubwa

alafu Ngwea alizikwa na wengi sio sababu tu alikuwa msanii,ngwea alikuwa mtu poa sana ( mshkaj) ndio maana watu waliifeel...ungepata nafasi ya kukaa na ngwea ata dakika 10 kipnd cha uhai wake ndio ungenielewa vizuri
 
Mbona hamsemi kuhusu vyombo vya habari vilivyyohairisha program zao NA kuonyesha misiba ya wengine siku nzima. We una bifu NA jide na mamwanafa unatafuta wa kukuunga mkono katafute pengine... useless character
 
Hakuna wimbo wa jide na langa, wala na fa, alikua msanii ila sio mkubwa hvyo, ngweah alikua msanii mkubwa, fikir kabla hujapost ki2
 
hata langa alikuwa msanii mkubwa

Sikiliza kijana kuhairisha show ---- cost implication kubwa sana. Hivyo huwezi hairisha hairisha kila siku

Pia huwezi kufananisha Langa na Ngwea hata kidogo, Langa sio msanii mkubwa kama Ngwea ukitaka kujua angalia umaarufu wa Langa na Ngwea katika kushirikishwa na wasanii wengine utagundua kuwa Ngwea ameshirikiana na karibu wasanii wote wakubwa Bongo hata hao waliohairisha amefanya nao nyimbo kibao (Jide na FA)

Langa kwa Ngwea ni sawa na kufananisha Messi na Ngassa hamna mtu hatakayekuelewa
 
Pamoja na yote, ukweli ni kwamba ilibidi wahairishe tu, kwa sababu hakuna tofauti yoyote ya Ngwair na Langa; wote ni wasanii wa Bongo Flava. Kiukweli hawajafanya uungwana!

Acheni uswahili huo, muziki ni kazi wewe waache kufanya kazi kisa kuna msiba wa Langa. Ngwea na Jide wako pamoja kwenye game long time na walikuwa watu wa karibu. Sijawahi kusikia ukaribu wa Jide na Langa...

Huyo MwanaFatuma yeye alikuwa anaambiwa tu sasa aihirisha shoo, sasa tangaza tarehe mpya na Mliberali wake Ruge, wala hakuwa na maslahi na msiba wa Ngwea kwa kuwa Ruge alishamnyonya na kumfrustrate Ngwea enzi za uhai wake
 
Wewe ndio mnafiki. Kuahirisha show kungetegemea ukaribu wake na marehemu. Plus langa sio hata level ya jide na sijui kama tunaweza hata kumuita msanii. Binafsi nilishasahau kama yupo!

Umeona lakini show ya jide ilivyobamba?
 
Kwa kweli Langa alikua under ground Maarufu sana hivyo Wavuta Bangi na Wabwia unga nao wahairishe kutumia ktk kipindi hichi cha Maombolezo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom