S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Mimi niseme wazi humu kuna wengi ni watu ambao kama usipokuwa mfatiliaji utadhani ni watu ambao kweli wanaumizwa sana na kitendo cha Mkurugenzi wa JF Mello Kukamatwa. Wengi wanapiga kampeni FREEMAXENCEMELLO na vitu vingine viiingi.
1. Je, mnakumbuka mjadala wa Zitto Zuberi Kabwe na Nnape Nauye kuhusu Mswaada wa Habari?????. Wengi na leo wanashupaa FREEMAXENCEMELLO bila kujua mwanzoni mliona kama Wakina Zitto ni vichaa na mlikaa pembeni katika mjadala huu leo mpaka kwenye Facebook, Twitter, na Instagram mmeandika FreeMaxenceMello kwanini mwanzoni mlikuwa mnashadadia hamkujua yanayokuja.
2. Kuna mengi sana yaliyongelewa kuhusu Swala la Mswaada wa Habari kuna wengine humu badala ya kujadili na kushauri ili serikali ichukue yaliyo mazuri, mlijaa uchama badala ya Utaifa. Mlisifia sifia na wale walioonyesha hofu kuhusu Mswaada mliwaona kama ni watu ambao hawafai. Leo hii eti kila mtu FREEMAXENCEMELLO.
Kwa wale ambao mmekuwa mkipigania utu na haki ya kupata na kutoa habari tangu mwanzo nyie mna haki ya kuweka picha ya Maxencemello hawa wanajijua vyema kabisa na nafsi zao haziwasuti. Wengine mnajijua kwani mlikuwa mnaona kama wanaoupinga Mswaada wa Sheria kama ni watu wasiofaa. Mswaada ulipitishwa na ukawa sheria leo sheria hiyo hiyo ambayo mliiunga mkono baadhi yenu mnasema FREEMAXENCEMELLO
Tufike hatua kama Bashe akiongea maswala ya Kitaifa tumuunge mkono hata kama hatuko naye kichama na Tundu Lissu akiongea maswala ya msingi katika Taifa tumuunge mkono kama anaongelea maswala ya msingi katika Taifa. Na huu ndo Uzakendo. Eti unahangaika na tawi wakati mti ulivyokuwa unapandwa ulikuwa unasifia kuwa ni hatua nzuri.
Mkiwa mnaendelea na kampeni hii mnatakiwa baadhi yenu mjitafakari sana.
Tubadilikeni.