Unafiki na Uzandiki wa Migiro, Kinana na Nape

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Watatu hawa wa CCM wamekamilisha ziara yao ya kupiga picha katika mikoa mitatu kusini mwa Tanzania juzi. Baada ya hapo wameitisha kikao cha CC ya CCM na kuwashitaki na kuwahoji mawaziri kadhaa kutokana na "utendaji mbovu" walioshuhudia huko.
Huu ndio unafiki na uzandiki wa mapacha hawa watatu, na walichofanya ndio taswira halisi ya USANII wa CCM

1. Waheshimiwa hawa (hususani Kinana na Nape) walishazunguka maeneo mengine mengi ya Tanzania lakini mabovu ya huko waliyaona na kuyafumbia midomo

2. Watatu hawa kwa macho yao walishuhudia migogoro na matatizo makubwa ya ardhi Tanzania lakini hawajamgusa waziri mhusika, Mh. anna Tibaikuja

3. Waheshimiwa wameshuhudia matatizo makubwa ya rasilimali za taifa hususani uwindaji haramu, lakini hawajamgusa waziri mhusika, Mh Kagasheki

4. Waheshimiwa wanajua uozo mkubwa uliopo kwenye wizara ya mambo ya ndani; matatizo ya polisi, balaa la madawa ya kulevya, lakini hawajasema chochote kuhusu waziri Nchimbi

5. Wakuu hawa wameshuhudia matatizo makubwa yaliyopo kwenye sekta ya maji Tanzania, na wakiwa Mbeya waliambiwa kuna sh 1.5bn zililiwa na mkandarasi bila hatua kuchukuliwa, lakini wamemkalia kimya waziri wa maji!

6. Waheshimiwa hawa wanafahamu kuwa taswira ya Tanzania ilichafuliwa na kitendo kisicho cha kiuongozi cha waziri wa mambo ya nje kudai talaka EAC kwenye vyombo vya habari, lakini wanajifanya kama hayawahusu

7. Hivi ina maana hawa wakuu wa CC hawajaona ubovu kwenye wizara ya teknolojia na mawasiliano ambako watanzania wanazidi kupoteza hela kila siku kwa kuletewa ving'amuzi zisivyo na viwango?

Yapo mambo mengine mengi ambayo hawa wasanii wanajifanya hawajayaona. Ukweli ni kwamba hakuna tofauti kati ya Kinana na Mulugo, au Nape na Chiza, au Migiro na Kawambwa. Wote ni wale wale, watoto wa baba mmoja Kikwete na hata wapewe wao ikulu hakuna watakachofanya zaidi ya usanii.

Huu ni muendelezo tu wa mbinu dhaifu ya kujenga mtandao wa uraisi 2015, kwa kudhoofisha wasiokua kwenye kambi yao...
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom