Nikukumbushe
JF-Expert Member
- Jun 4, 2013
- 2,602
- 408
Wakati wa uchaguzi wa 2005,walikuja na kauli mbiu lukuki ikiwemo "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"kinyume chake yamekuwa maisha magumu kwa kila mtanzania.Kwa sasa hiyo kauli mbiu haipo tena isipokuwa wanajisifia wameleta maendeleo. Kusema kuwa wameleta maendeleo, kuwambia watanzania kuwa wameleta maendeleo sio kazi yao bali wananchi ndio watasema kuwa kweli kuna maendeleo.
Wapi uliona mtu anajisifia peke yake,hata ikitokea basi ni kimoyomoyo na siyo hadharani. Eti wasema wamejenga barabara,shule,hosptali nk,kama hakuna huduma zinazotolewa na miundo mbinu hii,kuna faida gani kwa wananchi? Shule hazina walimu ,vitabu,maabara,hospitali hali kadhalika,kuna haja ya kusifia kweli kama sio unafiki wa Nape na CCM?
Hata kama zina walimu na vifaa,je kuna uwiano wa huduma hizi na idadi ya wahusika? Leo hii wanasimama majukwaani na kutamba CCM imeleta maendeleo,kwa lipi? Hizi ni kodi za watanzania na lazima zirudi kwa mfumo usio wa moja kwa moja(indirect system),sasa suala la kujisifia linatoka wapi kama sio unafiki ni nini?
Kwa lazima au kwa hiari/kwa kusifiwa au kutosifiwa kuleta maendeleo ni lazima,kwa kuwa wanatumia kodi zetu! Sasa kjuna haja gani ya kuwasifia/kujisifia wakati ni wajibu wao kufanya hivyo. Hata kama kwa lazima,kupata returns ya kodi zetu ni haki zetu,haki haiombwi ila inadaiwa na ni lazima haki ya kodi zetu itendeke.
Sasa wanataka kuwasifia kwa lipi walilolifanya? Wangekuwa wamekamata mafisadi,watu walioficha pesa zetu,wafanyabiashara wa madawa ya kulevya,wezi wa EPA,rushwa nk,wangekuwa wameweka mikataba yote hadharani,hapa ndio walistahili kusifiwa.Lakini kwa kuleta siasa hata kwenya mambo ya msingi,siwezi kuwasifia kamwe na hawana hadhi ya kusifiwa.
Ahadi kibao,lakini zimekuwa sehemu ya kuwadanganyishia wananchi ili waendelee kuficha pesa(kodi za wananchi) nje. Sitawasifia kamwe ccm kwa uovu,ufisadi,dharau,rushwa,uonevu na ukandamizaji wao wa haki za raia,na uvurugaji wa amani ya nchi kwa kusingizia maandamano ya CHADEMA,wakati wao ndio wenye dola. CCM haifai na ni wanafiki wakubwa.
Nawasilisha!