Unafiki na Uongo Wetu Viongozi: Usiyoilamba Haikuwashi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki na Uongo Wetu Viongozi: Usiyoilamba Haikuwashi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Aug 7, 2012.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wasalaam,

  Kwa makusudi kabisa nitaendelea kuepuka kuzungumzia mambo magumu kwa Mtanzania wa kawaida kama vile utafiti wa gesi/mafuta, ofisi za ukaguzi Malaysia, jengo la ubalozi Marekani nk.

  Kwa mwananchi wa Kata ya Mabogini hayo ni mambo yaliyo mbali sana. Yanamuhusu ila kwake ni sawa na habari za utafiti wa viumbe wengine kwenye sayari nyingine.

  Nitasemea tu unafiki na uongo wetu viongozi. Na kuhusu viongozi kwa kiasi fulani nawagusa wasomi ambao pia kwa njia moja au nyingine wanawaongoza wale ambao hawakuwa na nafasi kama yetu ya 'kusoma'.

  Tutaongolea kuhusu mgomo wa Madaktari na huduma mbovu katika mahospitali lakini sisi hatukanyagi huko kutibiwa. Tunaenda kwenye ziara kuangalia. Hata kukiwa na mgomo hautugusi ingawaje tutajidai tunawasupport madaktari.

  Madereva wa Hiace na mabasi wakigoma sisi tutatumia magari yetu na watoto wetu watapelekwa shuleni kwa school buses. Walimu wao hawajagoma kwa sababu hawana matatizo kama ya walimu wa shule za umma.

  Ni viongozi hao hao watajidai kupigia kelele sheria za mifuko ya jamii wakati asilimia 90 ya viongozi wote hawalipi makato ya wafanyakazi wao. Ni viongozi wangapi wanawalipia madereva, wasaidizi wa nyumbani, makarani asilimia 10 ya mwajiri? Au ni watu gani watazeeka kwa majonzi kama wale ambao tayari ujana wao ni mateso?

  Asilia zaidi ya 70 ya viongozi ni viongozi kwa sababu zao binafsi na sio maslahi ya umma. Wengi siasa ni ajira. Njia ya kupatia kipato aidha kwa posho halali au kwa njia za udanganyifu!

  Tukiacha hayo yote, maendeleo ya nchi yetu hayatafikiwa siku za usoni. Wengi tunashuhudia 'vita za uraisi'. Kila mara utasikia nani Raisi 2015 au hata 2020. Hakuna anayejali na Mwenyekiti wa Kijiji 2014. Hakuna chama chochote kinachoweza kujisifu kwamba kina mkakati wa kuimarisha nafasi hiyo muhimu kabisa kuliko hata nafasi ya uraisi!

  Kuna maana gani kutaka nafasi ya Uraisi wakati nafasi za Wenyeviti wa Vijiji na Udiwani hazina watu ambao ni viongozi thabiti na wenye uwezo?

  Kila mtu anajipanga kugombea ubunge na uwakilishi! Kuteuliwa Mbunge wa Viti Maalum au kuwa Waziri. Lakini mamlaka za chini zitaendelea kuwa legelege. Halmashauri zetu kila mtu anaziona! Mipango na mikakati mingi ila utekelezaji hamna.

  Wito wangu kwa wote, ni lazima tuchukue hatua na kuanza kujenga mamlaka za kiungozi kuanzia chini. Kuanzia kuwa kiongozi bora wa familia yako hadi ngazi ya Taifa. Wote tukikimbilia kuwa wabunge hakuna tutakachofanikiwa kama Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji (na Serikali za Mitaa) hawana uwezo.

  Siasa zinatuponza sana! Sana!
   
Loading...