Unafiki ni usaliti-huwezi niibia kura na kunipiga mabomu halafu nikifa ujifanye ulinipenda

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Ni ukweli niko kwenye majonzi makubwa sana ya kupotelewa na dada yangu kipenzi, mwanamapinduzi na mwanaharakati. Dada aliyejua jinsi ya kuunganisha watanzania kujiletea maendeleo. Dada aliyesema ukweli na kuutetea. Dada aliyewaonyesha wanawake walioduni kuwa wanaweza wajitahidi na kujituma. Dada aliyepigania haki na usawa bila kuchoka, dada ninakulilia sana na kamwe sinta kusahau. Ulale pema peponi Regia Mtema.

Mazishi yake yamekutanisha wengi, yametukumbusha mengi, yameliza wengi wengi. Ni utamaduni wa Mtanzania kusahau ya kale kwenye matatizo hasa misiba. Watanzania huzikana na kusaidiana kwenye matatizo mbali mbali na hili linatujengea udugu na undugu popote duniani wakutanapo Watanzania.

Unafiki unaofanywa na serikali ya sasa iliyoko madarakani ya kunyanyasa wananchi huku ikitamani wafe ili iendelee kuongoza halafu tukifa inajifanya inauchungu ni dhambi, dhihaka, na unafiki mkubwa sana.

Jk aliwatumia polisi kupiga mabomu na risasi mikutani na maandamano ya CDM ili wao na viongozi wao wafe kwani serikali yake haiwapendi, leo naona wanavaa nguo nyeusi kuombeleza wale wanaowapiga mabomu kila kukicha.

Waliwapinga kwa kauli zao na harakati zao leo ndio wa kwanza kuwalilia wakisema walikuwa mashujaa.
Walitamani wafe ili waendelee kuwa ikulu na majimboni mwao leo wote wanalia machozi ya kinafiki eti wanawakumbuka.
Simpendi mnafiki wala simtaki mnafiki, serikali haikuwa na nafasi na wanyonge wala haiwatakii mema ndio maana inawapiga mabomu ya machozi na risasi za moto ili tufe.

Vyanzo vya ajali zinazoua kila kukicha ni hujuma za serikali na watendaji wake. Siwapendi wanafiki wala siwahitaji.

Siasi za kutokuheshimiana na viongozi wasioheshimiana kuchekeana kinafiki ni janga kubwa sana. Leo anakupa mkono kesho anamwambia Mwema wapige mabomu wapeleke keko, wadhalilishe waumize, halafu wakiuwa wanakuja kujifanya wanauchungu sana. sipendi wanafiki siwahitaji.

Kifo cha dada yangu kinaweza kujenga Tanzania mpya, amekufa ili kuunganisha nchi, kifo chake kiwe mwanzo wa kuheshimiana na kuthaminiana kisiwe ndio mwanzo wa kuuwana.

Pasco usiwe mnafiki, JK amemdhalilisha sana Dr Slaa, anampiga mabomu, anamfungulia kesi kila kukicha anamkeli wakati akijua amemwibia kura. sina uhakika kama kweli Dr ana mkimbia ila ni sawa kutokutana na mnafiki.

Serikali ijenge jinsi ya kuwaheshimu viongozi wengine wasio wa serikali. Viongozi wa vyama vya siasa nao ni viongozi wana watu na majukumu.

Poleni wote na tuijenge Tanzania mpya bila wanafiki. Vijana hasa akina dada igeni mfano wa Regia Mtema kwa kumuenzi kwa ushujaa wake na utumishi wake.

Chief Mkwawa wa Kalenga Real Talk
 
Wanataka wadumu wao daima pole kwakuumia lakini hata wewe ukiwa juu ungefanya hivyo ili kujilinda
 
WaTZ ni wanafiki.

kwani wewe ni wa wapi mkuu? Kama watanzania ni wanafiki , na wewe ni Mtanzania obviously wewe ni mnafiki namba moja, tena baba lao. U can prove this by using a Sylogism.
I hate generalization.
 
wewe ndo mnafiki kikwete wapi amefungua mashtaka dhidi ya padiri 'mstaafu' slaa,lete ushahidi wapi kikwete kaiba kura acha kuropoka.Ni kweli anamkimbia anao aibu kwa yale aliyokuwa anayasema dhidi ya jk
 
Ni ukweli niko kwenye majonzi makubwa sana ya kupotelewa na dada yangu kipenzi, mwanamapinduzi na mwanaharakati. Dada aliyejua jinsi ya kuunganisha watanzania kujiletea maendeleo. Dada aliyesema ukweli na kuutetea. Dada aliyewaonyesha wanawake walioduni kuwa wanaweza wajitahidi na kujituma. Dada aliyepigania haki na usawa bila kuchoka, dada ninakulilia sana na kamwe sinta kusahau. Ulale pema peponi Regia Mtema.

Mazishi yake yamekutanisha wengi, yametukumbusha mengi, yameliza wengi wengi. Ni utamaduni wa Mtanzania kusahau ya kale kwenye matatizo hasa misiba. Watanzania huzikana na kusaidiana kwenye matatizo mbali mbali na hili linatujengea udugu na undugu popote duniani wakutanapo Watanzania.

Unafiki unaofanywa na serikali ya sasa iliyoko madarakani ya kunyanyasa wananchi huku ikitamani wafe ili iendelee kuongoza halafu tukifa inajifanya inauchungu ni dhambi, dhihaka, na unafiki mkubwa sana.

Jk aliwatumia polisi kupiga mabomu na risasi mikutani na maandamano ya CDM ili wao na viongozi wao wafe kwani serikali yake haiwapendi, leo naona wanavaa nguo nyeusi kuombeleza wale wanaowapiga mabomu kila kukicha.

Waliwapinga kwa kauli zao na harakati zao leo ndio wa kwanza kuwalilia wakisema walikuwa mashujaa.
Walitamani wafe ili waendelee kuwa ikulu na majimboni mwao leo wote wanalia machozi ya kinafiki eti wanawakumbuka.
Simpendi mnafiki wala simtaki mnafiki, serikali haikuwa na nafasi na wanyonge wala haiwatakii mema ndio maana inawapiga mabomu ya machozi na risasi za moto ili tufe.

Vyanzo vya ajali zinazoua kila kukicha ni hujuma za serikali na watendaji wake. Siwapendi wanafiki wala siwahitaji.

Siasi za kutokuheshimiana na viongozi wasioheshimiana kuchekeana kinafiki ni janga kubwa sana. Leo anakupa mkono kesho anamwambia Mwema wapige mabomu wapeleke keko, wadhalilishe waumize, halafu wakiuwa wanakuja kujifanya wanauchungu sana. sipendi wanafiki siwahitaji.

Kifo cha dada yangu kinaweza kujenga Tanzania mpya, amekufa ili kuunganisha nchi, kifo chake kiwe mwanzo wa kuheshimiana na kuthaminiana kisiwe ndio mwanzo wa kuuwana.

Pasco usiwe mnafiki, JK amemdhalilisha sana Dr Slaa, anampiga mabomu, anamfungulia kesi kila kukicha anamkeli wakati akijua amemwibia kura. sina uhakika kama kweli Dr ana mkimbia ila ni sawa kutokutana na mnafiki.

Serikali ijenge jinsi ya kuwaheshimu viongozi wengine wasio wa serikali. Viongozi wa vyama vya siasa nao ni viongozi wana watu na majukumu.

Poleni wote na tuijenge Tanzania mpya bila wanafiki. Vijana hasa akina dada igeni mfano wa Regia Mtema kwa kumuenzi kwa ushujaa wake na utumishi wake.

Chief Mkwawa wa Kalenga Real Talk

Ni kweli uliyoyasema tuache unafiki
 
nimeguswa naa hyo hoja kuna uonevu wa kupindukia kwa wapinzani ndio maana wanaonekana kama maadui. CCM inakesha ikifikiria namna ya kuua upinzani badala ya kufikiria namna ya kujenga nchi.
 
Back
Top Bottom