Unafiki huu wa wanasiasa hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unafiki huu wa wanasiasa hadi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bbukhu, Oct 5, 2012.

 1. b

  bbukhu Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]UNAFIKI HUU WA WANASIASA WETU HADI LINI?[/h]
  Mwaka 2008, baada ya kuibuka kwa kashfa ya kampuni hewa ya richmond, watanzania tuliamini kuwa ukombozi wa kweli umepatikana kwani wabunge wengi walionesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujadili kuhusu kashfa ya richmond na kuunda kamati teule kuchunguza kampuni ya richmond. Kamati teule baada ya uchunguzi, ilibaini kuwa kampuni ile ilikuwa hewa au ya mfukoni. Wabunge wengi wakatoa machozi yao kuonesha uchungu walionao kwa rasilimali ya wananchi wa tanzania.
  Mfano wabunge kama vile: Anne kilango, Samwel Sitta, Harrison mwakyembe, na wengine wengi walichukizwa sana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond.
  Imani ya watanzania kuwa wabunge wao ni wazalendo, ilianza kufifia baada ya kugundua kuwa kashafa mbalimbali za ufisadi zilizokuwa zikiibuliwa ikiwamo hii ya richmond hazikushughulikuwa. Imani hiyo ilitoweka kabisa mwaka jana baada ya wabunge walewale wa ccm ambao mwaka 2008 walionesha uzalendo kwa kuchukia ufisadi, kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 bila kujali matakwa ya watanzania. Tuliona kuwa wabunge wa chadema na nccr mageuzi walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge ili kupinga muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba,wale wa ccm wakaanza kuupitisha kwa mbwembwe nyingi huku wakionesha madharau kwa wabunge wa upinzani. Hapo ndipo tulipobaini kuwa wabunge wetu ni wanafiki wakubwa kwani wanapuuza matakwa ya wapiga kura wao. Ajabu mwaka huu mwezi wa pili mheshimiwa rais pamoja na kusaini ule muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mwaka jana akawasilisha mabadiliko ambayo wabunge wa chadema waliyataka. Wabunge wa ccm walichukia sana kitendo kile kwani mwaka jana wapinzani walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge kupinga muswada huo, wao waliwacheka kwa hiyo ilikuwa aibu kubwa kwao. Haikutegemewa kabisa kuwa wabunge kama akina Kilango na wenzake waliokuwa wakitoa machozi bungeni kutokana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond leo wangekuwa mstari wa mbele kutetea mambo ambayo hayana maslahi kwa umma. Hii inaonesha ni jinsi gani wanasiasa wana ndimi mbili. Yaani unafika uliokithiri. Unafiki huu hadi lini?
   
 2. p

  pazzy Senior Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli baadhi ya wanasiasa ni wanafiki hasa wanapojifanya wazalendo mbele ya vyombo vya habari lkn matendo yao ni hatari...!mimi kama mtanzania sikulizika nakufungwa kwa mjadala wa richimond kwa dhambi hii sitakuja kumuunga mkono waziri wa jumuia ya afrika mashariki,pia kitendo cha Mh spika Anna.s.makinda kushindwa kusimamia utekelezaji wa maazimio ya bunge ni usariti kwa UMA...pia aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge Iliyochunguza sakata la richimond ambaye sasa ni waziri wa uchukuzi amepoteza thamani mbele ya moyo wangu kwa kuficha baadhi ya maovu waliyoyagundua! naamini maovu yote yaliyofichwa ndio matatizo sugu ya tanesco leo hii,kila umeme unavyokatika ndio chuki kwa watu hawa Inavyoongezeka...binafsi nawaombea maisha marefu Ili mje muione tanzania mpya 2015!
   
Loading...