Unafiki wa balozi wa Kenya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki wa balozi wa Kenya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TX, Jul 22, 2009.

 1. T

  TX Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Jackson Odoyo
   
  Last edited: Jul 22, 2009
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Huo unafiki uko wapi? Mimi naona anatoa tu ushauri. Au nini haswa unafiki wake?
   
 3. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nafikiria aungane na waslam kutupatia mahakama hiyo
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo mtu asipo kubaliana na wewe basi ni mnafiki? Hapa angepinga kuwepo kwa mahakm hiyo unge lalamika mtu wa nje anaingilia mambo ya ndani. Sorry hapaumekosa hoja.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  tumechoka na hoja mfu
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Balozi wa Kenya anatoa ushauri kuzingatia uzoefu wao katika swala nyeti hili.Huo unafiki sijui ni upi.

  Ni vema kutafuta kichwa cha habari kwa umakini zaidi pale mtu unapotaka kuanzisha mada.Vinginevyo utataka wasomaji/wachangiaji waanze kukujadili wewe mtoa mada badala ya mada.
   
 7. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mahakama kama hizi zimeshashindwa huko kenya, zinawaletea kichefuchefu na usumbufu, wanajuta kwanini walianzisha. ni bora ametoa ushauri ili watu waelewe, tusiingie kichwa kichwa.

  hawa jamaa tatizo lao, sijui hawaelewi? ati unaleta jambo kwenye secular govt halafu unasema NI JAMBO LA IBADA, jambo la ibada kwenye selikali ya watu wasoipenda hiyo dini yako?ingekuwa islamic gvt sawa, lakini hii ni secular jamani. hapa tz huwa tunavumiliana tu,ila hakuna hata anayependa dini ya mwenzake kiundani, mimi sipendi hata kusikia dini ya kiislam, na waislam hawapendi dini ya kikristo, lakini kwasababu wote tulizaliwa hapa, tunavumiliana, tunazidi kupendana na kushirikiana kwa uvumilivu. hayo ndo maisha.tusipovumiliana, patakuwa hapatoshi, haya maisha tunayoishi magumu sasahivi yatakuwa magumu mara mia kwasababu ya vita. tupilia mbali huko upuuzi huuu unaoligawa taifa.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Balozi ametoa mawazo yake tu na kutushauri ulitaka aseme kwa nini hatujaanzisha hadi sasa ??hapo ungemsifia??no way hayupo kwa ajili ya upande mmoja anatushauri kama taifa....
   
 9. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi akitokea Balozi wa Msumbiji ama Rwanda, akatoa ushauri wa ubaya wa Waraka wa Kanisa Katoliki kutakalika. Hayo hayatokuwa mawazo yake bali itaonekana ni kuingilia masuala ya nchi. Lakini huyu kwa kuwa yuko upande wa Wakristo, ahh anaonekana kasema.
   
 10. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mabalozi wana akili, hawawezi kufanya hivyo, zaidi watasapoti. labda kama balozi huyo atakuwa mjahidina anayevaa visuruari vifupi...hahaha. sehemu ya chini ya suruari amekata kama vile amekata na akili zikamtoka...
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani kumbukeni freedom of speech ata kama ni raia wa nje.
  Alafu akili ni kama nywele kila mtu ana zake,kumbuka maneno hayalipiwi VAT so u can talk anything
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwani balozi kasema nini?
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180


  Mbona hoja imekimbizwa jamani?
  Jamaa kasepa baada ya kuona mashambulizi!!!!
  tuh thuh tuh tuh!!!!kwe kwe!!!!
  Usiwe mwoga kukosolewa Odoyo...ndo kiume!
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  amesema mahakama za kadhi kule kenya zinawaletea usumbufu sana, na wanajuta kuzianzisha, laiti kama wangejua wangekuwa wamefanya kwa njia nyingine bora zaidi ambayo haingeleta mkanganyiko kwao kwa sasa. na anasema watz tuwe makini kulifanya hilo.

  nafikiri alifuatwa kwenda kuulizwa maoni yake kwasababu watu wanasema kule kenya mahakama hii ipo. hivyo waandishi wa habari walimfuata kumwuliza maoni yake na uzoefu wa nchi yake, ndo akatoa jibu hilo. sio kwamba alikuwa anaingilia mambo ya ndani ya nchi yetu, alichokozwa, au kwa lugha nzuri ,aliuzlizwa. asingeulizwa asingesema hivyo.

  nashangaa wanaomlaumu.
   
 15. m

  mwaka New Member

  #15
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni vema sana kutenganisha sayansi na imani katika maauzi, historia inaonesha maamuzi mengi zamani yalitokana na imani za dini na yalishindwa. kama mtu ahamini asome zile philosoph za greace thinker Plato
   
 16. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  watu kama hawa ni wa kusamehewa...kafunza kanamnyefuanyefua ktk bongo lake
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu,
  Nadhani tunachanganya mambo hapa.
  1. Kichwa cha habari kinasema "Unafiki wa balozi wa KEnya tz"...Ukisoma mada unashangaa, badala ya kuona unafiki, unaona mtu anatoa ushauri wake kuwa, mkitaka kuanzisha mfanye homework yenu vizuri kwa maana wao ambao tayari wanazo, wanaona changamoto zinazowakabili.
  2. Ulishawahi kusikia " best/good practices" that needs to be replicated? Kama jibu ni ndio, basi utakubaliana nami kuwa hakuna haja ya kufanya makosa pale mwenzio alishayafanya.Unachotakiwa ni kuchunguza alikosea nini na wapi na wewe uanzishe chako kwa kurekebisha yale makosa na siyo kuyarudia vilevile.
  3. Inashangaza unaingiza udini hata mahali ambapo sio pake.Waraka - ambao ni mawazo ya kundi fulani katika jamii kuhusu suala fulani ambalo hata kikatiba watu wana uhuru kutoa mawazo yao, haifanani na kuanzisha taasis ndani ya mfumo wa serikali ambao watu wa imani zote watawajibika kugharamia kwa njia ya kodi zao.jARIBU KUTOFAUTISHA NDUGU.
  4. Usihukumu watu kwa misingi ya dini kwa maana utashangaa utawabandika watu dini ambazo siyo zao!
   
 18. U

  Umushoshoro Senior Member

  #18
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45

  Kaka bado sijakuelewa
   
 19. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na Jackson Odoyo
  WAKATI mjadala wa Mahakama ya Kadhi ukizidi kupamba moto, balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, ameionya serikali ya Tanzania kuwa inapaswa kuwa makini katika suala hilo, akikiri kuwa limeshaanza kuwasumbua kwao.

  Nchini Kenya ambako idadi ya Waislamu ni asilimia 10 ya watu wote, Mahakama ya Kadhi imeruhusiwa, lakini inafanya kazi kwenye maeneo yaliyo na Waislamu wengi hasa ukanda wa pwani; Mombasa na visiwa vya Lamu na Malindi.

  Akizungumza na Mwananchi jana katika mahojiano maalumu ofisini kwake, Balozi Mutiso alisema suala la Mahakama ya Kadhi linapaswa lifanyiwe kazi kwa kina zaidi kuepuka serikali kuingia kwenye lawama baadaye.

  "Ninaunga mkono kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoitoa hivi karibuni juu ya kuundwa kwa kamati akitaka pande zote mbili (serikali na viongozi wa Kiislamu) ili zikae pamoja na kufikia mwafaka kabla ya Kadhi kuruhusiwa," alisema Mutiso.

  "Suala hili ni nyeti sana na lina umuhimu wake katika ngazi ya serikali na kijamii, hivyo haipaswi kukimbiliwa na kugeuzwa la mzahamzaha ni lazima kwanza serikali ikajifunze kutoka nchi nyingine na historia kamili ya mahakama hiyo katika nchi hizo."

  Mutiso alifafanua kwa kusema: "Kenya, suala la Mahakama ya Kadhi liko kisheria kwa sababu iko ndani ya katiba ya nchini na iliingizwa katika katiba hiyo tangu enzi za Waingereza, na si serikali ya Kenya."

  Alisema sehemu ya pili ya katiba ya Kenya inaeleza mahakama nyingine mbali na zile za kiraia, ikiitaja Mahakama ya Kadhi kuwa mojawapo ya mahakama hizo.

  Katika sehemu hiyo, kifungu cha 65 kinaeleza: "Bunge linaweza kuunda mahakama zitakazokuwa chini ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Kijeshi, na mahakama itakayoanzishwa, kwa kuzingatia katiba hii, ina mamlaka na nguvu kulingana na itakavyopewa na sheria yoyote."

  Kifungu hicho kinaendelea kusema kuwa, "Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusimamia kesi yoyote ya kijinai au ya madai kabla ya mahakama ya chini yake au Mahakama ya Kijeshi, na inaweza kutoa amri, kutoa hati ya kuitwa mahakamani na kutoa maagizo kwa kadri itakavyoona kuwa sahihi kwa lengo la kuhakikisha kwamba haki inasimamiwa vizuri na mahakama hizo."

  Kifunga cha 66 (1) cha katiba ya Kenya ndio kinaunda Mahakama ya Kadhi kikisema: "Kutakuwa na Kadhi Mkuu... wa makadhi wengine wote kama itakavyoelezwa au chini ya Sheria ya Bunge."

  Balozi Mutiso alifafanua kuwa, suala hilo la Kadhi halina budi kuangaliwa kwa makini kabla ya kuanzishwa kwa kuwa lina mambo mengi ya kuzingatiwa.

  Awali, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, balozi huyo alitaja mambo mbalimbali yanayopaswa kufanyiwa kazi kabla ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

  Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na wafanyabiashara kutowekewa mfumo mzuri wa soko, hususan soko la pamoja.

  "Suala la soko la pamoja haliwezi kufanikiwa kabla ya mfumo wa biashara kurekebishwa; mfano," alisema na kuongeza: "Wafanyabiashara kutoka Kenya wakitaka kufungua akaunti hapa ni lazima wawe na kibali cha kufanya kazi pamoja na pasi ya kusafiria, kitu ambacho ni kikwazo."

  Mbali na suala hilo, balozi huyo alisema kuwa mfumo wa huduma ya kutoa pesa kwenye ATM sio mzuri kwa sababu ATM zote zinatoa fedha za Kitanzania tu, wakati Kenya kuna mfumo wa dola na shilingi ya Tanzania na Kenya kwa wakati mmoja:"

  "Mfumo huu unaotumika Kenya ni mzuri na unasaidia sana kwa sababu wafanyabiashara ni watu wenye matumizi ya haraka, hivyo hayo ni kati ya mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi haraka," alisema.

  Source: Mwananchi 21 July 2009
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu TX,
  Kufuta ulichobandika hapa, ambacho ndicho kinachofanyiwa rejea na wachangiaji siyo ustaarabu maana wachangiaji wanaonekana wazushi!
  Rudisha, au omba Mods wafunge mjadala huu.
   
Loading...