Unafiki tulio nao baadhi ya Wana JF walio wengi kuhusu kampeni ya FREEMAXENCEMELLO

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
500
Mimi niseme wazi humu kuna wengi ni watu ambao kama usipokuwa mfatiliaji utadhani ni watu ambao kweli wanaumizwa sana na kitendo cha Mkurugenzi wa JF Mello Kukamatwa. Wengi wanapiga kampeni FREEMAXENCEMELLO na vitu vingine viiingi.

1. Je, mnakumbuka mjadala wa Zitto Zuberi Kabwe na Nnape Nauye kuhusu Mswaada wa Habari?????. Wengi na leo wanashupaa FREEMAXENCEMELLO bila kujua mwanzoni mliona kama Wakina Zitto ni vichaa na mlikaa pembeni katika mjadala huu leo mpaka kwenye Facebook, Twitter, na Instagram mmeandika FreeMaxenceMello kwanini mwanzoni mlikuwa mnashadadia hamkujua yanayokuja.

2. Kuna mengi sana yaliyongelewa kuhusu Swala la Mswaada wa Habari kuna wengine humu badala ya kujadili na kushauri ili serikali ichukue yaliyo mazuri, mlijaa uchama badala ya Utaifa. Mlisifia sifia na wale walioonyesha hofu kuhusu Mswaada mliwaona kama ni watu ambao hawafai. Leo hii eti kila mtu FREEMAXENCEMELLO.

Kwa wale ambao mmekuwa mkipigania utu na haki ya kupata na kutoa habari tangu mwanzo nyie mna haki ya kuweka picha ya Maxencemello hawa wanajijua vyema kabisa na nafsi zao haziwasuti. Wengine mnajijua kwani mlikuwa mnaona kama wanaoupinga Mswaada wa Sheria kama ni watu wasiofaa. Mswaada ulipitishwa na ukawa sheria leo sheria hiyo hiyo ambayo mliiunga mkono baadhi yenu mnasema FREEMAXENCEMELLO

Tufike hatua kama Bashe akiongea maswala ya Kitaifa tumuunge mkono hata kama hatuko naye kichama na Tundu Lissu akiongea maswala ya msingi katika Taifa tumuunge mkono kama anaongelea maswala ya msingi katika Taifa. Na huu ndo Uzakendo. Eti unahangaika na tawi wakati mti ulivyokuwa unapandwa ulikuwa unasifia kuwa ni hatua nzuri.

Mkiwa mnaendelea na kampeni hii mnatakiwa baadhi yenu mjitafakari sana.

Tubadilikeni.
 
Zuwenna

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,828
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo
 
Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,170
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo
Nani ni mfuata sheria?
 
Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,555
2,000
Hata mleta thread ni mnafiki tu

Kwanza leo umeenda keko..?

[HASHTAG]#freeMaxenceMelo[/HASHTAG]
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,973
2,000
Wote tupige kelele kwanza kuwa Max aachiwe huru bila kujali hitilafu hiyo. Tusutane akishawekwa huru!
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,964
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo
Bunge kibogoyo haaaa!
 
Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,030

Nakuunga mkono tatizo siyo Magufuli na chama chake kila siku ninaitwa mtu wa kijani. Mimi najua wabaya wa hii nchi ni kambi ya upinzani ndio waliotufikisha hapa tulipo. Wapinzani wa kweli walishatutangulia mbele ya haki kina Chief Fundikila Abdalah, James Mapalala na mzee Kasanga Tumbo. tatizo hawa wazee waliingizwa mjini na wapiga deal kina Marando na Lamwai Dr. Lengo lao la kudai katiba mpya lilizimwa na mamluki wa ccm kina Marando, Lamwai na Kina Mtei. Hii katiba ni ya chama kimoja na inampa nguvu nyingi rais na chama chake kwanini watu wabobezi wa sheria kama Lamwai na Marando walikubali kuibadilisha NCCR kuwa chama cha siasa na kuacha lengo la uanzilishwaji wake? Tunamlaum rais wakati anatumia katiba. Magufuli anajua katiba inamlinda hata afanyeje hawezi shitakiwa lazima tukubaliane na msemo huu DON'T BLAME THE PLAYER BLAME THE GAME
 
Mbona wailopita walitumia katiba hiyo nikweli katiba inatakiwa mpya kwa masirahi mapana ya nchi tena ita mrahisishia rais kutawala ambapo sasa anakomaa mwenyewe kila idara nadhani atakuwa na stress za kutosha ukibana watu wasiwe huru kuongea utapataje taarifa (call a spade a spade not a big spoon)
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,306
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo
Comment yako ina walakini...
 
kulwa MG

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
1,290
2,000
naona tunakumbuka shuka wakat kumekucha..kuna wajinga mwanzoni mwa mjadala wa mswada wa sheria ya habar walijifanya wao ndio wenye nchi na mawazo ya wengine ni upuuzi,lakn sasa hivi wanaanza kukumbka kumbe tuliokuwa tunaupinga tulikuwa sahihi..
 
Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,030
2,000
Mbona wailopita walitumia katiba hiyo nikweli katiba inatakiwa mpya kwa masirahi mapana ya nchi tena ita mrahisishia rais kutawala ambapo sasa anakomaa mwenyewe kila idara nadhani atakuwa na stress za kutosha ukibana watu wasiwe huru kuongea utapataje taarifa (call a spade a spade not a big spoon)
Nadhani hujanielewa wao wana mambo mengi machafu wameyafanya mpaka sasa hatuwezi kuwashitaki pia hawataweza kumuumbua huyu jamaa kama nyerere alivyofanya wakati wa Mwinyi sababu wanajua ni wachafu atawaanika na uchafu wao unaoshwa na katiba yetu. Nyerere aliweza kuwakemea hadharani sababu alijiamini kuwa ni msafi lakini si Mwinyi wala Mkapa ama Kikwete wana ubavu huo maana akiwajibu watapata aibu na hii yote lawama inaenda kwa wapinzani hawakutumia akili wakati vyama vingi vinaanza. Ujinga wao ni kwamba walijua Mwinyi na CCM hawakupenda vyama vingi maana kamati ya Nyalali ilisema 20% tu ya Watanzania walipenda vyama vingi ila nyerere akawashinikiza hivyo mpaka hapo walitakiwa kukomaa mpaka ipatikane katiba mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka 1995 hata kama kungekua na serikali ya muda chini ya Mwinyi najua Mwalimu angetusaidia kupiga chapuo lakini wakaingia mkenge wa ccm ktk uchaguzi hapo ndiyo kosa lao kubwa. Hata kama wangepata rais sidhani kama wangekua na wabunge wengi kuibadilisha katiba ccm wasingeunga mkono.
 
Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,011
2,000
Nadhani tunachanganya mambo, kesi ya Mex inahusiana na masuala ya Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crimes Act) na hii nyingine Electronic and Postal Communications (Electronic Communication Numbering and Addressing) na siyo Sheria ya Huduma za Habari
 
kama kazz

JF-Expert Member
Apr 28, 2015
1,060
2,000
Mimi niseme wazi humu kuna wengi ni watu ambao kama usipokuwa mfatiliaji utadhani ni watu ambao kweli wanaumizwa sana na kitendo cha Mkurugenzi wa JF Mello Kukamatwa. Wengi wanapiga kampeni FREEMAXENCEMELLO na vitu vingine viiingi.

1. Je, mnakumbuka mjadala wa Zitto Zuberi Kabwe na Nnape Nauye kuhusu Mswaada wa Habari?????. Wengi na leo wanashupaa FREEMAXENCEMELLO bila kujua mwanzoni mliona kama Wakina Zitto ni vichaa na mlikaa pembeni katika mjadala huu leo mpaka kwenye Facebook, Twitter, na Instagram mmeandika FreeMaxenceMello kwanini mwanzoni mlikuwa mnashadadia hamkujua yanayokuja.

2. Kuna mengi sana yaliyongelewa kuhusu Swala la Mswaada wa Habari kuna wengine humu badala ya kujadili na kushauri ili serikali ichukue yaliyo mazuri, mlijaa uchama badala ya Utaifa. Mlisifia sifia na wale walioonyesha hofu kuhusu Mswaada mliwaona kama ni watu ambao hawafai. Leo hii eti kila mtu FREEMAXENCEMELLO.

Kwa wale ambao mmekuwa mkipigania utu na haki ya kupata na kutoa habari tangu mwanzo nyie mna haki ya kuweka picha ya Maxencemello hawa wanajijua vyema kabisa na nafsi zao haziwasuti. Wengine mnajijua kwani mlikuwa mnaona kama wanaoupinga Mswaada wa Sheria kama ni watu wasiofaa. Mswaada ulipitishwa na ukawa sheria leo sheria hiyo hiyo ambayo mliiunga mkono baadhi yenu mnasema FREEMAXENCEMELLO

Tufike hatua kama Bashe akiongea maswala ya Kitaifa tumuunge mkono hata kama hatuko naye kichama na Tundu Lissu akiongea maswala ya msingi katika Taifa tumuunge mkono kama anaongelea maswala ya msingi katika Taifa. Na huu ndo Uzakendo. Eti unahangaika na tawi wakati mti ulivyokuwa unapandwa ulikuwa unasifia kuwa ni hatua nzuri.

Mkiwa mnaendelea na kampeni hii mnatakiwa baadhi yenu mjitafakari sana.

Tubadilikeni.
Kwa hiyo unataka tufanyeje swala sio kusimamia sheria inafatwa au sheria ipo kwa makapuku tu max aachiliwe mambo mengine badae
 
mtunzasiri

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
1,344
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo
Nani wako tayari kupeleka sheria zilekebishwe? Ccm hell no hawana wala hawafikirii hayo wao wanawaza kuwabana ukawa kimbe wanajibana wenyewe tuu twendelee kuisoma namba
 
Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,440
2,000
Tatizo ni sheria ile ya habari
Tatizo sio Magufuli
Magufili ameikuta hii sheria
Yeye anaisimamia tu .
Chamsingi sio kumkejeli Rais
Hapa tuwaombe au tutafute namna ya kuirudisha bungeni
Baadhi ya vipengele vifutwe.
Rais Magufuli yeye ni mfuata sheria
Kuandika humu au kuropoka hovyo
Hakuta saidia ikiwa Sheria ile ipo

hivi wewe huwa unafikiria kwa kutumia makalio au?wakat muswada ule unajadiliwa sikuiona hii ID ikihoji kuhusu ubovu wa muswada!

kuna mtu hapa yuko juu ya katiba,kwa hiyo inatakiwa atamke tu ili [HASHTAG]#Maxencemello[/HASHTAG] aachiwe huru!

[HASHTAG]#MAXENCEMELO[/HASHTAG] is innocent!
 
Polycarp Isaya Urio

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
2,008
2,000
Wote tupige kelele kwanza kuwa Max aachiwe huru bila kujali hitilafu hiyo. Tusutane akishawekwa huru!
Alitakiwa kua nje siku ileile alipofikishwa mahakamani lkn bahati mbaya akishindwa kukidhi masharti dhamana.Ili atoke ni lazima akidhi masharti ya dhamana manake dhamana iko wazi.Hiyo hashtag haiwezi kumsaidia iwapo masharti ya dhamana yake hayatatimizwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom