Unafiki na siajabu Uongo Gesi ya Rostamu kuzuiwa Kenya!

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,398
8,885
Nimesoma mahali kwamba sijui hiyo inayoitwa gesi ya Rostamu kuzuiwa kuwekeza nchini Kenya, kwangu mimi huu ni usanii na naweza hata kwenda mbali kusema kwamba labda ni Uongo mkubwa na kuna vitu hawasemi.

Raisi Samia na raisi wa Kenya wanaelewana sana na hata walikuwa pamoja juzi kati Arusha na wamefungua barabara pamoja, iweje ashindwe kumzungumza raisi wa Kenya kwenye hilo swala kama ni kweli? Rostamu alikuwemo kwenye ziara ya raisi nchini Kenya na hata ile ziara kubwa ya USA Rostamu alikuwemo ina maana wako karibu sana na walisaini Mikataba tukaona picha Rostamu na raisi akiwa pembeni, iweje raisi ashindwe kumpigania ishu kama hiyo ?
 
Nimesoma mahali kwamba sijui hiyo inayoitwa gesi ya Rostamu kuzuiwa kuwekeza nchini Kenya, kwangu mimi huu ni unafiki na naweza hata kwenda mbali kusema kwamba ni Uongo mkubwa na kuna vitu hawasemi.

Raisi Samia na raisi wa Kenya wanaelewana sana na hata walikuwa pamoja juzi kati Arusha na wamefungua barabara pamoja, iweje ashindwe kumzungumza raisi wa Kenya kwenye hilo swala kama ni kweli? Rostamu alikuwemo kwenye ziara ya raisi nchini Kenya na hata ile ziara kubwa ya USA Rostamu alikuwemo ina maana wako karibu sana na walisaini Mikataba tukaona picha Rostamu na raisi akiwa pembeni, iweje raisi ashindwe kumpigania ishu kama hiyo ?
Kenyatta ni rais asiye na meno kwa sasa.
Anachokifanya ni kuaga marais waliobaki.

Halafu sijajua mleta mada wewe unautafsiri vipi "unafiki"
Naona kama hilo neno umelitamka vibaya kwenye andiko lako
 
Yani ulitegemea Samia na Kenyata wapigane ngumi ndio uamini kama wakenya ni wakora?
 
Wakati mwingine haya mambo yanafanywa na wasaidizi bila kiongozi kujua au kuwapa maelekezo, usishangae kitu hapo.
 
Wakati mwingine haya mambo yanafanywa na wasaidizi bila kiongozi kujua au kuwapa maelekezo, usishangae kitu hapo.

Lakini Raisi wa Tanzania angeshindwaje kumzunguza raisi wa Kenya ? Rostamu kuzuiwa kuwekeza nchini Kenya unataka kuniambia Raisi Samia atakuwa hajui? Au Rostamu ameshindwa kumfikia raisi Samia na kumwambia ?
 
Back
Top Bottom